Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Watanzania wengi hawana uhusiano mzuri na Jeshi la Polisi hali inayopelekea hata kufurahia kuuliwa kwao, sasa hili ni jambo la ajabu sana kwa kawaida jamii nyingi Wananchi huwa pmj na Polisi wao kwetu ni kinyume, sasa ni kwa nini?
Sababu ni kwamba Mlm.Nyerere alirithi Jeshi la Polisi ktk kwa Wakoloni kama nchi nyingi za Kiafrika zilivyofanya bila ya kufanya reforms zozote, hivyo tulilonalo ni Jeshi la Polisi la Kikoloni!
Maana yake ni kwamba liko kwa ajili ya maslahi ya Wakoloni, izingatiwe kwamba Mzungu aliunda Jeshi la Polisi ili kumlinda dhidi ya mtu mweusi, hivyo mafunzo yote ya Jeshi la Polisi yamejikita kwenye kumlinda Mzungu dhidi ya ,,muhalifu Mwafrika" yamejikita kwenye kuzuia na kuzima uprising ya Waafrika dhidi ya Mzungu na ndilo Jeshi tulilolirithi na hatujabadilisha hata nukta!
Sasa mara nyingi jamii nyingi zinapofanya mabadiliko makubwa kimfumo pia hufanya mabadiliko ya Jeshi ili yaendane na jamii husika, AK walifanya baada ya Apartheid, Ujerumani walifanya baada ya utawala wa NAZI kuanguka, Ulaya Mashariki walifanya baada ya Dola ya Kisovieti kuanguka n.k.!
Sasa sisi Waafrika hatukufanya reforms ina maana Jeshi letu la Polisi bado kazi yake ni kumlinda ,, Mzungu" dhidi ya mtu mweusi, ndiyo maana kwa mfano mpaka leo hii nchini Kenya Polisi anakusimamisha na kukuuliza Kipande chako yaani Kitambulisho cha ukazi, na sababu ni kwamba Mzungu alileta mfumo wa kipande Kenya na ni Waafrika tu ndiyo waliotakiwa kuwa na kipande ili waishi Nairobi lkn Mzungu au Muhindi hakuhitaji na lengo lilikuwa ni kumlinda Mzungu dhidi ya mtu mweusi yaani ilikuwa ni lazima Mzungu ajue wewe ni nani, unatokea wapi, Kabila lako lipi, Chifu wa Kabila lako nani, na unafanya nini Nairobi na alitumia Polisi kufanikisha hili, walipopata Uhuru kama vile sisi wakalichukuwa Jeshi la Polisi kama lilivyo!
Na ndiyo maana mpaka leo hii Polisi wa Tanzania wanauliza Kabila lako, unajiuliza ili iweje? Je mimi kuwa Mtanzania niliyezaliwa Pangani au Tunduru kijiji fulani haitoshi?
Hivyo kwa kuhitimisha ni kwamba tuna Jeshi la Polisi ambalo mafunzo yake na muundo wake wote linamuona mtu mweusi kama mhalifu na ikumbukwe wkt wa Ukoloni Polisi walikuwa wanaruhusiwa kutumia nguvu hasa kupiga Waafrika hata neno Tanganyika jeki ni kwa ajili ya mtu mweusi tu, Mzungu au Muhindi hawezi kupigwa tanganyika jeki hata leo hii, na wanafundishwa hili, tangu Ukoloni!
Hivyo ni lazima tufanye reforms na kuunda Jeshi letu la Polisi kwa ajili yetu Waafrika ambalo litatuona sisi kama watu Wema na siyo Wahalifu, lkn ni lazima ianzie kwenye mafunzo yao,...
Polisi wa Kiafrika (pichani) akipiga Mwafrika, huyu angekuwa Mzungu,Muhindi au Mchina wasingethubutu kumfanya hivi hata kama Mzungu akiwa Muuwaji wa kutisha bado Polisi wa Afrika hawezi kumpiga Mzungu, kwa maana anafundishwa hivyo, kumpiga Mwafrika na kumlinda Mzungu!!