Mwl. Nyerere alisema kama mnampenda Kikwete kanyweni naye chai - Sasa tunayaona!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwl. Nyerere alisema kama mnampenda Kikwete kanyweni naye chai - Sasa tunayaona!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magezi, May 5, 2010.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tangu Kikwete aingie madarakani wengi tulianza kuwa na wasi wasi hasa pale alipowahi kusema mgao wa umeme utakuwa historia lakini leo anaogopa hata kivuli chake linapokuja suala zima la umeme kwa nchi.

  Marais wengine duniani wanahangaika kuona wananchi wao wanapata huduma nzuri za afya, elimu, chakula n.k. lakini Kikwete anahangaika na kufurahisha ulimwengu kwa kutembelea kila nchi kwa kutumia kodi za wananchi tena walio maskini sana.

  Mbaya zaidi anawatishia wananchi walio taabani kwa njaa na maradhi eti watapigwa virungu na polisi kama watatimiza haki yao ya kudai uhuru wao kazini, huyu si raisi tulimhitaji Tanzania. Rais Obama anahangaika kupitisha sheria ya bima ya afya ili hata maskini wapate huduma, yeye Kikwete anahangaika na sheria mfu za kukandamiza demokrasia, tena anatia saini bila kuzisoma.

  Natoa wito kwa Watanzania, huu ni wakati wa kupiga kura sahihi kwa mtu sahihi lakini siyo Kikwete.
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160

  hapa umenifurahisha sana mkuu
   
 3. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Magezi, Biiig UUUUUP !

  Jamaa hamna kitu jamani mimi nasema sijawahi kumpigia kura kikwete na sitokuja kumpigia kamwe hata akigombea uenyekiti wa serikali za mitaa ninapokaaa. Ni mtu wa mambo ya kitoto kila kitu anapandikiza watu, hata mkutano wa wazee alikuwa na mapandikizi kibao.

  Wewe watu gani wananza kwa kushangilia hata hujajua umeitiwa nini? Unashangilia nini?????? Alileta kamtindo ka kupiga simu kwenye TV laivu watu siku ya pili wakamsema na mapandikizi yake. Huyu jamaa hata skul atakuwa alipita hivyo hivyo. Lakini watanzania tunaweza tukaamua na kufanya mabadiliko, rais unakaa kutisha watu tuuuuu, kwa nini asingeacha waziri mwenye dhamana ndiye ashughurike.

  Halafu angekuwa mtu fulani angewasikiliza TUCTA kwanza sasa yeye kamsikiliza waziri naye kamdanganya basi kakurupuka. ngoja tumalizie miaka michache iliyobaki tuwaachie nchi yenu tumeshazeeka wengine sana.
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mhhhhhhhhhhhhhhhh maombi mazeeeeeeeee tu
   
 5. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Mimi nadhami Rais amedanganya na kwa mtu aliye makini atagundua alichosema si kweli.

  Najua atakuwa amefanya analysis na kugundua kuwa wafanyakazi ni laki tatu na nusu tu, akadhani kura laki tatu na nusu si chochote kwake! Asichokumbuka ni kwamba kuna watu kibao ambao wanawategemea hao wafanyakazi laki tatu na nusu. Mimi pia nadhani nina haki ya kumkosoa Raisi kwakuwa amesema uongo na ni kwa mtu asiye na umakini tu ndiye anaweza kufikiri Rais alichosema ni sahihi.

  Kwa mfano, alisema ".....pesa wanazotaka wafanyakazi hazipo kwani zinatumika kununulia madawa, kuboresha miundo mbinu, kununua vifaa mashuleni, vitabu na madaftari...". Mimi najiuliza, ni wapi leo hii serikali inatoa madaftari kwa wanafunzi nchi hii? Ziko wapi hizo huduma ambazo Rais anasema zinaboreshwa kwa hiyo hela amabayo wanaitaka? Ukweli ni kuwa hakuna kinachofanyika, huo ndio ukweli!

  Rais anajigundua ni mwajiri mkuu wa serikali hivyo ana haki ya kuwa mkali katika suala la kudaiwa mshahara mkubwa na waajiriwa wake. Je, kwa ukali feki aliokuwa anuonyesha, alikuwa na kofia ya mwajiri ama alikuwa na kofia ya Rais? Maana jazba alioionyesha kila mwajiri atakuwa ameionyesha, na hilo tulilitegemea. Ninajiuliza, mbona suala la msingi ambalo lilihitaji tamko - lile la kupunguza kodi kwa mshahara mdogo wa mfanyakazi- yeye kama rais hakulizungumzia? Akafikiri hicho alichokiongelea atakuwa ametuzuga tusahau hili! Hii inaonyesha tu kuwa Rais hayuko makini, washauri wake si makini na watendaji wake si makini. Matokeo yake anatuhadithia hadithi za kiswahili kuhusu mbayuwayu wakati watu wanataka kusikia masuala ya msingi yanayohusu maisha yao.

  Halafu suala la yeye kusema kuwa anayeona mshahara wa serikali hautoshi aache kazi akatafute kazi kwingine ni kauli ya mtu aliyefilisika kimawazo, na aliyekosa mwelekeo wa kuongoza na asiyefaa kuwa kiongozi wa serikali ama nchi bali kwa wake zake na wanawe.

