Mwongozo wa CCM kuhusu Katiba Mpya wakwamisha Tume Huru ya uchaguzi na Mgombea Binafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwongozo wa CCM kuhusu Katiba Mpya wakwamisha Tume Huru ya uchaguzi na Mgombea Binafsi

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mikael P Aweda, Sep 17, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Wiki kadhaa zilizopita mtu moja alinipa mwongozo wa ccm kuhusu katiba mpya ulioandaliwa Dodoma na wajumbe waliotajwa hapo chini; Nimescan, kisha nikajaribu ku upload nimekwama, japokuwa nisingweza ku upload kurasa zote kwa kuwa una kurasa 27. Hata hivyo, nimewaandikia hoja mbili tu kati ya nyingi kwa ajili ya kuchokoza mjadala wakati ninaomba mwongozo wa jinsi ya ku upload kutoka kwa wataalam wa IT. Sijajua kama tatizo ni laptop yangu au kitu kingine. Ifahamike hoja mbili zilizoandikwa hapo chini nimecopy na kupaset. Sijabadilisha hata nukta wala koma.

  NB; Kwa wale mlioangalia ITV waliporusha live kongamano la Katiba mpya yule mwanasheria wa ccm alizunguzia mwongozo wa ccm. Aliyasema yako humu kama alivyosema ila hakuzungumzia maeneo nyeti katibsa.
  1)Mh.Andrew Chenge (MNC) (MB) -Mwenyekiti
  2) Ndg Abdulrahaman O Kinana ( MNEC) Mjumbe
  3)Mh Jenista Mhagama (MNEC) (MB) Mjumbe
  4)Ndg Vuai Ali Vuai (MNEC) (MB) Mjumbe

  5)Kingunge Ngumbalu Mwiru ( MNEC) Mjumbe
  6)Machano Othaman ( MNEC) Mjumbe
  7)Mh. Kidawa Hamid Saleh Mnec (MNEC) (MB) Mjumbe
  8)Ndg Francis K. Mwonga Secretariet
  9)Ndg Benedict E Lyamuya Secretariet – katibu
  10)Ndg Salum Kh. Reja - Secretariet
  [TABLE="class: MsoTableGrid"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"][/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]HOJA[/TD]
  [TD]Uchambuzi wa Chama
  [/TD]
  [TD="width: 170, bgcolor: transparent"]Tafakuri ya Chama.[/TD]
  [TD="width: 264, bgcolor: transparent"][/TD]
  [TD="width: 280, bgcolor: transparent"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 42, bgcolor: transparent"]E[/TD]
  [TD="width: 170, bgcolor: transparent"]Utaratibu wa uteuzi wa Tume huru ya Uchaguzi[/TD]
  [TD="width: 264, bgcolor: transparent"]i)Muundo wa Tume ya Uchaguzi kwa sasa unazingatia matakwa ya ibara ya 74 ya jamhuri ya Muungano, ambayo inatoa madaraka kwa Rais, kumteua mwenyekiti wa Tume na wajumbe wengine wanaotajwa katika sheria husika
  ii) Wapo baadhi ya watu wanaohoji muundo huo na kudai kuwa, hauzingatii uwakilishi wa vyama vya siasa na kwamba wajumbe wake huteuliwa na Rais, ambaye pia ni kiongozi wa chama cha siasa kinachotawala. Kwa sababu hiyo, wajumbe wa Tume katika utendaji wao wa kazi ama watakuwa na upendeleo kwa chama husika au watakuwa wanalipa fadhila.
  iii) Wenye hoja hii wanapendelea kuwe na ama uwakilishi wa vyama vya siasa au kuwe na Chomba kitakachochuja majina ya wajumbe wa Tume kabla ya Rais kuwateua.[/TD]
  [TD="width: 280, bgcolor: transparent"]Kwa kuzingatia dhamana kubwa aliyonayo Rais wa Nchi kikatiba, ya kuwateua hata majaji, ni muhimu Rais akawateua pia wajumbe wa Tume ya Uchaguzi. Hata hivyo, ili kuimarisha uongozi wa Pamoja katika nchi yetu, sasa ni wakati muafaka wa kuanzisha utaratibu utakaoshirikisha Bunge katika uteuzi wa baadhi ya vyombo ya utendaji ikiwemo Tume huru ya Uchaguzi.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 42, bgcolor: transparent"]f[/TD]
  [TD="width: 170, bgcolor: transparent"]Suala la Mgombea binafsi[/TD]
  [TD="width: 264, bgcolor: transparent"]Yapo maoni ya baadhi ya watu kwamba, ipoa ha ya kuruhusu wagombea binafsi katika uchaguzi wa Urais, wabunge, Wawakililshi na madiwani bila kuwa wanachama au kupendekezwa na vyama vya siasa. Hoja yao ni kwamba, kutomruhusu kutomruhusu mgombea binafsi ni kumnyima haki yake ya kikatiba ya kushiriki katika shughuli za utawala wan chi na kuwanyima watu wengine haki ya kuchaguliwa ambao siyo wanachama wa chama cho chote cha siasa.[/TD]
  [TD="width: 280, bgcolor: transparent"]Wananchi sio tu wanayo haki ya kuchagua viongozi wao kwa njia ya kidemokrasia bali vile vile wanastahili kufahamu na kupima itikadi , sera na dira ya wale wanaotaka kuwaongoza.
  Aidha, Lengo la kuanzishwa vya kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ni kushindanisha vyama na sio watu binafsi katika uchaguzi wa vyombo vya dola. Kuruhusu mgombea binafsi ni sawa na kuweka rehani uhuru na maendeleo ya wananchi na pia ni kudhoofisha nidhamu katika vyama vya siasa. Hata hivyo, endapo katika mjadala wananchi walio wengi watapendelea katiba iruhusu mgombea binafsi ni vyema yawekwe masharti maalumu ambayo mgombea binafsi ni lazima ayatimize.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  My take,
  CCM hawako tayari kuja katiba mpya kwa sababu;
  Hawataki mgombea binafsi kwa kuweka masharti maalum kwa mgombea binafsi. Maalum ukiangalia wanalenga kuweka masharti magumu ambayo ni sawa na kukataa.
  Pili, hakutakuwa na tume huru kwa wajumbe wake kuteuliwa na Rais na kupitishwa Wabunge ambao kimkakati inajulikana kuwa wengi wao ni wanaccm.
  Hapa naanza kuamini kwamba katiba mpya inaweza kuwa Changa la Macho, It might be just my faithlessness.

