Mwongozo Toka Kamati ya Madaktari waliogoma kuhusu mwelekeo wa Mgomo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwongozo Toka Kamati ya Madaktari waliogoma kuhusu mwelekeo wa Mgomo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chitage, Jan 31, 2012.

 1. c

  chitage Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 41
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  MWONGOZO:

  STRIKE EXTENSION: MASAA 48 YA MGOMO KAMILI
  Baada ya serikali kutoonesha niaya kutatua madai ya madaktari na kuendelea kupotushwa na baada ya mashaurianona mapendekezo ya madaktari wa miko mbalimbali, imeazimiwa kuanzia leo tarehe31/01/2012, kuongeza siku tatu za kutofanya kazi kufikia Ijumaa ya tarehe3/2/2012. Wakati huo huo tunaendelea kufungulia milango ya mazungumzo naserikali kwa kuwa tunatambua na kusikitikia hali mbaya ya wagonjwailiyosababishwa na mgogoro huu.

  Je, Tutarudi nyuma kugeuka jiwela chumvi? Je tutarudi nyuma na kuendelea kupokea call allowance ya 10,000/=wakati hata stahiki yetu iliyoandikwa ya half per diem haijafanyiwa kazi? Je, tutarudi kule wananchiwanakokosa vitanda na kulala chini, kukkosa dawa hata kama zinawezekana, kuonawatoto, wakina mama na wazee wekiteketea kwa huduma duni zinazosemwa ni za burena hazipatikani? Ni kweli hatuwapendi Watanzania? Je nani atakayewatetea hawa?

  Je Tutarudi nyuma bila kutimiziwahata nusu ya kile tunachostahili katika posho ya mazingira hatarishi (riskallowance)? Sisi tunafahamu ni madaktari wangapi katika kuhudumia wagonjwa, wanashatumia PEP na kupata side effects kalihuku tukiwa hatuna posho yeyote ya mazingira hatarishi.Hatuwezi rudi nyuma na kuadhibiwakwa chuki kali kutoka kwa watendaji wa wizara akiwemo yule Mtendaji Mkuu mwenyekiburi anyenyanyasa na kudharau watumishi wa afya hususan madaktari.

  Pale vitisho vinapojitokea kutoka kwa ngazi zozote za dola ama waganga wakuu wambaonao watafaidika maradufu, posho na mishara ukiongezeka, tuvikatae vitishohivyo, hata kama inahitajika kusaini mkataba mara sita kwa siku, saini na usomemagazeti na majarida mbalimbali ya kukuimarisha. Tunadharauliwa madaktari kuwa hatujui stahiki zetu, sababu hatusomi, tutumie muda huu kusoma majarida nakukanusha taarifa chache za uoptoshaji kwenye forums na mijadala mbalimbali.

  Ifahamike wazi taarifa na kauliza Mh. Waziri Mkuu zimeimarisha mtazamo hasi walio nao watumishi wa sekta yaafya kwa watendaji wa wizara. Ifahamike kuwa Mh. Waziri Mkuu hakujibu hoja za msingi na alitumia muda mwingi kusema mshahara hautekelezeki. Mh.Waziri Mkuu alitakiwa kutaarifiwa na Waziri wa utumishi kuwa mshahara tajwa nisttahiki ya madaktari kulingana na utafiti uliofanywa mwaka 1998na idara yautumishi kuwa uzito wa kazi ya madaktari ni sawa na senior managers katikautumishi wa umma ( REF civil service benchmark job grading evaluation ,finalreport 1998).

  Sababu ya kuwa mshahara huo hautekelezeki , ofisi yake nautumishi walitakiwa kutamka watatoa ongezeko la kiasi gani kama ile iliotajwahaiwezekani.
  Kwa kuwa mh. Waziri Mkuualikubali kupotoshwa na wasaidizi wake pamoja na watendaji wa wizara ya afya,muaaka wa suala hili unalekezwa sasa kwa Mh. Rais wa Jamhuri Ya Muungano waTanzania.

  Ifahamike kuwa mgomo huu ni wamiko mbalimbali na ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa taarifa iliyochelewa wakatimaamuzi ya kikao yalishapita kumuomba Waziri Mkuu aonane nasi jumatatu. Wasaidizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu walelezwa kuwa madaktari kutoka mikoambalimbaliwanawasili Jumapili kuitikia mwitho wa Mh. Waziri mkuu. Ikumbukwe kuwa barua ya PM ilikuwa kwa ajili ya kuzungumza na madaktari wote walio kwenyemgomo na siyo wa Dar peke yake. Tunawashukuru madaktari na watumishi wote wa afya kwa umoja na mshikamano wanaoendelea kuuonesha.

  Taarifazinazoenezwa sasa kwenye mitandao kuhusu kukutana kwa PM na Kamati, si zakweli. Ila inatarajiwa kuwa leo serikali itatoa tamko hapo baadaye kupitia kwaPM au Mh. Rais.
  Kwa taarifa zote tarajiwa zaserikali, Kamati itatoa maamuzi ya mwisho kupitia mashauriano na madaktari.

  Mungu Ibariki Tanzania.

  Imetolewa na:
  Kamati Kuu ya Mpito ya Jumuiya yaMadaktari
  Kkwa niaba ya Madaktari wote, Tanzania.
   
