Mwongozo ni vitu Gani vya kuzingatia unavyopelekwa mara ya kwanza kutambulishwa ukweni

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Naombeni mwongozo huyu huyu mwanamke nilienae anahitaji nifike kwao akanitambulishe nyumbani,

Kama mnavyojua ukweni kabla ya kwenda kuna maandalizi ni lazima uyafanye ili usije ukaibika hivyo naombeni mwongozo washika dau mambo muhimu ya kuzingatia
Na vitu Gani vya msingi huwa familia wanapenda kuvisikia
 
Cha muhimu ni muonekano wako tu.

1. Watakuthaminisha uvaaji wako. uvae kiheshima, Usivae mlegezo.
2. Uongeaji wako na wakwe uwe wa adabu, usijifanye mjuaji sana wa kila kitu.
3. Hata kama huna kazi, jifanye unajishughulisha na kazi fulani.
4. Kama bado unaishi kwa wazazi wako usiwaambie, jifanye unajitegemea kwenye Gheto lako
5. Siku ya kwenda usiwe peke yako. Ambatana na mshenga au mtu mwingine aliyekuzidi umri ili uonekane upo serious
6. Usiende kwa Baiskeli. Tafuta rafiki yako mwenye gali akusindikize na kama unaweza kuendesha gali, endesha wewe.
 
Anaenda kukutambulisha kwao kama nani, rafiki? Mchumba? Au?

Usije ukajipanikisha bure ukaanza kutafuta na watu wa kukusindikiza kumbe yeye anaenda tu kukutambulisha kwa mama yake ambae kila siku anamsumbua akulete akuone.

Kama ni utambulisho rasmi kwa maana ya mume mtarajiwa ndio uulize taratibu za huko kuhusu maswala ya nini kitafanyika na nyie mnatakiwa mjipange vipi wewe na team yako.
 
Vaa vizuri,usivae miwani ya aina yoyote ile, Kama ni mtumiaji wa pombe acha siku tano kabla hujatimba ukweni

Punguza maongezi ya simu ukiwa ukweni ikiwezekana zima kwa muda

Usioneshe hisia flani iwe movie au muziki,siyo unausikia wimbo wa Rayvani ule wa nyegezi ukaanza kutikisa kichwa

Punguza sifa,siyo watu wanagombana/pigana ukajifanya unawaamua utajuta

NB: akili za kuambiwa........
 
Cha muhimu ni muonekano wako tu.

1. Watakuthaminisha uvaaji wako. uvae kiheshima, Usivae mlegezo.
2. Uongeaji wako na wakwe uwe wa adabu, usijifanye mjuaji sana wa kila kitu.
3. Hata kama huna kazi, jifanye unajishughulisha na kazi fulani.
4. Kama bado unaishi kwa wazazi wako usiwaambie, jifanye unajitegemea kwenye Gheto lako
5. Siku ya kwenda usiwe peke yako. Ambatana na mshenga au mtu mwingine aliyekuzidi umri ili uonekane upo serious
6. Usiende kwa Baiskeli. Tafuta rafiki yako mwenye gali akusindikize na kama unaweza kuendesha gali, endesha wewe.

Mkuu umeiva
 
Mkuu hakikisha unakoenda usalama upo otherwise utakuja leta thread ingine, hapo fanya hvi mwambie mama awambie home then wakitaka kukuona tuma mshenga anaejielewa ikiwezakana upate na wa kabila lao wewe usiende, nenda siku ya kutoa mahari tu.

Ni kabila gani uyo dada tukupe nondo
 
Usije ukafanya kosa ukaenda mikono mitupu, nakushauri kama una chini ya laki saba usitie miguu... Utaaibika!! Kwa mila nyingi za kibantu unapoenda kutambulishwa maana yake lazima ufuate taratibu za mahali, kutambulishwa sio kuona sura yako...
Jaribu kupeleleza vzr

Sent from my Android using JamiiForums mobile app

Hana haja ya kwenda aende siku ya kutoa mahali tu, au posa
 
Naombeni mwongozo huyu huyu mwanamke nilienae anahitaji nifike kwao akanitambulishe nyumbani,

Kama mnavyojua ukweni kabla ya kwenda kuna maandalizi ni lazima uyafanye ili usije ukaibika hivyo naombeni mwongozo washika dau mambo muhimu ya kuzingatia
Na vitu Gani vya msingi huwa familia wanapenda kuvisikia
Tuma mshenga kwanza apeleke barua na ndani ya barua hiyo ambatanisha chochote kitu kadri ya uwezo wako.

Mshenga akipokelewa vizuri na akarudi na taarifa ya kupokelewa vizuri hapo sasa ndo utapeleka pua yako mkuu.
Mara nyingi mshenga huwa anapewa majibu ya kukubaliwa au kukataliwa, kama amekubaliwa baadhi huwa wanatoa mchanganuo wa vitu vyakwenda navyo wakati wa utambulisho + kutoa posa (hivyo vitu viwili ni kama mapacha)
Ila kabla hautajitokeza lazima ujue ni kabila gani la hao watu ambao unaenda kukutananao maana kila kabila lina mambo yake.

Pamoja na yote ujiandae na mazagazaga yakutosha
1. Mkaja wa mama.
2. Vitenge vya mashangazi
3. Blanket la bibi
4. Jembe
5. Panga.
6.koti la bahu
7. Fedha ikiwa ni sehemu ya mahali
Maana hamnaga utambulisho wa kienyeji tu bila kuambiwa swala la mahali
 
Mimi na mai waifu tulikubaliana tuipige kihuni maana kwanza hatukua na hela ndio kwaanza tunaanza anza maisha. Yeye aliwaambia wazazi wake tu pamoja na kaka/dada baas! Hakukua na hata jirani au sijui shangazi alienusa. Mimi mwenyewe nikatimba peke yangu kwa miguu! Basi tukakaa na wazazi wake pale piga sana stori, vimaswali vya hapa na pale nk. Tukala cha mchana mida ya saa tisa tisa kumi nikasepa zangu utambulisho ndio ukawa umeisha ivyo.

Sherehe tulikuja kufanya siku wazazi wangu walipoenda kutambulishwa ukweni ndio na mimi nikaenda watu wengine wakanijua, tukatoa na mahari hapohapo ikabaki send off na harusi tu. Ukiwa na mke muelewa haya mambo ni simple sana.
 
Back
Top Bottom