   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Duuuuuuuu hakuna kulala mpaka kieleweke kama mbwai mbwai ngoma mpaka The Hague wapi mtikila?
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mwizi unapompa mamlaka ya kujiukumu unategemea nini..? CCM inajua wazi kuruhusu mgombea binafsi, ni mwisho wa uhai w chama chao, amini watu kama sita, membe, mwandosya, mwakyembe, watakuwa wa kwanza kugombea ugombea binafsi kwani hawana sababu ya kubebwa na vyama vyao
  na ugombea binafsi means mwisho wa michango ndani ya vyama kwani wengi watasimama bila vyama
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tume 'huru' ya uchaguzi inaonekana kama ndoto! Sijaelewa wanamaanisha nini pale wanaposema... "Kwa kuzingatia dhamana kubwa aliyonayo Rais wa Nchi kikatiba, ya kuwateua hata majaji, ni muhimu Rais akawateua pia wajumbe wa Tume ya Uchaguzi".

  Huu ni utani mbaya sana! Bado wanataka nchi iongezwe kwa utashi wa mtu mmoja na sio mfumo.
   
 5. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
 6. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Wamesahau kwamba hata majaji tunataka wasiwe chini ya raisi. Pia wamesahau kwamba nchi sio yao tena.
   
 7. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Panga pangua, mgombea binafsi ni lazima kwenye Katiba Mpya! Idadi ya Watanzania inatarajia kuvuka milioni 45(idadi kamili hadi itangazwe kisheria na TAKWIMU); wakati idadi ya wanachama wote wa vyama vya siasa haizidi milioni 10! Kwahiyo sisi tuliobaki takribani watu milioni 35 hatuwezi kutawaliwa na kundi dogo la watu milioni 10!
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Hii concept waliyonayo CCM ya kufikiria kuwa ni wao peke yao wanaojua wana uwezo wa kutuamulia kuwa yapi ni mazuri au yanatufaa Wanazania (whta is good for the Tanzanians) huwa inaniudhi sana.
   
 9. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  if you are not well informed about the position of Tanzanian on tume huru na mgombea binafsi anza leo kusoma gazeti la mwanchi column ya katiba mpya ndiyo utajua watanzania wanmsimamo gani!!!!!

  Kifupi ni kwamba mimi ni mmoja wa wasomaji wa hiyo column, nakutaarifu kwamba mambo haya yatabadilika kwani watu wengi sana wamekuwa-concerned, kuundwa kwa tume huru, na pia wengi wanataka mgombea binafsi, hawataki wakuu wa wilaya na mikoa, madaraka ya rais yapunguzwe, kuondoa viti maalumu na umilikaji wa ardhi.Haya kila kukicha wananchi wanayasemea.Anza kufuatilia utabaini mengi
   
 10. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Hii nchi hadi tuchapane bakora kwanza ndio mambo yatakwenda.
   