 2. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  aluta continua!!!!
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  huduma kwa wazee ni bure.je kuna fungu lolote lililopelekwa kwa halmashauri nchini ili kuhudumia mzigo huu ?matokeo yake wagonjwa wanakosa vitu na kuhisi wahudumu wa afya ni wachakachuaji.unaposema huduma bure kwa wajawazito,watoto,wazee una maana huduma za afya ni bure kwani haya ndio makundi yanayoumwa mara kwa mara.je baketi ya serikali inaliangalia hili?jibu ni hapana na tunabaki kusubiri misaada.hali za hospitali ni mbaya,leo hii mbunge anaongezewa posho kwa nini tukae kimya?
   
 4. U

  Utubora Senior Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  huu ni upepo wa mabadiliko , utavuma tu hata wabane kiasi gani!
   
 5. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Toa hili tamko katika mpangilio tulisome kwa urahisi

   
 6. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono mgomo japo naweka rehani maisha yangu lakini najua Mungu atatujalia kipindi hichi tusiumwe magonjwa makubwa.......
  Endeleeni mpaka kieleweke
   
 7. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Ukitaka uonekane mbaya dai chako,ukitaka kumuua nyani usimtizame usoni sasa madaktari wanadai chao wanaonekana wabaya nini kifanyike wakitaka kufanikiwa ktk azma yao wasigeuke nyuma mpaka watakapopata chao.
   
 8. Dr Klinton

  Dr Klinton Senior Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja hawa magamba kwa propaganda hawa washenzi now they are preparing grounds for next ambush
  But we wont retaliate,

  Stupid Regime

  Na mpaka sasa hii serikali sio halali kwani imeua sana wananchi bila ya huruma
  Na sisi haturudi kazini watufukuze tukae kitaaa

  f**K em all Bastards
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  pinda nakushauri umuone profesa kisali pale muhimbili akupe profile ya huyu mtu aliyepost hii thread halafu uwatangazie watanzania.this guy is damn smart!!
   
 10. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kwanini?
   
 11. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  mungu awabariki madaktari.....mungu awatie akili viongozi wa taifa wasiwe na kiburi na wawasikilize kwani hoja zenu ni za msingi.....

  na hiklo liendelee katika kadre zote profession isipokuwa za TISS
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Jaribuni kusoma hivyohivyo.......nimejaribu Ku-edit kidogo.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Herufi kubwa bila ya shaka n kwa sababilu ya kuposti jwa simu. Watajifunza polepole. Madaktari wapeabe taarifa kupitia jf
   
 14. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,214
  Likes Received: 10,558
  Trophy Points: 280
  serikali ya kishenzi....x 100 na PM ni mshenzi wa tabia kakomaa uso kaa nyani.
  haturudi nyuma madactari.
   
 15. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  huu 'msamiati hapo kwenye red kusema kweli siuelewi!

  Hivi hawa watu tunawaingiza ofisini ili wategemee washauri!?? Maana nadhani hata kama una mshauri inabidi kuwepo na mambo yale ya msingi inabidi kiongozi ayafikirie mwenyewe alafu washauri wajazie jazie 'nyama'.

  Hivi fikiria pale rais anaposaini muswada ambao watu wengi na vyombo vya habari vimepiga kelele kuwa una makosa, na baada ya week rais huyo huyo anaibuka na kusema "nimekuwa misled na washauri"!!

  Kweli PM kwa umri alionao na nyadhifa alizoshika anahitaji/alihitaji ushauri kujua kuwa wananchi tunazidiwa na kufa mahospitalini kwa sababu ya mgomo huu!? Na vitisho alivyotoa ilikuwa ni uhalisia wake au 'alishauriwa'!?

  Wakubali tu kuwa wameshindwa kuongoza nchi na wanachofanya ni kutumia rasilimali zilizopo KUTAWALA. Madaktari ni sehemu ndogo tu ya matatizo na ni kwa sababu ya upeo wao wa kisomi ndio unawapa ujasiri ukilinganisha na akina Mgaya (TUCTA), Mkoba (CWT) nk. Hongereni madaktari kwa kusimamia mnachokiamini

   
 16. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  hahahahaa!!!
  pole sana mkuu...........tupo pamoja.

  Hawa akili yao inaishia kwenye FFU, hawana akili nyingine.

  Vijana wakigoma pale UDSM, wanapelekewa FFU,
  Wananchi wakitaka kusema dukuduku zao, wanapelekewa FFU,
  Madaktari wamegoma, wameleka FFU Muhimbili........

  Hapondo mwisho wa akili yao.
   
 17. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  aluta continua.
   
 18. G

  Goodsize Member

  #18
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nndiyoo......! Naunga nkono asilimia mia..100%
  Njia hii ya madaktari kudai haki zao za kimsingi ni halali asilimia mia moja na ushee.
  Kwani wabunge walitumia njia halali kudai ongezeko la posho zao zilizoongezwa abundantly? Mbona baraka zote walipata!!
  ... Tz people tuamke, tunalala mno.
   
 19. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  niliwaona wajinga pale mlipokataa kwenda kuongea na waziri mkuu. was much more childish pale mpliposhindwa hata kuwasikiliza mwaziri wa afya na utumishi wa umma. Mwanzoni nilikuwa nanyi bega kwa bega lakini sasa mnaleta mambo ya kichuochuo. You need no behave like a graduate na si childish.
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Best wishes namsubiri yule puppet aje na mbwe mbwe zake
   
Loading...