Mwongozo ni vitu Gani vya kuzingatia unavyopelekwa mara ya kwanza kutambulishwa ukweni

Mimi na mai waifu tulikubaliana tuipige kihuni maana kwanza hatukua na hela ndio kwaanza tunaanza anza maisha. Yeye aliwaambia wazazi wake tu pamoja na kaka/dada baas! Hakukua na hata jirani au sijui shangazi alienusa. Mimi mwenyewe nikatimba peke yangu kwa miguu! Basi tukakaa na wazazi wake pale piga sana stori, vimaswali vya hapa na pale nk. Tukala cha mchana mida ya saa tisa tisa kumi nikasepa zangu utambulisho ndio ukawa umeisha ivyo.

Sherehe tulikuja kufanya siku wazazi wangu walipoenda kutambulishwa ukweni ndio na mimi nikaenda watu wengine wakanijua, tukatoa na mahari hapohapo ikabaki send off na harusi tu. Ukiwa na mke muelewa haya mambo ni simple sana.
Ni kweli mkuu hapo mkeo alikuokoa sana ila pia wazazi wake walikuwa waelewa.
Sehemu nyingine wazazi wake wanasema uende tu wakakuone ila ukifika utakachokutananacho hautakaa uamini.

Unaweza ukaanza kuwachukia tokea siku hiyo maana utakutana na mambo magumu ambayo haukuwa umejiandaa kukutananayo
 
Kwa kweliioo
 
Naombeni mwongozo huyu huyu mwanamke nilienae anahitaji nifike kwao akanitambulishe nyumbani,

Kama mnavyojua ukweni kabla ya kwenda kuna maandalizi ni lazima uyafanye ili usije ukaibika hivyo naombeni mwongozo washika dau mambo muhimu ya kuzingatia
Na vitu Gani vya msingi huwa familia wanapenda kuvisikia
Usianze kubishana na wakwe kuhusu mambo ya Simba na yanga.Hata akikwambia Yanga inaongoza ligi we suport tuu.cha pili ni pale kwenyw chakula ,mtatengewa chakula pekee enu wawili wewe na baba mkwe na nyama wataweka tatu wakati nyinyi mpo wawili ili wakupime kama unajua hesabu
 
kakodi gari kali uende nalo ukweni utanikumbuka heshima itakuwa juu baba mkwe hawezi kukuliza maswali ya kijinga jinga wala kukudharau nashauri kodi ata range au hammer oiga na suti yako kali ukiingia nayo ukweni wote watakuheshimu jifanye upo kwenye system serikalini na usikae nao sana kaa lisaa limoja tu mpange mshikaji akupigie ujifanye unahitajika dodoma kikazi aga sema unaelekea dodoma makao makuu una shughuli za kiserikali unawahi. ukifanya nilichokwambia wakwe hawatajishauri kukupa mke ata kesho ukaoe
 
Naombeni mwongozo huyu huyu mwanamke nilienae anahitaji nifike kwao akanitambulishe nyumbani,

Kama mnavyojua ukweni kabla ya kwenda kuna maandalizi ni lazima uyafanye ili usije ukaibika hivyo naombeni mwongozo washika dau mambo muhimu ya kuzingatia
Na vitu Gani vya msingi huwa familia wanapenda kuvisikia
Fanya vyote ila usisahau kunyoa upara. Ikiwezekana unyoe ile siku unaenda, ili uwe bado unang'aa.

Kama upo sehemu za baridi, hakikisha umeupaka mafuta. Ila kama ni sehemu za joto uache ubaki natural tu.
 
Tuma mshenga kwanza apeleke barua na ndani ya barua hiyo ambatanisha chochote kitu kadri ya uwezo wako.

Mshenga akipokelewa vizuri na akarudi na taarifa ya kupokelewa vizuri hapo sasa ndo utapeleka pua yako mkuu.
Mara nyingi mshenga huwa anapewa majibu ya kukubaliwa au kukataliwa, kama amekubaliwa baadhi huwa wanatoa mchanganuo wa vitu vyakwenda navyo wakati wa utambulisho + kutoa posa (hivyo vitu viwili ni kama mapacha)
Ila kabla hautajitokeza lazima ujue ni kabila gani la hao watu ambao unaenda kukutananao maana kila kabila lina mambo yake.