 11. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa majambazi bado tu wana imani ya kuendelea kutawala milele?
   
 12. k

  karim wade Member

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimechoka kusikia haya majina ya wajumbe kila siku chenge, kinana, kingunge. Hawa watu ni miungu midogo katika nchi hii? Je wana hati miliki na hii nchi? Elite group want to remain elite mpaka kwa wajukuu zao? NO!Jamani wake up tuchukue hatua imetosha.
   
 13. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,892
  Trophy Points: 280
  Ndio maana huwa nasema sisi washabiki na wanachama na wapenzi wa CDM tunaimani kuwa 2015 tutaiondoa CCM ila kwa kweli there is an uphill task, katiba safi vyombo vya dola kama police, usalama wa taifa na jeshi kuvivua u ccm na kuvivalisha uzalendo sio kazi ya mchezo, M4C iendelee ila pia tuanze ku focus namna gani ya kushinikiza kupata katiba safi tume huru ya uchaguzi na mazingira sawa ya ushindani wa kisiasa kinyume na hapo 2015 tutaendelea na hadithi za kuilamu tume, kulaumu polisi na usalama wa taifa wakati huo mafisadi wameshachukua nchi!
   
 14. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Unatarajia nini kipya toka kwa watu Kama Kingunge Ngombale Mwiru au Kinana wanaosubiri tu kufa? Hawa ndio waliotuletea katiba ya sasa na bado wanaaminiwa kuandaa mapendekezo ya Katiba mpya. Kwanini CCM iswatumie wanasheria wake kama kina Mwakyembe na kina Beno Malisa?
   
 15. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Labda hao wateuliwa wa huyu rais wao wagome kutangaza matokeo tu. Au labda wafanye mizengwe yao ili wasiitishe uchaguzi 2015. Lakini wwa hali yoyote CCM hawawezi furukuta wala kusalimika, OUT! Liwake, panyeshe lazima kutambazuka tu.

  Kwa ufupi nirudi kwenye mada.

  Ikumbukwe kuwa wote ,Kikwete na CCM, walidandia hoja ya mchakato wa katiba mpya. Hawakuwahi kuijadili wala hata kuifkiria kwenye ilani yao ya uchaguzi 2010 ambayo ndio dira wanayotekeleza sasa. Hivyo maoni yao na kutokujiandaa kwao kunadhirishwa na hoja dhaifu namna hiyo. Tena kuna spelling errors kibao, je ni Lusinde au Hizza ndiye aliyeihariri huo "mwogozo"?

  Toka mwanzo mchakato huu wa kisanii wa JK ulikosa vitu vingi vya msingi. Ndugu yetu MM Mwanakijiji aliandika uzi mmoja maridhawa sana na una michango mizuri yenye kujibu huu usani na udhaifu wa mchakato unaoendelea. Kwa ufupi HAKUNA KITU PALE.
   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #16
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Tuliliona hili mapema tujkaonya kuhusu 'utekaji nyara wa ajenda ya katiba mpya'.
  Haiwezekani CCM itawale miaka 48 halafu usiku mmoja waamke na kutaka katiba mpya.

  Kuna mahalai tuliponzwa kwa kuamini na kukabidhi watu ajenda nao wakaikabidhi kwingine.
  Tulitakiwa tushike usukani sisi wananchi.
   
 17. C

  Chipolopolo JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2013
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mgombea binafsi anaweza kusimamia hoja kwa maslahi ya waliomtuma,yaani wananchi, pasipo woga wowote tofauti na ilivyo sasa ambapo wagombea hulazimika kutimiza matakwa ya chama kwanza kulipo ya wananchi waliomtuma au akiwa na wazo ambalo hakubaliani na chama chake hawezi kulipinga kwa kuhofia kuwajibishwa kichama au kutoswa atakapo onyesha nia ya kugombea kupitia chama hicho husika. Mgombea binafsi ninaamini atatanguliza maslahi ya taifa kwanza ambayo ndiyo haswa lengo la wananchi.Vile vile itatoa nafasi kwa wagombea watakao toswa kwa fitna ndani ya chama kukata rufaa kwa wananchi ambao ndiyo waamuzi wa mwisho wa nani wanamtaka awe mwakilishi wao.Nina wasilisha.
   
Loading...