Mwl. Nyerere ametujenga kwenye misingi ya uzalendo au misingi ya nidhamu ya woga? Au vita vya majirani zetu vimetutia upumbavu?

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
2,946
2,929
Saalam wanabodi,

Napata taabu ninapoona mambo yanayotendwa na viongozi na vyombo vya dola vya nchi yetu.

Najiuliza, ivi baba wa taifa Mwl Nyerere ametujenga katika misingi gani?
1. Kizalendo halisi?
2. Nidhabu ya woga?
3. Au machafuko na vita vya majirani zetu vimetupumbaza?

Viongozi wanatuburuta watakavyo, lakini tumekaa kimyaaaa! Na hata tukisema, basi kwa sauti ya unyongeee, kiasi kwamba wanaotuburuta wanajua kuwa hawa tumeshawalegeza.

1. Tunatungiwa sheria za hovyo, za kutuziba midomo na kutukandamiza lakini tupo tu. Shame on us!

2. Pesa zetu zinatumika bila utaratibu, lakini tupo tu!

3. Democracy inabinywa, lakini tupo tu!

4. Watu wanajiwekea kinga za kisheria wasishitakiwe wakitoka madarakani kwakuwa wanajua wanayotenda ni maovu,
lakini sisi tupo tu. PUMBAVU SISI!

5. Tulitaka katiba mpya, pesa nyingi zimetumika, leo hii ukiuliza sababu za kutopata katiba mpya ni nini, majibu yatakuwa haikuwa sera wala kipaumbele changu. Sisi tupo tu!

6. Watu wanatekwa, wanapotezwa na kuuawa, sisi tupo tu. Nk, nk, nk

Hao wanaofanya haya wakitaka tuwachague wanakuja na maneno, kuwa msiwachague wapinzani, isijekuwa kama Burundi, Rwanda au Congo.

Watanzania tunakubali tu!

MWALIMU NYERERE, UMETUJENGAJE? KWENYE UMOJA ULIFANIKIWA, KWENYE KUDAI HAKI ZETU UMETUJENGA KWENYE MSINGI UPI?

INAUMA SANA, TUMEKUWA KAMA SAMAKI KWENYE JARIFE, WANAVUTWA TU, AKIRUKARUKA KUJITETEA ANAPIGWA RUNGU. DAAAAH!
 
Nyerere aliacha uzalende na upendo miongoni mwetu Watanzania

Ndio maana ukienda nje ya nchi kila mtu anatamani kuwa Mtanzania ukijitambulisha
 
Ningekuelewa vizuri kama swali lako la tano lingeisshia kwenye nchi imetumia fedha nyingi bila sababu kupata katiba mpya. Ulipoendelea nimegundua unapolenga ni awamu ya tano. Wakati awamu ya nne imetumia fedha hizo ovyo kabisa mpaka marehemu akasema ameomba fedha za ziada na zile zilizobaki akakataa kuzirudisha akisema atazipangia kazi nyingine.

Usijali majina yenu yataandikwa kwa wino wa dhahabu
 
CCM imevamiwa na watu ambao wasingeweza kupewa uanachama ,wakabahatisha kuwa viongozi.Hawajui mwongozo wa TANU,hawakupitia vyuo vya uongozi wa chama,hawana heshima mbele ya wananchi wao ni wahuni tu.
Wametanguliza pesa na mali badala ya utu.Wameongeza manyanyaso na jeuri .
Katika mazingira kama hayo nani wakuwasemea wananchi?
 
Ccm ya sasa ndio ya kuleta maendeleo nyerere yeye alikuwa anajenga misingi sisi tunajenga nyumba
 
Back
Top Bottom