Pamoja na yote ujiandae na mazagazaga yakutosha
1. Mkaja wa mama.
2. Vitenge vya mashangazi
3. Blanket la bibi
4. Jembe
5. Panga.
6.koti la bahu
7. Fedha ikiwa ni sehemu ya mahali
Maana hamnaga utambulisho wa kienyeji tu bila kuambiwa swala la mahali
Nadhani muuliza swali ana maanisha utambulisho wa kawaida tuu,kabla ya hizo hatua zingineee.

Mwenye uzoefu wa kabila la wahaya anisaidie, Nadhani nime naswa rasmi na binti wa kihayaa
 
Usije ukafanya kosa ukaenda mikono mitupu, nakushauri kama una chini ya laki saba usitie miguu... Utaaibika!! Kwa mila nyingi za kibantu unapoenda kutambulishwa maana yake lazima ufuate taratibu za mahali, kutambulishwa sio kuona sura yako...
Jaribu kupeleleza vzr

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
Kwaiyo mkuu hapo sindio kutoa mahari kabisa unatoaje mahari hata hawajakujua vizuri
 
Kisa cha kujidanganya nafsi yako wakati unajijua kabisa kuwa hali yako ni tia maji? Be real, sidhani kama ni jambo zuri kuwadanganya wakwe zako kuhusu hali yako ya kiuchumi. Binti yao si amekupemda hivyohivyo bila kuwa na gari; na wakwe wacha wakupende na hali yako hiyohiyo. Uongo ni kitu kibaya sana
kakodi gari kali uende nalo ukweni utanikumbuka heshima itakuwa juu baba mkwe hawezi kukuliza maswali ya kijinga jinga wala kukudharau nashauri kodi ata range au hammer oiga na suti yako kali ukiingia nayo ukweni wote watakuheshimu jifanye upo kwenye system serikalini na usikae nao sana kaa lisaa limoja tu mpange mshikaji akupigie ujifanye unahitajika dodoma kikazi aga sema unaelekea dodoma makao makuu una shughuli za kiserikali unawahi. ukifanya nilichokwambia wakwe hawatajishauri kukupa mke ata kesho ukaoe
 
Vaa vizuri,usivae miwani ya aina yoyote ile, Kama ni mtumiaji wa pombe acha siku tano kabla hujatimba ukweni

Punguza maongezi ya simu ukiwa ukweni ikiwezekana zima kwa muda

Usioneshe hisia flani iwe movie au muziki,siyo unausikia wimbo wa Rayvani ule wa nyegezi ukaanza kutikisa kichwa

Punguza sifa,siyo watu wanagombana/pigana ukajifanya unawaamua utajuta

NB: akili za kuambiwa........
Yaani nisikie anachukua anaweka waaaah nisitikise kichwa
 
Vaa vizuri,usivae miwani ya aina yoyote ile, Kama ni mtumiaji wa pombe acha siku tano kabla hujatimba ukweni

Punguza maongezi ya simu ukiwa ukweni ikiwezekana zima kwa muda

Usioneshe hisia flani iwe movie au muziki,siyo unausikia wimbo wa Rayvani ule wa nyegezi ukaanza kutikisa kichwa

Punguza sifa,siyo watu wanagombana/pigana ukajifanya unawaamua utajuta

NB: akili za kuambiwa........
Hhahaha ukwebi hata ukisikia songi unalikubali kausha tu.
 
kakodi gari kali uende nalo ukweni utanikumbuka heshima itakuwa juu baba mkwe hawezi kukuliza maswali ya kijinga jinga wala kukudharau nashauri kodi ata range au hammer oiga na suti yako kali ukiingia nayo ukweni wote watakuheshimu jifanye upo kwenye system serikalini na usikae nao sana kaa lisaa limoja tu mpange mshikaji akupigie ujifanye unahitajika dodoma kikazi aga sema unaelekea dodoma makao makuu una shughuli za kiserikali unawahi. ukifanya nilichokwambia wakwe hawatajishauri kukupa mke ata kesho ukaoe
huu utapeli sasa
 
Fanya vyote ila usisahau kunyoa upara. Ikiwezekana unyoe ile siku unaenda, ili uwe bado unang'aa.

Kama upo sehemu za baridi, hakikisha umeupaka mafuta. Ila kama ni sehemu za joto uache ubaki natural tu.
mkuu umeua kabisa
 
Back
Top Bottom