Mwongozo Toka Kamati ya Madaktari waliogoma kuhusu mwelekeo wa Mgomo

ALUTA CONTINUA DOCTORS.[QUOTE=chitage;3242145]
MWONGOZO:

STRIKE EXTENSION: MASAA 48 YA MGOMO KAMILI
Baada ya serikali kutoonesha niaya kutatua madai ya madaktari na kuendelea kupotushwa na baada ya mashaurianona mapendekezo ya madaktari wa miko mbalimbali, imeazimiwa kuanzia leo tarehe31/01/2012, kuongeza siku tatu za kutofanya kazi kufikia Ijumaa ya tarehe3/2/2012. Wakati huo huo tunaendelea kufungulia milango ya mazungumzo naserikali kwa kuwa tunatambua na kusikitikia hali mbaya ya wagonjwailiyosababishwa na mgogoro huu.

Je, Tutarudi nyuma kugeuka jiwela chumvi? Je tutarudi nyuma na kuendelea kupokea call allowance ya 10,000/=wakati hata stahiki yetu iliyoandikwa ya half per diem haijafanyiwa kazi? Je, tutarudi kule wananchiwanakokosa vitanda na kulala chini, kukkosa dawa hata kama zinawezekana, kuonawatoto, wakina mama na wazee wekiteketea kwa huduma duni zinazosemwa ni za burena hazipatikani? Ni kweli hatuwapendi Watanzania? Je nani atakayewatetea hawa?

Je Tutarudi nyuma bila kutimiziwahata nusu ya kile tunachostahili katika posho ya mazingira hatarishi (riskallowance)? Sisi tunafahamu ni madaktari wangapi katika kuhudumia wagonjwa, wanashatumia PEP na kupata side effects kalihuku tukiwa hatuna posho yeyote ya mazingira hatarishi.Hatuwezi rudi nyuma na kuadhibiwakwa chuki kali kutoka kwa watendaji wa wizara akiwemo yule Mtendaji Mkuu mwenyekiburi anyenyanyasa na kudharau watumishi wa afya hususan madaktari.

Pale vitisho vinapojitokea kutoka kwa ngazi zozote za dola ama waganga wakuu wambaonao watafaidika maradufu, posho na mishara ukiongezeka, tuvikatae vitishohivyo, hata kama inahitajika kusaini mkataba mara sita kwa siku, saini na usomemagazeti na majarida mbalimbali ya kukuimarisha. Tunadharauliwa madaktari kuwa hatujui stahiki zetu, sababu hatusomi, tutumie muda huu kusoma majarida nakukanusha taarifa chache za uoptoshaji kwenye forums na mijadala mbalimbali.

Ifahamike wazi taarifa na kauliza Mh. Waziri Mkuu zimeimarisha mtazamo hasi walio nao watumishi wa sekta yaafya kwa watendaji wa wizara. Ifahamike kuwa Mh. Waziri Mkuu hakujibu hoja za msingi na alitumia muda mwingi kusema mshahara hautekelezeki. Mh.Waziri Mkuu alitakiwa kutaarifiwa na Waziri wa utumishi kuwa mshahara tajwa nisttahiki ya madaktari kulingana na utafiti uliofanywa mwaka 1998na idara yautumishi kuwa uzito wa kazi ya madaktari ni sawa na senior managers katikautumishi wa umma ( REF civil service benchmark job grading evaluation ,finalreport 1998).

Sababu ya kuwa mshahara huo hautekelezeki , ofisi yake nautumishi walitakiwa kutamka watatoa ongezeko la kiasi gani kama ile iliotajwahaiwezekani.
Kwa kuwa mh. Waziri Mkuualikubali kupotoshwa na wasaidizi wake pamoja na watendaji wa wizara ya afya,muaaka wa suala hili unalekezwa sasa kwa Mh. Rais wa Jamhuri Ya Muungano waTanzania.

Ifahamike kuwa mgomo huu ni wamiko mbalimbali na ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa taarifa iliyochelewa wakatimaamuzi ya kikao yalishapita kumuomba Waziri Mkuu aonane nasi jumatatu. Wasaidizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu walelezwa kuwa madaktari kutoka mikoambalimbaliwanawasili Jumapili kuitikia mwitho wa Mh. Waziri mkuu. Ikumbukwe kuwa barua ya PM ilikuwa kwa ajili ya kuzungumza na madaktari wote walio kwenyemgomo na siyo wa Dar peke yake. Tunawashukuru madaktari na watumishi wote wa afya kwa umoja na mshikamano wanaoendelea kuuonesha.

Taarifazinazoenezwa sasa kwenye mitandao kuhusu kukutana kwa PM na Kamati, si zakweli. Ila inatarajiwa kuwa leo serikali itatoa tamko hapo baadaye kupitia kwaPM au Mh. Rais.
Kwa taarifa zote tarajiwa zaserikali, Kamati itatoa maamuzi ya mwisho kupitia mashauriano na madaktari.

Mungu Ibariki Tanzania.

Imetolewa na:
Kamati Kuu ya Mpito ya Jumuiya yaMadaktari
Kkwa niaba ya Madaktari wote, Tanzania.
[/QUOTE]
 
Hakuna sababu ya kurudi nyuma. Kurudi nyuma kwenu kutaleta athari kubwa kwa sekta ya afya na sekta nyingine nyingi.
Mshahara gani hautekelezeki? Hiyo miposho yao lukuki wanaojiongezea bila mpango, tena wengine kwa kulala tu bungeni mbona inasimamiwa kidete hata na huyo kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, aka mtoto wa mkulima? Madaktari wanapaswa kupata hali nzuri ya maisha. Hiyo kila mtu mwenye akili ataelewa. Eti wapewe elfu kumi, kisha wao wajiongezee malaki bila mpango. Kama ni kutumia vizuri kodi za wananchi, madaktari wanastahili, sio mijitu mingine kukwapua kisha kwenda kulala, badala ya kuwawakilisha hata waliowatuma.
 
Back
Top Bottom