Wakuu,ninakerwa sana na umasikini na ukosefu wa ajira uliopo kwa sasa.Hali hii itaondoka kwa kubadilisha mfumo mzima wa uongozi na utawala.Swali mfumo wa uongozi na utawala utaondokaje bila kua na Tume Huru ya Uchaguzi?Tume ya sasa,inaongozwa na mtaafu ambaye maisha ameshayapita,pia ameteuliwa na kiongozi wa chama tawala.Wakurugenzi wa wilaya,maafisa watendaji wa wilaya wa chama tawala ndio pia husimamia chaguzi zetu Tanzania.Tumeahidiwa draft ya katiba mpya 2014,muda hautatosha kuipitisha kwa kura za maoni na kuitumia 2015.Haitawezekana kua na chaguzi huru na haki wakati tume imechaguliwa na chama kimojawapo.Ni sawa na timu ya mpira,uwanya wako,refa wako halafu ushindwe mechi,sii rahisi.Wengi tunawaza na kuongea kishabiki sana ooh 2015 CCM kwisha,lakini kauli hizi hazitawezekana bila kuwa na Tume Huru