Mwl. Nyerere alisema kama mnampenda Kikwete kanyweni naye chai - Sasa tunayaona!!

Magezi, nakubaliana nawe. Lakini katika Africa kura za wananchi hazina mantiki yeyote. Mkwere atamuita Jaji Makame na atamuamuru atangaze kwamba yeye ndio mshindi wa Urais. Watajenga jukwaa haraka haraka pale magogoni na Jaji Augustino Ramadhani ataitwa kumwapisha. Ndio maana amesema hahitaji kura za wafanyakazi ifikapo mwezi October 2010. Tafakari tafadhali!

Mkuu hilo liko wazi kwani miaka yote wamefanya hivyo. Sasa kinyume na hapo labda vijana wetu pale ngerengere waingie msituni.
 
Huu Mgomo haujaisha bado. Mnakumbuka Mataifa makubwa yalipoanza kushambulia CD Pirats? Jamaa wakaona ok, kununua CD sasa basi na wakaja na na hizi Programs za P2P kama Kazaa, Amule, nk. Wakaanza kuzishambulia nazo na kuwasaka wanaozitumia. Kwa hili walifanikiwa saana ila hawakufahamu kuwa sasa ndiyo wanamuamsha SMOKE kwani kumefumuka akina Torrents, Filetube huku watunza mafaili wakiwa akina Mediafire, Rapidshare, Megaupload nk nk. Hawa sasa watu wanaweka hadi film na tena za BURE kwenye HIGH quality (hadi Bluray).

Kama Kikwete anafikiri kutisha kumemaliza matatizo basi kweli anajidanganya. Alichofanya ni sawa na kunywa POMBE. Pombe ikiisha atajikuta matatizo yako palepale na maumivu ya kichwa juu. Tunafanya petition ya "Dr. Slaa agombee Urais". Jamaa hadi leo kashathibitisha uwezo wake na kwa kutumia madudu haya yanayoendelea leo, who knows? Karibuni mjiandikishe.
 
Nimekuelewa vizuri kama watanzania na wafanyakazi wote wataungana kumtoa huyu jamaa pale magogoni.

As long as CCM wanampitisha kugombea tena, pale Magogoni hatoki mkuu!

At this stage, ingepaswa watu makini, jasiri, shupavu ndani ya CCM waungane na kujitokeza kuchukua form kumpinga huyu jamaa.

Sikutegemea kama Rais mzima angeingia front na kuanza kutisha watu ati watapondwa virungu! Aibu hii angemuachia japo Mkuu wa jeshi la Polisi au hata Naibu Waziri.

Inaonekana kile cheo ni kikubwa sana kwake
 
sizungumzii mambo ya imani, lakini mi nimewahi kusema, ilimu ndiyo tatizo kubwa kwa mwenzetu huyu, angekuwa na ELIMU japo kidogo lazima angekuwa na maamuzi mazuri na ya hekima yatokanayo na serikali ya kichwani kwake, tatizo umbeya, majungu, unafiki na uzandiki ndiyo vilimtawala kichwani mwake, usije shangaa akamfukuza mtu kazi kisa kasimuliwa tu kisa
 
sizungumzii mambo ya imani, lakini mi nimewahi kusema, ilimu ndiyo
tatizo kubwa kwa mwenzetu huyu, angekuwa na ELIMU japo kidogo
lazima angekuwa na maamuzi mazuri na ya hekima yatokanayo na
serikali ya kichwani kwake, tatizo umbeya, majungu, unafiki na uzandiki
ndiyo vilimtawala kichwani mwake, usije shamgaa akamfukuza mtu
kazi kisa kasimuliwa tu kisa, ama akamfunga mtu maisha jera kisa amewahi kugombea
naye mwanamke
, ama akatia sihihi kwenye kitu asicho kijua, huyu ni juha.

Pigia jibu sahihi mstari
 
Uyu ndo JK wetu ni kimeo kwa kwenda mbele,mfano mimi niko kwa familia ya watu 12 ivi nikiwaconvice wote wasimpigie kura si itakula kwake!
Mkwere huyu anajua kuongeza wake tuu!
 
Kama ni katika masoko customer care zero yaani unawakacha wateja wako kura laki 3 kwake si bure,hii ni kibri ya chama am telling you
 
mimi nadhami rais amedanganya na kwa mtu aliye makini atagundua alichosema si kweli. Najua atakuwa amefanya analysis na kugundua kuwa wafanyakazi ni laki tatu na nusu tu, akadhani kura laki tatu na nusu si chochote kwake! Asichokumbuka ni kwamba kuna watu kibao ambao wanawategemea hao wafanyakazi laki tatu na nusu. Mimi pia nadhani nina haki ya kumkosoa raisi kwakuwa amesema uongo na ni kwa mtu asiye na umakini tu ndiye anaweza kufikiri rais alichosema ni sahihi. Kwa mfano, alisema ".....pesa wanazotaka wafanyakazi hazipo kwani zinatumika kununulia madawa, kuboresha miundo mbinu, kununua vifaa mashuleni, vitabu na madaftari...". Mimi najiuliza, ni wapi leo hii serikali inatoa madaftari kwa wanafunzi nchi hii? Ziko wapi hizo huduma ambazo rais anasema zinaboreshwa kwa hiyo hela amabayo wanaitaka? Ukweli ni kuwa hakuna kinachofanyika, huo ndio ukweli!
Rais anajigundua ni mwajiri mkuu wa serikali hivyo ana haki ya kuwa mkali katika suala la kudaiwa mshahara mkubwa na waajiriwa wake. Je, kwa ukali feki aliokuwa anuonyesha, alikuwa na kofia ya mwajiri ama alikuwa na kofia ya rais? Maana jazba alioionyesha kila mwajiri atakuwa ameionyesha, na hilo tulilitegemea. Ninajiuliza, mbona suala la msingi ambalo lilihitaji tamko - lile la kupunguza kodi kwa mshahara mdogo wa mfanyakazi- yeye kama rais hakulizungumzia? Akafikiri hicho alichokiongelea atakuwa ametuzuga tusahau hili! Hii inaonyesha tu kuwa rais hayuko makini, washauri wake si makini na watendaji wake si makini. Matokeo yake anatuhadithia hadithi za kiswahili kuhusu mbayuwayu wakati watu wanataka kusikia masuala ya msingi yanayohusu maisha yao.
Halafu suala la yeye kusema kuwa anayeona mshahara wa serikali hautoshi aache kazi akatafute kazi kwingine ni kauli ya mtu aliyefilisika kimawazo, na aliyekosa mwelekeo wa kuongoza na asiyefaa kuwa kiongozi wa serikali ama nchi bali kwa wake zake na wanawe. Hivi anasema hivi kwakuwa anajua yule mwalimu aliyekuwa mwalimu kule kijijini kwa muda wa miaka ishirini sasa hawezi kuacha kazi kwakuwa atapoteza mafao yake (kwanza ataweza asipate mafao yake,kwani mafao yenyewe kufapata ni kazi kweli kweli, pili sekta binafsi haiwezi kumwajiri mwalimu huyu, kwani alichonacho sicho sekta binafsi wanachokihitaji - kwanza amesoma kwa mitaala mingine, sekta binafsi wanafundishia mitaala mingine).
Inauma sana kuona wachache wananufaika na maposho kibao, na safari zisizo na tija kwa taifa, ilhali mfanyakazi wa msingi kabisa wa nchi hii anaumia sana. Fikiri, posho ya mtu kwa siku ni zaidi ya mshahara wa mwalimu kwa mwezi mzima! Jamani, tunaelekea wapi kama si kufanya watu waishi kwa ujanja ujanja!
Ndio maana watu serikalini hawatendi kazi bali wanazuga-zuga tu wanaripoti makazini, halafu wanaaga kwenda kutafuta cha kujazilia kwenye kipato chao.
Upande wa pili pia nije kwa upande wa wafanyakazi wa serikali. Hivi jamani ndugu zangu, nani aliwaloga? Mbona sioni weledi, uadilifu na kujituma maeneo yenu ya kazi? Mbona mnakuwa watu wasiojali wala kuthamini kazi zenu? Wengi ni mashahidi, serikalini huduma ni mbovu vibaya mno kila mahali; hospitalini, ofisi za serikali, mashirika ya umma nakadhalika. Hivyo basi wafanyakazi muanze kujipanga, la-sivyo tutaishia kuona wafanyakazi wanaendelea kudharaulika, kudhalilika na kuumia ilhali kila kitu kinamilikiwa na wafanya biashara. Hebu basi wafanyakazi serikalini muamke, muache kusoma magazeti bali muanze kufanyakazi ili angalau siku moja tanzania iwe kama japan, ama ujerumani.
Nilikuwa nasikiliza bbc asubuhi hii na nikasikitishwa sana na jibu alilotoa waziri wa fedha bwana mkulo alipokuwa akihiojiwa na mwandishi kuhusu biashara ya japan na tanzania. Anasema biashara kati ya japan na tanzania imekua sana, akulizwa (nadhani hakutegemea swali hili): Je, tanzania inauza nini na cha thamani gani japan na japan inauza tanzania bidhaa za thamani gani, akajikuta anaanza kubwabwaja na kukiri tanzania inauza malighafi tu ya thamani kidogo ilhali japan finished goods zenye thamani ya mabilioni ya shilingi kwa tanzania. Ni kwa utendaji huu pia ndio maana hadi leo hatuna kiongozi hata mmoja anyetamani ama kuwaza tanzania tunatengeneza mitambo, magari yetu wenyewe, ama japo hata ku-assemble kama wanavyofanya hapo bondeni afrika kusini. Miaka arobaini ya uhuru bado hata trekta tunaagiza nje wakati tunajua kilimo ni uti wa mgongo wa nchi hii!
Kweli rais ajipange yeye na watu wake, la sivyo itafika mahali watu wataona potelea mbali, mali za umma ni za kuibwa na ukipata na nafasi mtu usifanye makosa.
Tusipojiangalia tutakuja kuishia kusifia nchi za wenzetu wenye akili timamu kuwa ni nzuri na zinapendeza ilhali yetu inaoza na inanuka.
Kuna wakati huwa natamani, mwalimu nyerere alipomaliza kipindi chake angerudisha tu nchi kwa wakoloni, labda pengine tungekuwa mbali. Maana wangetunyonya lakini miundo mbinu ingeonekana, huduma zingeboreshwa, tungekuwa bado na usafiri wa reli na mashamba ya kahawa na mikonge yangeendelea kuwa hai hadi leo.
Namuomba mungu ifike mwisho wa mateso haya na kama ni mapenzi yake wasiotenda haki na kwa uadilifu katika ngazi yoyote serikalini wafe! Tumechoka na wakoloni wenyeji hawa!

nimekusoma mkuu, kesho na keshokutwa hili poyoyo linalia..oooh wasomi acheni kukimbilia nje ya nchi, kuweni na uzalendo na nchi yenu...leo hii anajifanya anayeona mshahara mdogo na aache kazi.....sasa nje hatutakimbilia tena, kazi hatutaacha ila tutapambana nae humu humu...keshawatia watu hasira, nadhani kila mfanyakazi keshaanza kupambana nae kivyake, mimi mke wangu siku ile nimemkuta kavimba kwa hasira kwa maneno yake kikwete, akasema hatakaa ampigie kura kikwete, mi nilishaamua tangu kipindi hicho kuwa kikwete ni hafai mpaka basi, so kura yangu no, kila mfanyakazi akifanya hivyo akaongea na wanaomtegemea haki ya nani hata jamaa akishinda ni atakuwa kachagulliwa na mapoyoyo wenzie tuu..kila mtu na afanye kwa nafasi yake..just you and your relatives at home, mwisho wa siku huyu atang'oka tuu atake asitake..watu wengine wanaweza wakaona kama haiwezekani, lakini ni simple sana...usipomtumia bi. Mkubwa kahela kule kijijini ukamwambia raisi ndo kasababisha haya haki ya nani hatamchagua uchaguzi ujao..lets try and see....
 
Kwa mtindo huu balaa linakuja, huu ni moshi tu, kwa mwenye busara atajua kuwa ukiona moshi unafukuta juu ujue huko chini kuna moto unawaka, hawa wakubwa nadhani hawatutakii mema,
 
Tangu Kikwete aingie madarakani wengi tulianza kuwa na wasi wasi hasa pale alipowahi kusema mgao wa umeme utakuwa historia lakini leo anaogopa hata kivuli chake linapokuja suala zima la umeme kwa nchi.

Marais wengine duniani wanahangaika kuona wananchi wao wanapata huduma nzuri za afya, elimu, chakula n.k. lakini Kikwete anahangaika na kufurahisha ulimwengu kwa kutembelea kila nchi kwa kutumia kodi za wananchi tena walio maskini sana.

Mbaya zaidi anawatishia wananchi walio taabani kwa njaa na maradhi eti watapigwa virungu na polisi kama watatimiza haki yao ya kudai uhuru wao kazini, huyu si raisi tulimhitaji Tanzania. Rais Obama anahangaika kupitisha sheria ya bima ya afya ili hata maskini wapate huduma, yeye Kikwete anahangaika na sheria mfu za kukandamiza demokrasia, tena anatia saini bila kuzisoma.

Natoa wito kwa Watanzania, huu ni wakati wa kupiga kura sahihi kwa mtu sahihi lakini siyo Kikwete.

Tangu aingie madarakani Obama ameshakwea Pipa mara ngapi na trip za nje ya USA. Rais wetu Bwana teh teh kho!!

Lakini si 2005 Tluway aliwaambia laivu wakati anarudisha fomu ya ugombea ikulu kuwa jamaa anayetumia silaha ya magazeti kuwachapa wenzake akiingia ikulu atatumia Dola. Si ndio ninyi mlibisha mkasema tumaini lilopotea? Haya mbishieni PM wetu wa zama ndugu Fred Tluway.
 
Nakumbuka mzee Ben wakati anachomoka alisema kuwa mtakuja nikumbuka.
 
:angry:
Mimi nadhani wananchi tuamke, tuanzie kwa wabunge na madiwani. Yeyote anayekuja na ahadi uchwara na ushabiki wa chama TUPA KULE..! Bungeni kukiwa na wabunge wengi machachari cha moto atakiona. naona anajiona kichwa kubwa kwakuwa hakuna mpinzani halisi wa kupambana naye. Lakini tunamwahidi kuwa hao wabunge wake wanajua hali ni mbaya kwao, ndio maana wote waliokuwa wamemzunguka wakati wa hotuba had grim faces, nyuso zisizo na matumaini, yaani kama vile walikuwa wanomba kaka yao aache kubwabwaja maana athari zitakuwa kubwa.

Mwache aendelee kujisifia ushindi wa kishindo kwa kuwa watanzania wengi hawajaamka kutoka lindi la ujing la kupambanua mambo, ila iko siku, na safari hii haki ya nani tena wabunge/ madiwani uchwara wajiandae!

Halafu na nyinyi wapinzani itafikia pahala tuta wachapa viboko kama watoto ama kuwapopoa! Mtu anakuwa machachari akiwa upinzani, anapata kuaminika, anapata wafuasi halafu eti mwishoni anajidai "..nimeona ccm ni chama kizuri kinatekeleza mambo yake vizuri na kina nia ya kuwasaidi wananchi..." watu kama hawa unawachapa viboko ama kuwanyonga hadharani! Wewe watu wenye akili zao wanakuamini wanakusikiliza halafu dakika za mwisho mwisho, kwa sababu ya njaa yako na mkeo na wanao, unaamua kuhama kama vile unabadilinguo tu hivi hivi kirahisi rahisi halafu mtu asikushungulikie? mimi naona hii si sawa, ukiachwa hivi hivi wananchi na wafuasi wako wanakuwa hawatendewi haki. Dawa ni kuwachapa viboko tu hawa.

Vi-mtu vyenye njaa kama hivi ndivyo vinavyowafanya wana-ccm wavimbe kichwa, waendelee kutamba! Mimi si mwanachama wa chama chochote lakini kama mwananchi wa nchi hii ninayaona haya, na nina haki ya kuyasemea.
Mwisho, kwa nyinyi wapinzani mnaoona kuwa mara baada ya uchaguzi kinachofuata ni likizo na kulala usingizi,nanyi nawaombe KIFO kutoka kwa Mungu maan hamtufai wala hamuifai nchi yetu hii.

Inatakiwa wewe mpinzani ukija kuomba kura mara hii na ulishiriki uchaguzi uliopita, utueleze kwa muda wa miaka mitano ambayo hukuchaguliwa, ulikifanyia nini chama chako! Usikurupuke tu kwa vile una hela za kampeni na una kajikundi ka walevi wenzio wanaoweza kukupigia debe ukaja kwetu kuomba kura na ahadi uchwara TUTAKUPOPOA ama KUKUCHAPA! Nenda kakae na mkeo na wanao acha nchi iongozwe na watu walio na nia ya kuwa watumishi wa wananchi!

Halafu jamani watanzania wenzangu, asije mtu akaja na ahadi za kijinga za kusema eti: "....oh mkinichagua nitawajengea bara bara, nitaleta maji, nitajenga shule ..." n.k Hivyo vyooote si suala la wananchi kuomba, bali ni wajibu wa lazima wa kila mtumishi wa nchi a.k.a kiongozi kulifanya. Yaaani hizo ni agenda za lazima kwa hiyo sio za kujinadi nazo! Wananchi tuamke!

Naona wengine wameanza kufanya kampeni chini chini, mara oooh REDET utafitin unaonyesha ..... atashinda kwa aslimia zaidi ya 75, mbona nikijaribu kuchunguza naona sample space ya uchunguzi wenu inatia mashaka, eti wamehojiwa watu elfu mbili. ELFU MBILI out of say milioni ishirini wanaoweza kupiga kura. How realistic is that? Na isitoshe, the uhalali na uhalisia ya kilichosemwa na REDET ama REDET yeneywe unatia shaka.

Niwaombe wanajamii, kila mwenye uelewa wa haya mambo tuanze kuwaelimisha watu wengine, japo watatu kwa wiki, tupo pabaya kwani uelewa wa watu walio wengi kwenye mambo ya msingi ni mdogo mno. Uhakika wa hilo ni mfano mdogo tu wa World Economic Forum inayoendelea hapa Dar Es salaam, leo asubuhi kuna mtangazaji alikuwa anawahoji watu mitaani, majibu aliyokuwa anapewa ni aibu kuyataja!
 
WanaJF

Napenda kuwarudisha nyuma enzi za mwalimu alipomkataa J kikwete akisema KIJANA HAJAKOMAA HAWEZI KUONGOZA NCHI, waliokuwepo kipindi kile walimpuuza wakamuona Nyerere hafai lakini sasa madhara yake ndo tunaanza kuyaona.

Hapa sisemi kwa matakwa binafsi wala ya kisiasa nasema ukweli mana Mheshimiwa ameonesha upungufu mkubwa sana.

Je wanaJF Huyu mheshimiwa akiendelea kuongoza nchi matokeo yake yatakuwa nini?

lowasa%20na%20kikwete1995.jpg

BAADA ya kutuma mtandaoni uchambuzi mfupi wa nafasi ya Mwalimu Julius Nyerere katika kututafutia "mgombea safi" (Mr. Clean) mwaka 1995 nimejulishwa kwamba kuna utata, tatizo au walakini katika uchambuzi huo. Inasemekana siyo kweli kwamba Nyerere alihusika na kuhakikisha kwamba Benjamin Mkapa anamshinda Jakaya Kikwete. Kwa kuwa mimi ni muumini wa kuweka historia sawa, ningependa tujadili suala hili kwa kutumia vyanzo mbalimbali ili kuhakikisha hatupotoshi historia au ukweli hasa mwaka huu wa Uchaguzi Mkuu.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 1995 nilikuwa nasoma Shule ya Sekondari ya Azania. Nyumbani nilikuwa nasaidia kukata vipande vya magazeti kwa ajili ya uchambuzi wa kisiasa. Kipindi hicho nilikuwa navutiwa sana na harakati za kisiasa za Kikwete na nilifuatilia sana msisimko uliotokea wakati yeye na Edward Lowassa walipopanda ndege ndogo ya kukodi na kwenda Dodoma kuchukua fomu za kugombea dakika za lala salama, lakini kwa sasa nimepata picha tofauti.

Hali kadhalika nilikuwa nafuatilia kwa karibu sana hotuba za Nyerere na vile vitabu vyake alivyovitoa kabla ya uchaguzi huo ambavyo, kwa uelewa wangu, kimsingi vilitumika pia, kwa namna moja au nyingine, kuhakikisha kuwa mwaka 1995 John Malecela hapati urais (hasa) baada ya lile sakata la OIC na G55.

Kwenye mjadala wa wanazuoni, mwaka 2009 kuhusu niliwahi kuandika maneno yafuatayo: "When Nyerere was asked that question, I am told, he responded by saying that he was unlucky, implying that two people in particulary that he groomed died prematurely: (Hussein Ramadhani) Shekilango (from whom we get the name of that road in Dar) and Edward Moringe Sokoine, another person that he groomed but, due to malicious campaigns, never became our President (The President who never was as Zitto Kabwe calls him) is Dr. Salim Ahmed Salim.

Now we are struggling with the legacy of a president Nyerere 'chose' for us in 1995 but if we look at what was in his mind as his 1995 book Our Leadership and the Destiny of Tanzania reveals, we will realize that his was a genuine attempt to make sure that the other folks that he groomed to be good leaders - and turned bad according to his standards - do not take over. Now should we blame him for who we become?"

Hayo maneno nimeyakumbuka kwa sababu wanaoona kuna walakini kwenye madai au hoja kuwa Nyerere alikuwa na 'mkono' katika kumzuia Kikwete kuwa Rais mwaka 1995, wanasisitiza - na nakubaliana nao kabisa - kuwa mgombea wa Nyerere alikuwa ni Dk. Salim. Lakini tatizo ni kwamba kwenye kile kinyang'anyiro cha 1995 hakuweza kuingia ulingoni kutokana na sababu ambazo nadhani sote tunazielewa. Hivyo, pia ni rahisi kuelewa madai au hoja nzito inayosema kwamba Nyerere alimpigia debe Kikwete aingie kwenye 'tano au tatu' bora ya wagombea wa urais kupitia CCM ili wagombea wote wasiwe wa dini moja, hasa ukizingatia kwamba 'nyufa za udini' zilikwishajitokeza katika medani ya siasa au kampeni na ilibidi azikemee mara kwa mara.

Lakini tukumbuke kabla ya kinyang'anyiro cha awali tunaambiwa Kikwete alienda kuonana na Nyerere nyumbani kwake Msasani, jijini Dar es Salaam. Inasemekana aliitwa (aende) mwenyewe ila akaenda na Lowassa. Na kuna tafsiri kinzani kuhusu taarifa mbalimbali za wakati huo, zinazosema kwamba Nyerere aliona kuna tatizo na Lowassa japo pia tunaambiwa alibariki uamuzi huo wa Kikwete wa kwenda kugombea.

Baada ya hilo la Kikwete kuendelea kuwa pamoja na Lowassa kweli tunaweza kusema bado Nyerere alikuwa hajachagua 'amuunge' nani mkono kati ya Mkapa na Kikwete kwenye raundi za mwisho za kinyang'anyiro cha kuchaguliwa kugombea urais kwa tiketi ya chama tawala pale Dodoma?

Kweli Nyerere alikuwa anaona ni sawa yeyote kati ya Mkapa na Kikwete akishinda hivyo hakutumia mbinu yoyote kuzuia Kikwete asishinde maana (eti) alikuja tu kugundua kuwa yeye na Kamati Kuu ya CCM 'wamepigwa changa la macho' mwishoni kabisa kabla tu ya kupiga kura ilipoonekana Kikwete amedhamiria kumteua Lowassa awe Waziri Mkuu iwapo atashinda nafasi hiyo?

Sasa kuna hoja nyingine ya msingi kabisa, kwamba kambi ya Kikwete ilikuwa haijasoma au haijaelewa vizuri katiba au kanuni za CCM kuhusu 'kutosha kwa kura' ila (eti) kambi ya Mkapa ndiyo ilikuwa inalijua suala hilo fika, hivyo, basi ikautumia mwanya huo kuhakikisha kwamba pamoja na Kikwete kupata kura nyingi zaidi kuliko Mkapa, kikanuni, kura zipigwe tena na hivyo kwenye raundi ya mwisho ya kinyang'anyiro Mkapa akamshinda Kikwete, baada ya wengi wa wale waliopigia kura wale wagombea wengine walioenguliwa mwanzoni au katikati kumpigia Mkapa.

Ni hoja ya msingi maana inawasaidia kutuonesha au kuthibitisha kwamba siyo Nyerere aliyemzibia Kikwete bali lilikuwa ni suala tu la kikanuni (na kampeni za kambi) lililosababisha kura zipigwe tena na zile zingine zihamie kwa Mkapa hivyo kumzidi mwenzake.
Lakini swali la kujiuliza: Ni kina nani hao waliokuwa kwenye hiyo kambi (ya kampeni) ya Mkapa maana kwa uelewa wangu walikuwa ni 'Wanyerere' ('Nyerereists') wakuu? Kama ni hivyo, wako upande gani leo hii hasa wanapoona Nyerere wao anatumiwa 'ndivyo sivyo' katika kampeni za uchaguzi wa wagombea urais?

Wajitokeze sasa basi kutusaidia kuiweka historia sawa hasa ukizingatia mwaka huu wa 2015 una mengi sana yanayofanana na yale yale mwaka 1995.

Chanzo:raia mwema
 
Mhhh tutabaki kuwa shamba la Bibi,.... Sasa atakuja komaa lini?:flypig:Kambayuwayu ketu
 
Yuko hivyo alivyo kwa sababu hana shinikizo la kumfanya achange..! Naona theory ya survial of the fittest imsehindwa kuaply kwake..!
 
Sio kila mtu anafaa kuwa kiongozi. Na wengi uwezo wao wa kuongoza unaishia level fulani tu na zaidi ya hapo anakuwa sio effective. Mfano Keenja alifanya vizuri sana akiwa kiongozi wa tume ya jiji lakini kwenye level ya uwaziri hajaweza kuonyesha umahiri wake. Mrema alifanya vizuri sana akiwa waziri wa mambo ya ndani, lakini kwenye level ya uenyekiti wa chama hajaweza kuonyesha cheche zake.

Pengine Kikwete alikua katibu wa chama mzuri tu kwenye level za mikoa lakini sina record yake hata kwenye level za uwaziri aliyofanya beyond expectation. Naona ilikua ni ushabiki shabiki tu ulimnyanyua alipombomoa Kigoma Malima hata watanzania wakajiaminisha kuwa ni kiongozi mahiri.

Kimsingi JK hana uwezo wa kuwa Raisi wa nchi. Cheo hicho ni kikubwa sana kwake ndio maana anapwaya.:angry:
 
Mwl alikuwa anafocus mbali sana, aliposema alikuwa anajua akili za JK ni fupi kama mkia wa sungura. Yaani cognitive yake ndogo sana. Yanajithibitisha kwa matendo na kauli zake.
 
Back
Top Bottom