Mwl Nyerere aliwahi kumpigia kura Mbunge wa Upinzani. Je, alikuwa msaliti?

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Mwl. Nyerere wakati wa enzi zake akiwa ameng'atuka aliwahisema katika uchaguzi fulani wa kitaifa alipiga kura ya urais kwa mgombea wa CCM lakini kwa nafasi ya ubunge alimpigia mgombea wa upinzani. Hivi, jambo hili katika zama hizi za siasa uchwara (Rostam, 2009). Mwl. tungemweka kundi gani?

Msaliti? Mwanamakundi? Mchumia tumbo? Ndumilakuwili? Oil-chafu?

Tafadhali, ondoeni ushabiki. Jenga hoja unapochangia, wengi tuelimike
 
Alitumia Demokrasia ya kupigia mtu anayemuona atasaidiana na wanachi katika kuleta maendeleo. Mwl. hakuwa katika mlengo wa UCCM bali maslahi ya taifa na wananchi wake. Kwangu sioni shida kwa DR Slaa. Kuwa na Kadi ya CCm kwani nani hajui kama aliwahi kuwa CCM na baadaye akaondoka kwa ufedhuri wa hao watu. Kadi ya shibuda na Mrema walisharudisha? Sambwe Shitambala naye alirudisha ya CDM?
 
Toa details, source yako ni ipi, Nyere alisema hili lini na alimpigia mbunge gani wa upinzani huyo?
 
Kiranga ,
Ilikuwa katika jimbo la Musoma. Mwaka 1995. CCM walisimamisha mwizi (sasa hivi tunawaita mafisadi). Mwalimu akawaonya kuwa huyu mtu mliyemsimamisha ni mwizi, tafuteni mwingine. CCM kama kawa yao wakakataa. Mwalimu akasema hadharani kuwa hawezi kumpigia kura mwizi na atampigia kura mgombea wa NCCR/ Mageuzi, Ndobho, ambaye alishinda uchaguzi mwaka huo.
 
Yaani hii habari ya wezi CCM mpaka aibu, we limtu kama Mabina lile limtu la kazi kabisa linajulikana, wameenda kulifanya "Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza"

Duh,

Aibu.
 
Yaani hii habari ya wezi CCM mpaka aibu, we limtu kama Mabina lile limtu la kazi kabisa linajulikana, wameenda kulifanya "Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza"

Duh,

Aibu.

CCM wote ni wezi na wanalindana. Kuanzia ngazi ya juu hadi wilayani. Ndiyo maana kauli ya kujivua gamba sasa wanatamani hata wasingeitoa.
 
Kiranga ,
Ilikuwa katika jimbo la Musoma. Mwaka 1995. CCM walisimamisha mwizi (sasa hivi tunawaita mafisadi). Mwalimu akawaonya kuwa huyu mtu mliyemsimamisha ni mwizi, tafuteni mwingine. CCM kama kawa yao wakakataa. Mwalimu akasema hadharani kuwa hawezi kumpigia kura mwizi na atampigia kura mgombea wa NCCR/ Mageuzi, Ndobho, ambaye alishinda uchaguzi mwaka huo..........

Kaka hapo kwenye blue naomba kupatie jina la huyo mwizi aliyeangukia pua..! Teh teh teh, Nyerere alikuwa hamumunyi maneno. kwenye ufisadi
 
Naomba kusahihisha kidogo, Mwalimu hakumpigia kura huyo mpinzani, ila alimnadi mbele ya wapiga KURA, hii ilikua Musoma mjini wakati anamnani Mr. Clean Mkapa, mgombea wa magamba alikua na scandals kibao, mwalimu akamtolea uvivu hapo hapo na akasema, kama mimi ningekua ndio nyie wananchi ningempa Kura fulani. Yasemekana pia mwalimu hakufurahishwa na kitendo cha kamati kuu ya CCM kutoa jina la Dr. Slaa na kuweka mtu mwingine kule Karatu, ccm wanaipata sana leo kwa kitendo chao hico, na kama ni wakweli, lazima watakua wanajutia kutokumpa Dr. Slaa ile nafasi though sina hakika kama Dr. angepewa nafasi ile wakati ule, sijui kama hadi sasa angeendelea kuwepo ndani ya magamba, nahisi misimamo yake na sisiem wangetofautiana tu mbele ya safari.
 
Naomba kusahihisha kidogo, Mwalimu hakumpigia kura huyo mpinzani, ila alimnadi mbele ya wapiga KURA, hii ilikua Musoma mjini wakati anamnani Mr. Clean Mkapa, mgombea wa magamba alikua na scandals kibao, mwalimu akamtolea uvivu hapo hapo na akasema, kama mimi ningekua ndio nyie wananchi ningempa Kura fulani.

Mkuu yule aliekataliwa na Mwalimu alifanya kosa kubwa sana machoni mwa Mwalimu.. Alishiriki kukihujumu na kukiua chama cha ushirika cha Mara.. Mwalimu aliwaambia wananchi wacimchague kwa kuwa alishiriki kukiua chama chao cha ushirika..

Huyo ndo alikuwa Nyerere.. Hana hata chembe cha unafiki.. Wamseme kwa mengine..
 
ccm walimpisha munema ambaye alikuwa fisadi papa pale mara co-operative union .

mheshimiwa hakulipenda hili akaamua kumpa kura yake ndobo Ailikuwa mgombea wa NCCR!
 
Assume wewe ni mwana CCM kati Nape wa CCM na Dr.Slaa wa CHADEMA ungemchagua nani?. Weka uahabiki pembeni.
 
Assume wewe ni mwana CCM kati Nape wa CCM na Dr.Slaa wa CHADEMA ungemchagua nani?. Weka uahabiki pembeni.

Hilo swali halihitaji hata form 6 kujibu.... Dr. Slaa all the way.

Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk
 
Hukumbuki Paul Ndobo - Musoma Vijijini.

Asante.

Mkuu Jasusi kanipa hapo juu.

Licha ya mimi kutokukumbuka kuna wengine hawakujua kabisa, vijana (na hata wazee) wengi wanajifunza hapa kwa hiyo details ni muhimu.

Ukimnominate jambazi kwa tiketi ya CCM kwa kweli unawa force hata die hard members wa CCM wenye principles ama kuacha kupiga kura, ama kumpigia mpinzani.
 
Yaani hii habari ya wezi CCM mpaka aibu, we limtu kama Mabina lile limtu la kazi kabisa linajulikana, wameenda kulifanya "Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza"

Duh,

Aibu.

wakazi wa mwanza hakuna asiyemjua mabina, Ila hakuna asiyejua kuwa CCM wameweka pesa mbele
 
wakazi wa mwanza hakuna asiyemjua mabina, Ila hakuna asiyejua kuwa CCM wameweka pesa mbele

Wote walioshiriki kumchagua Mabina - na majambazi wengine kama yeye walio katika CCM-wameruhusu ujambazi kuwekwa juu na hawawezi kulalamikia matatizo ya CCM kutojali wananchi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom