Mwongozo bora na vitu vya kuzingatia katika kuanzisha kuku wa mayai

theriogenology

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
8,750
15,639
MWONGOZO BORA WA KUKU WA MAYAI

Utangulizi

Kuku wa mayai wanafaida kubwa iwapo utawalea na kuwatunza vizuri. Kwa kawaida kuku anaekaribia kutaga (pullets) wanatakiwa kuwa na mifupa na misuli iliyokomaa ambayo itawawezesha kutaga mayai bila kupata tatizo lolote.

Na kwa kawaida kuku wanaokaribia kutaga wanatakiwa kuwa na uzito wa 1.5kg na pia wanatakiwa kuwa na afya na kizazi imara ambacho kitamwezesha kutaga vizuri bila kupata tatizo lolote.

Hivyo basi wewe kama mfugaji ni vyema kuzingatia vitu vifuatavyo ambavyo vitakuwezesha kuwalea vifaranga wako mpaka pale watakapoanza kutaga mayai.

1.1 Kabla ya vifaranga kufika

> Hakikisha banda au nyumba ya kufikia yapaswa kusafishwa na kunyunyiziwa dawa ili kuweza kuuua bakteria na wadudu wengine ambao hupelekea kuku kupata magonjwa. Na disifectant au dawa ya kusafishia banda unayotakiwa kuitumia ni JIK ambayo hupatikana kwa bei ya kawaida.
> Nyumba yapaswa kuachwa kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuwaweka vifaranga wako. Na kumbuka kuweka footbath katika mlango wa kuingilia bandani na hakikisha ina disfectant ambao utatumia kuloweka miguu yako kabla na baada ya kutoka bandani.
> Safisha vyombo na vifaa ambavyo utatumia katika kuwalea vifaranga wako kwa maji safi yaliyochanganywa na disfectant.
> Masaa matatu kabla ya vifaranga kuingia ndani weka chanzo cha joto ambacho chaweza kuwa jiko au bulb za 200 watts na hakikisha joto la banda lako linasona 35°C.
> Tengeneza brooder kwa kutumia ceiling board hakikisha lina mwonekano wa duara na kwa kawaida unaweza tengeneza brooder kwa kutumia ceiling ya futi mbili ambao itaweza kuwatunza vifaranga 300.
> Weka drinkers za kutosha katika brooder na hakikisha unawapa vifaranga wako maji yaliyochanganywa na glucose na kwa kawaida unashauriwa kuchanganya kiasi cha 1kg ya glucose kwa maji ya lita kumi.

1.2 Baada ya vifaranga kufika

> Hesabu vifaranga vyote kujua unaanza na kuku wangapi
> Weka vifaranga karibu na cahnzo cha joto.
> Waruhusu vifaranga kunywa maji kwa muda wa lisaa moja kabla ya kuwapa chakula.
> Wape vifaranga mwanga wa kutosha kwa kawaida inashauriwa kuwapa vifaranga mwanga kwa masaa 24 kwa muda wa wiki nne za mwanzo. Hakikisha joto liko sawa na epuka tofouti kubwa ya joto.
> Waweza tumia reflector kuruhusu mwanga wa kutosha kuwafikia vifaranga.
> Hakikisha unaongeza ukubwa wa eneo kadli vifaranga wanapokuwa wakubwa.
> Unaruhusiwa kutoa ceiling board ambayo iliyotumika kutengeneza brooder ifikapo siku ya kumi.

1.3 Uleaji wa vifaranga mpaka pale wanapoanza kukua

> Hakikisha unawapa vifaranga chakula cha kutosha, hapa nazungumzia chick mash kwa muda wa wiki nane na kwa kawaida kifaranga kimoja hula 2kg kwa wiki hizo tajwa hapo juu.
> Hakikisha kuku wanapata maji ya kutosha maji yawe safi na salama
> Hakikisha kuku wanapata eneo la kutosha na kwa kawaida kuku wakubwa watano wanaotaga wanahitaji eneo la 1m²
> Wape kuku wanaokua ( Growers) grower mash pale wanapofikisha umri wa wiki tisa mpaka pale wanapofikisha wiki ya ishirini na kwa kawaida kuku mmoja hula kilo 6 kwa wiki tajwa hapo juu.
> Wiki ya 16 anza kuweka vitagio katika banda la kuku ili kuku wanaotarajia kutaga ( pullets) waanze kuvizoea mapema.
> Anza kutunza kumbukumbu muhimu za gharama za chakula, mkaa/umeme pamoja na madawa na chanjo.
> Wiki ya 8 hadi 12 kumbuka kuwakata midomo

