Mwongozo kusitisha shughuli zote za Bunge kujadili Mgomo wa waalim 30/07/2012

Wabunge wa ccm. Haiwezekani hawa wenzetu kushabikia mgomo hivi. Lazima wao ndo wame organize. Waalimu tuwapuuze hao. Ccm oyeee. Wabunge ccm vigelegele bungeni
 
mimi mgomo nilianza siku nyingi sema kesho nauendeleza tu mana toka nianze january hata topic mbili hazijafika.

Amin usiamin Mwl. walim wengi sana Tz walishagoma na ndo mana sasa matokeo ni mabaya mabaya kila siku.
serikali lazima imrudie mwl na kuongea nae vema ili mwl arudi darasani upyaaa.
 
Walimu wakigoma tunawachapa bakora tu. Tumewaweza madaktari itakuwa walimu?. Na pia tunaweza kuwafukuza kazi na watakuwa hawana pa kwenda. Vyeti vyao hata Malawi havitambuliki acha kenya. Nyie walimu acheni kufuata mkumbo, fanyeni kazi huku madai yenu yanashughulikiwa na Serikali.

Kama unamsema hivi Mwl wako.
Je unakumbuka hata mchango wake wakati hujui hata "a"
ila wa TZ kwa kukandia ni noma.
 
Walimu hamna umoja wenzenu wanaomba muendelee kugoma ili wao waitwe kazini.
 
Nimepita wilaya ya same kuelekea daa Nimefanikiwa kupita shule zilizoko karibu na barabara kuu. Shule za njoro, ishinde, majevu, kisima, makanya. Nkwini hakuna waalimu shuleni wanafunzi wametelekezwa
 
Kama kweli wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wanajali maslah na wapo kwaajili ya kutetea haki za wananchi wao. Tunaomba jumatatu 30/07/2012. SPIKA Asimamishe shughuli zote Na kujadili swala la mgomo wa waalimu. Aidha hatutarajii kusikia majibu ya kipumbavu kutoka kwa Spika wala Lukuvi wala Werema kudai kuwa Swala hili lipo mahakamani. Kimsingi swala ambalo limesha anza kusikilizwa mahakamani ndo halitakiwi kuzungumziwa. Hili la waalimu bado halijaanza kusikilizwa kwani juzi ijumaa mahakama ilitaka pande zote mbili zikapange hoja zake vizuri ili jumanne zipokelewe mahakamani. Leo ni jumatatu, kesho juma4 hoja za pande mbili ndo zitapelekwa mahakamani. Tunaomba bunge litimize wajibu wa kuisimamia serikali. Hoja hii ikikataliwa tunategemea kuwaona wabunge wa vyama vyote wakitoka Bungeni ili kutoa msimamo wao nje ya Bunge. Mama ana Makinda jiandae kususiwa Bunge kama huna utu na kama huna watoto wanaoathirika na mgomo huu

Hili suala liko mahakamani na halite jadiliwa, full stop !
 
Itabidi Bunge letu lisiwe na ratiba ya mikutano yake ili liwe linakaa kila siku kujadili mambo yanayotokea siku hyo.
 
kama ilivyo kawaida ya serikali kukimbilia mahakama kama chaka la kuficha uovu wao... unaendelea kwa kusingizia kesi ishafika mahakamani...
MAONI YANGU : naona mambo haya tusiyavumilie kabisa la sivyo tutaelekea pabaya
 
Hii nchi ina laana, sina hakika kama watawala wanalijua hilo, pengine wangetafuta suluhu mapema.
 
Si wamuulize awatajie ni kesi namba ngapi na inasikilizwa na hakimu gani na iko hatua gani,

halafu wanamlea huyo ndugai,
sisi wananchi hatukuwachagua wabunge kutuwakilisha halafu wawe wadogo mbele ya ndugai. Akikwambia kaa chini mwambie sikai chini, bunge si jeshi, kama vipi tualikeni kupitia hilohilo bunge, semeni hiviii "wananchi njooni tujazane mjengoni ndio hoja zenu zitasikilizwa" uone mwitikio na upuuzi wa ndugai na makinda utaishia hapo.
 
Wanalea tatizo mpaka litakapokuwa kubwa ndio wataamka na kuanza kujadili,Ndugai kaelekezwa tayari asiruhusu hoja yoyote ya walimu kujadiliwa.
 
Spika na Naibu siyo wa Bunge tena, Ni spika na naibu spika wa serikali hivyo Wabunge wamekuwa fuata upepo. Yawezekana Wah. Wabunge wanalijua hilo au la, lakini hivyo ndivyo hali ilivyo bungeni.
 
Si wamuulize awatajie ni kesi namba ngapi na inasikilizwa na hakimu gani na iko hatua gani,

halafu wanamlea huyo ndugai,
sisi wananchi hatukuwachagua wabunge kutuwakilisha halafu wawe wadogo mbele ya ndugai. Akikwambia kaa chini mwambie sikai chini, bunge si jeshi, kama vipi tualikeni kupitia hilohilo bunge, semeni hiviii "wananchi njooni tujazane mjengoni ndio hoja zenu zitasikilizwa" uone mwitikio na upuuzi wa ndugai na makinda utaishia hapo.
kaka hapo umenena maana ndugai na makinda wake wanatumika na serikali kupiga chini uozo wao...
NAKUMBUKA MSEMO WA KAMANDA MNYIKA: TUMEFIKA HAPA KWA SABABU YA UDHAIFU WA RAISI NA WASHIRIKA WAKE
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom