Mwl. Nyerere hapa hukutenda haki ila Mungu akusamehe

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,046
Kila binadam uja Duniani kwa malengo mazuri ingawa sio kwa aslimia zote au muda wake wote awapo Duniani basi uyatenda mema peke yake. Hayati Mwl. Julius Kambarege Nyerere kweli yapo uliyofanya kwa faida ya watanzania lakini mengine kweli hayakua faida kwa watanzania. Yafuatayo ni haya mambo ambayo mpaka leo yamekua zigo la misumari kwa watanzania
1.Kuanzisha na kuiacha madarakani CCM
2.Kuunganisha Tanganyika na Zanzibar
3.Kuiacha katiba ya 1977 ikiwa bado inatumika wakati muda wake ulikua umeisha
4.Kuzifanya mali za wananchi kua za CCM
5.Kufuta uongozi wa kimila wakati ukijinasibu kuenzi tawala na tamaduni za Afrika
6.Kuleta sera za Ujamaa na Kujitegemea
Mungu akusamehe kama nasi tulivyo kusamehe lakini hatuwezi kamwe kusahau hii mizigo ya misumari uliyotuachia kwenye vichwa visivyo na nywele..
 
Ndiyo maana akasema tuchukue mazuri tuache mabaya ila chakushangaza viongozi wetu wanaacha mazuri wanachukua mabaya
Yanayo tutesa ni hayo ambayo wapo wanao diriki kusema eti ni mazuri mfano kuanzisha CCM,Katiba ya 1977 na kuunganisha Tanganyika kitu ambacho kimeifanya Zanzibar itawaliwe na nchi ambayo nayo ilipoteza jina lake halisi la Tanganyika kwa kuweka indirect colinialism
 
Kuna wanafunzi wake wamemfahamu vibaya hata kama alikuwa na maana mbaya moyoni mwake.Mungu turehemu na utukinge na wale chui waliovaa ngozi ya kondoo.Amin.
 
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Mwenye enzi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi) ni mmoja kati ya watu wachache sana makini na wakutilia mfano. Nakubali hakuwa malaika wala muungu, alifanya makosa hapa na pale ila ameacha mema mengi (legacy) kiasi cha kufanya hii thread yako kuwa moja kati ya thread zilizo sheheni ujinga wa hali ya juu kabisa. Hayati baba yetu wa taifa, pamoja na udogo wa uchumi wa Tanzania ya wakati ule alifanikiwa kufanya mambo yafuatayo:
1. Alisomesha watoto wote wa ki-Tanzania bure na kupiga vita adui ujinga,
2. Alifungua viwanda vingi kabisa na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira,
3. Aliboreshe huduma za hospitalini na kuzifanya kuwa kwenye kiwango cha kutukuka,
4. Aliimarisha na kuustawisha ushirika na kuhakikisha mazao ya mkulima yanapata soko na wakulima wanapata pembejeo kwa wakati,
5. Aliondoa matabaka kwa kuleta usawa katika jamii nyingi za kitanzania,
6 Alikuza matumizi ya lugha ya kiswahili, na mambo mengine mengi

Kimsingi, mwalimu hakuwa mbinafsi wala mbadhirifu tofauti na viongozi wa mataifa mengine ya Afrika katika kipindi kile, bali yeye ndiyo aliyejenga misingi imara ya nchi yetu na kukuza kuaminiana, undugu, ummoja na kuchochea amani ya taifa letu.
 
Kila binadam uja Duniani kwa malengo mazuri ingawa sio kwa aslimia zote au muda wake wote awapo Duniani basi uyatenda mema peke yake. Hayati Mwl. Julius Kambarege Nyerere kweli yapo uliyofanya kwa faida ya watanzania lakini mengine kweli hayakua faida kwa watanzania. Yafuatayo ni haya mambo ambayo mpaka leo yamekua zigo la misumari kwa watanzania
1.Kuanzisha na kuiacha madarakani CCM
2.Kuunganisha Tanganyika na Zanzibar
3.Kuiacha katiba ya 1977 ikiwa bado inatumika wakati muda wake ulikua umeisha
4.Kuzifanya mali za wananchi kua za CCM
5.Kufuta uongozi wa kimila wakati ukijinasibu kuenzi tawala na tamaduni za Afrika
6.Kuleta sera za Ujamaa na Kujitegemea
Mungu akusamehe kama nasi tulivyo kusamehe lakini hatuwezi kamwe kusahau hii mizigo ya misumari uliyotuachia kwenye vichwa visivyo na nywele..
Mimi sijaona tatizo hapo shida ni wewe uliezaliwa katika mfumo huu wa kibepari na vyama vingi, kwa sisi tuliozaliwa katika mfumo wa kijamaa na chama kimoja hatukuona hiyo shida unayoitoa, lakini pale zamani tulikuwa na redio ilikuwa inahitwa Player ili icheze lazima uweke santuri ndio ilie mfano wa santuri ilikuwa inaonekana kama CD na pia tulikuwa na Redio Kaseti ilikuwa double deck na single deck na kanda tulikuwa tunaludisha nyuma kwa peni sasa ukianza kuviangalia vitu hivyo kama vipo kwenu ujue lazima utamuona mzazi wako kama alikuwa mjinga hivi akuweza kufikilia kumbe wakati vitu hivyo vilikuwepo kulikuwa hakuna mbadala. Jaribu kujiuliza na utoe mbadala wake ndio utaweza kuuliza vizuri
 
Kila binadam uja Duniani kwa malengo mazuri ingawa sio kwa aslimia zote au muda wake wote awapo Duniani basi uyatenda mema peke yake. Hayati Mwl. Julius Kambarege Nyerere kweli yapo uliyofanya kwa faida ya watanzania lakini mengine kweli hayakua faida kwa watanzania. Yafuatayo ni haya mambo ambayo mpaka leo yamekua zigo la misumari kwa watanzania
1.Kuanzisha na kuiacha madarakani CCM
2.Kuunganisha Tanganyika na Zanzibar
3.Kuiacha katiba ya 1977 ikiwa bado inatumika wakati muda wake ulikua umeisha
4.Kuzifanya mali za wananchi kua za CCM
5.Kufuta uongozi wa kimila wakati ukijinasibu kuenzi tawala na tamaduni za Afrika
6.Kuleta sera za Ujamaa na Kujitegemea
Mungu akusamehe kama nasi tulivyo kusamehe lakini hatuwezi kamwe kusahau hii mizigo ya misumari uliyotuachia kwenye vichwa visivyo na nywele..
Mkuu uko serious kweli au unatania? Hata kuanzisha (sina uhakika kama kweli alieanzisha ni yeye au ndo maisha yetu halisi waafrika) ichukulie Tanzania bila ujamaa ingekuwaje leo?

Ukanda unatusumbua hadi leo na vijitabaka vinajianzisha. Na ndo mnachopigania kila siku ingawa hamjui kuwa hicho ndo mkipiginiacho.

Ukabila bado unatutafuna, ulitaka uchief uendelezwe are really serious?

Kipi ulichokikusudia kwanza? We kwa asili ulitokea kwenye jamii ambayo ubebari ungekunufaisha? Au hujui tofauti ya uchumi wa kibepari na kijamaa mkuu?

Vipi sera za ardhi, za kibepari zingekunufaisha kweli? Kumbuka akina Karimjee walikuwepo?

Ccm? Hiki kilichokuwepo c ccm alichokianzisha mwl. Irudie kuisikiliza hotuba ya mwl. OTU mbeya.
Poa, ila hata mimi leo hii nikipewa nafasi nitafanya kama alivyofanya Mwl.. na naamini hata Yesu angefanya kama Mwl. sijawahi kuona tofauti yoyote Kati ya Ukristo na Ujamaa mkuu.
 
"Kuzifanya mali za wananchi kuwa za CCM"

Daah viwanja vya mpira havina muendelezo kabisa pitch kama madaruga ya mpunga
 
Mimi namlaumu pale alipowaacha Wa Russia na wa China na kuwakumbatia Waingereza, endapo JKN angeamua kushirikiana na Warusi na Wachina sasa hivi tungekua mbali kwenye suala la Viwanda
 
Lawama.....lawama.....lawama.....lawama.....lawama....lawama......binadamu hawaishi kulaumu..........
 
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Mwenye enzi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi) ni mmoja kati ya watu wachache sana makini na wakutilia mfano. Nakubali hakuwa malaika wala muungu, alifanya makosa hapa na pale ila ameacha mema mengi (legacy) kiasi cha kufanya hii thread yako kuwa moja kati ya thread zilizo sheheni ujinga wa hali ya juu kabisa. Hayati baba yetu wa taifa, pamoja na udogo wa uchumi wa Tanzania ya wakati ule alifanikiwa kufanya mambo yafuatayo:
1. Alisomesha watoto wote wa ki-Tanzania bure na kupiga vita adui ujinga,
2. Alifungua viwanda vingi kabisa na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira,
3. Aliboreshe huduma za hospitalini na kuzifanya kuwa kwenye kiwango cha kutukuka,
4. Aliimarisha na kuustawisha ushirika na kuhakikisha mazao ya mkulima yanapata soko na wakulima wanapata pembejeo kwa wakati,
5. Aliondoa matabaka kwa kuleta usawa katika jamii nyingi za kitanzania,
6 Alikuza matumizi ya lugha ya kiswahili, na mambo mengine mengi

Kimsingi, mwalimu hakuwa mbinafsi wala mbadhirifu tofauti na viongozi wa mataifa mengine ya Afrika katika kipindi kile, bali yeye ndiyo aliyejenga misingi imara ya nchi yetu na kukuza kuaminiana, undugu, ummoja na kuchochea amani ya taifa letu.
 
Sikuleta hii mada kwa ajiri yakulinganisha mazuri na mabaya ya Mwalimu maana wengi tumejikita huko wakati mada hiko wazi..
Kuanzishwa kwa CCM,Katiba mbaya ya 1977,Ujamaa ,Kuchukua mali za wananchi kuwapa ccm pamoja na muungano ukoloni ni mambo ambayo leo imekua mizigo kwa watanzania kabisa..We forgive but we can not forget
 
Back
Top Bottom