1.4 Kuzuia magonjwa

> Unashauriwa kutenganisha sehemu ya kulelea vifaranga na kukuzia ili kuepuka uenezaji wa magonjwa kutoka kwa kuku wakubwa kwenda kwa wadogo
> Zingatia usafi, hakikisha vyombo vya kulia na kunywea maji viko safi kila siku
> Waangalie kuku wako kama wana utitiri au chawa na kisha nyunyizia dawa kuwaua
> Kila siku hakikisha foitbath ina disifectant ya kutosha kuepeuka kuingiza magonjwa katika banda lako la kuku
> Usiingize kuku wa nje katika banda lako au kuruhusu kuku wa nje kusogelea banda lako
> Wape dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu baada ya kufikisha wiki nane
> Hakikisha ndani ya banda lako bedding materia haizidi usawa wa inch 4

1.5 Vitu vya kuzingatia kila siku

> Weka feeders za kutosha na hakikisha kuku wako wana nafasi ya kutosha.
> Hakikisha kuku wako wanapewa chakula kwa muda maalamu hapa namaanisha kama umezoea kuwapa chakula saa4 iwe hivyo kila siku tofouti na hivyo utawasababishia stress kuku wako
> Usipunguze idadi ya chakula kwa kuku wako
> Hakikisha wanapata maji safi na salama kila siku
> Hakikisha kuku wanapata mwanga wa kutosha kila siku unashauriwa kuwapa kuku mwanga kwa masaa14 kila siku.
> Kuku wapewe dawa ya minyoo kila mwezi
> Epuka stress ambayo hupelekea kuku kudonoana au kula mayai
>Kusanya mayai kila mara na uyahifadhi katika eneo salama
> Angalia wadudu kama wapo nyunyizia dawa
> Tunza kumbukumbu
> Anza kutoa kuku wasiotaga
> Anza mapema kutunza akiba kwa ajili ya kununulia kuku wengine ( Stock mpya)
> Kuwa na mzani nyumbani ambao utatumika kupimia chakula kabla ya kuwapa kuku.
> Kwenye kipindi cha kiangazi wape kuku vitamin kwenye maji.
> Tenga kuku wagonjwa hakikisha unawatibubwakiwa peke yao na pale wanapopona warudishe katika kundi la kuku wazima
> Kumbuka kuwapa kuku wako majani kila siku baada ya kuwapa chakula
> Na mwisho zingatia kuwakata mdomo pale wanapofikia umri wa wiki 8 mpaka 12.

1.6 Vitu vya kuzingatia wewe kama mfugaji

1.6.1 chanjo

> Kumbuka na fuata ratiba ya uchanjaji vizuri
> Kumbuka kutokutumia chanjo zilizokwisha muda wake ( expire)
> Hakikisha unahifadhi chanjo mahali salama
> Tumia maji ya mvua au maji yaliyochemshwa kwa ajili ya kuandaa chanjo ( usitumie maji ya bomba)
> Kumbuka kuwapa kuku vitamin kwenye maji baada ya chanjo.

1.6.2 Madawa

> Fuata maelezo ya dawa kwa kusoma vipeperushi vizuri kabla ya kutumia
> Usitumie dawa zilizokwisha muda wake
> Hakikisha hutumii mayai au nyama ya kuku baada ya kutumia dawa mpaka pale dawa itakapokuwa imeikwiasha mwilini ( withdraw period)
> Hakikisha unapotumia antibiotic nzito kwa kuku kumbuka kuwapa vitamini ili kuepusha stress kwa kuku

1.6.3 Nyumba ya kuku

> Hakikisha nyumba ni kubwa na ndefu kwenda juu pia iwe na madirisha makubwa yaliyoweka wavu (wire mesh) ili kuruhusu hewa ya kutosha kuingia bandani.
> Pia sakafu inatakiwa kutengenezwa kwa kutumia zege hii itawaepusha panya na pia itakuwa rahisi kusafisha na kunyunyizia dawa
> Ndani ya banda kuwekwe maranda ya mbao, mabaki ya mpunga au majani kuepusha baridi na unyevu unyevu ndani ya banda.
> Hakikisha eneo la kuku watano ni 1m²

1.6.4 Vifaa vya kuku

> Hakikisha unatumia feeder ya mita moja kwa kuku ishidini
> Drinker moja kwa kuku thelathini
> Chombo cha kutagia mayai cha 1ft X 1ft kwa kuku watano

7. Ratiba ya chanjo

> Siku ya saba chanjo ya Kideri ( Newcastle) dozi ya kwanza kwa njia ya tone kwa jicho
> Siku ya kumi na nne chanjo ya gumboro dozi ya kwanza kwenye maji
> Siku ya ishirini na moja chanjo ya kideri dozi ya pili kwa njia ya tone kwenye jicho
> Wiki ya nne chanjo ya gumboro dozi ya pili kwenye maji
> Wiki ya 8 Chanjo ya kideri dozi ya tatu kwa njia ya tone
> Wiki ya kumi na mbili chanjo ya ndui ( fowlpox) njia ni kwenye bawa
> Mwezi wa tano chanjo ya kideri dozi ya nne kwa njia ya tone kwenye jicho

Zingatia: Rudia chanjo ya kideri kila baada ya miezi mitatu na wape dawa za minyoo kuku wako baada ya kufikisha umri wa wiki 8 na rudia kila baada ya miezi mitatu.

8. Ratiba ya utagaji kwa kuku wa mayai

> Umri wa kutaga ni wiki ya kumi na sita
> wiki ya kumi na tisa asilimia 6 ya kuku hutaga
> wiki ya ishirini ni asilimia 20 ya kuku hutaga
> wiki ya ishirini na moja ni asilimia 50 ya kuku hutaga
> wiki ya ishirini na mbili ni asilimia 78 ya kuku hutaga
> Wiki ya 23-43 ni 90-93% ya kuku hutaga
> Wiki ya 44-60 ni 80-89% ya kuku hutaga
> Wiki ya 61-73 ni 70-79% ya kuku hutaga
> Wiki ya 73-80 ni 70-65% ya kuku hutaga na kadri siku zinapozidi kuongezeka na utagaji hupungua na ukiona hivyo ni vyema kujitayarisha kwa batch mpya....
 
Apa kwenye chanjo sijui ntachanganya mambo
Fanya hivi;

- Siku ya 7 wape chanjo ya mdondo/Kideri kwa njia ya maji au matone
- Siku ya 14 wape chanjo ya gumboro kwa njia ya maji
- siku 21 rudia chanjo ya mdondo/kideri kwa njia ya maji au matone

Zingatia: Baada ya siku 21, utarudia kuchanja kideri baada ya siku 90 ambayo ni sawa na miezi mitatu (3) na unakua unarudia hivyo kila baada ya miezi 3.

- Siku ya 28 rudia chanjo ya gumboro kwa njia ya maji.
- Wiki ya 6-8 chanja Ndui kwa njia ya sindano hii unachoma kwenye utando laini kwenye bawa.
- Wiki ya kumi na mbili (12) chanja Homa ya matumbo ( salmonellosis) hii unachoma kwenye nyama hasa pajani.
 
Safiii
 
Asante,niombeeni safari yangu iwe ya Mafanikio

Nilinyunyuzia dawa kwenye banda sasa nikaja kuweka pumba za mpunga jamani zinawasha na zina wadudu wale wa mahindi ,vifaranga hawatapa shida kweli ?kwa juu nimeweka magazeti
 
Nilinyunyuzia dawa kwenye banda sasa nikaja kuweka pumba za mpunga jamani zinawasha na zina wadudu wale wa mahindi ,vifaranga hawatapa shida kweli ?kwa juu nimeweka magazeti
Nimependa jinsi ulivyofanya, kupuliza dawa na kutamdika magazeti juu ya matandazo na hakika watakuwa vizuri bila tatizo.

Sema kama bado hawajamaliza wiki na hali ya hewa jinsi ilivyo dar ni vyema ukawa unaenda kuwaangalia kila baada ya masaa 2 kujua wanaendeleaje ( Hasa ukaguzi wa vyanzo vya joto maana vifaranga huwa wanashambuliwa sana na baridi na usipokua makini unaweza poteza vifaranga wengi wakati huu wa wiki moja).

Ila kwako sina mashaka na imani umezingatia protocol zote muhimu.
 
Yani nimeshindwa kusubiri mvua iishe ,lakin banda nimeliwekea bruda na vyungu vya kuwapa joto ,nimeziba banda sehemu zenye nyavu ,nawalea kama watoto naogopa kuwapoteza
 
Yani nimeshindwa kusubiri mvua iishe ,lakin banda nimeliwekea bruda na vyungu vya kuwapa joto ,nimeziba banda sehemu zenye nyavu ,nawalea kama watoto naogopa kuwapoteza
Thumb up, keep on pushing pushing kazi nzuri wana siku ngapi?
 
Back
Top Bottom