  Hivi anasema hivi kwakuwa anajua yule mwalimu aliyekuwa mwalimu kule kijijini kwa muda wa miaka ishirini sasa hawezi kuacha kazi kwakuwa atapoteza mafao yake (kwanza ataweza asipate mafao yake,kwani mafao yenyewe kufapata ni kazi kweli kweli, pili sekta binafsi haiwezi kumwajiri mwalimu huyu, kwani alichonacho sicho sekta binafsi wanachokihitaji - kwanza amesoma kwa mitaala mingine, sekta binafsi wanafundishia mitaala mingine).

  Inauma sana kuona wachache wananufaika na maposho kibao, na safari zisizo na tija kwa taifa, ilhali mfanyakazi wa msingi kabisa wa nchi hii anaumia sana. Fikiri, posho ya mtu kwa siku ni zaidi ya mshahara wa mwalimu kwa mwezi mzima! Jamani, tunaelekea wapi kama si kufanya watu waishi kwa ujanja ujanja!

  Ndio maana watu serikalini hawatendi kazi bali wanazuga-zuga tu wanaripoti makazini, halafu wanaaga kwenda kutafuta cha kujazilia kwenye kipato chao.

  Upande wa pili pia nije kwa upande wa wafanyakazi wa serikali. Hivi jamani ndugu zangu, nani aliwaloga? mbona sioni weledi, uadilifu na kujituma maeneo yenu ya kazi? Mbona mnakuwa watu wasiojali wala kuthamini kazi zenu? Wengi ni mashahidi, serikalini huduma ni mbovu vibaya mno kila mahali; hospitalini, ofisi za serikali, mashirika ya umma nakadhalika. Hivyo basi wafanyakazi muanze kujipanga, la-sivyo tutaishia kuona wafanyakazi wanaendelea kudharaulika, kudhalilika na kuumia ilhali kila kitu kinamilikiwa na wafanya biashara.

  Hebu basi wafanyakazi serikalini muamke, muache kusoma magazeti bali muanze kufanyakazi ili angalau siku moja Tanzania iwe kama Japan, ama Ujerumani.

  Nilikuwa nasikiliza BBC asubuhi hii na nikasikitishwa sana na jibu alilotoa waziri wa fedha bwana Mkulo alipokuwa akihiojiwa na mwandishi kuhusu biashara ya Japan na Tanzania. Anasema biashara kati ya Japan na Tanzania imekua sana, akulizwa (nadhani hakutegemea swali hili): je, Tanzania inauza nini na cha thamani gani Japan na Japan inauza Tanzania bidhaa za thamani gani, akajikuta anaanza kubwabwaja na kukiri Tanzania inauza malighafi tu ya thamani kidogo ilhali Japan finished goods zenye thamani ya mabilioni ya shilingi kwa tanzania. Ni kwa utendaji huu pia ndio maana hadi leo hatuna kiongozi hata mmoja anyetamani ama kuwaza Tanzania tunatengeneza mitambo, magari yetu wenyewe, ama japo hata ku-assemble kama wanavyofanya hapo bondeni afrika kusini. Miaka arobaini ya Uhuru bado hata trekta tunaagiza nje wakati tunajua kilimo ni uti wa mgongo wa nchi hii!

  Kweli Rais ajipange yeye na watu wake, la sivyo itafika mahali watu wataona potelea mbali, mali za umma ni za kuibwa na ukipata na nafasi mtu usifanye makosa.

  Tusipojiangalia tutakuja kuishia kusifia nchi za wenzetu wenye akili timamu kuwa ni nzuri na zinapendeza ilhali yetu inaoza na inanuka.

  Kuna wakati huwa natamani, mwalimu Nyerere alipomaliza kipindi chake angerudisha tu nchi kwa wakoloni, labda pengine tungekuwa mbali. Maana wangetunyonya lakini miundo mbinu ingeonekana, huduma zingeboreshwa, tungekuwa bado na usafiri wa reli na mashamba ya kahawa na mikonge yangeendelea kuwa hai hadi leo.

  Namuomba Mungu ifike mwisho wa mateso haya na kama ni mapenzi yake wasiotenda haki na kwa uadilifu katika ngazi yoyote serikalini WAFE! Tumechoka na wakoloni wenyeji hawa!
   
 6. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Watanzania kazi tunayo bila kutoa ccm madarakani hamna kitakachoendelea kwanza no democrasia hapa nchini.
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwa mimi tokea atoe hiyo hotuba imani yangu kwake imekufaa kabisa, nitawasupport wengine akina Dr POmbe, Mwakyembe na wengine but sio huyo hhh
   
 8. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jaxo: Asante sana. Unajua nini serikalini mimi naona kuanzia juu kabisa hakuna umakini wa kazi mpaka kwa mfagizi. Maana naona kama rais mara nyingi watu wake wa karibu yaani mawaziri, washauri wana m mis-lead.

  Unajua kuwa mzembe kazini sio kwamba huna akili. Wana akili sana na washamsoma kwamba jamaa we mpelekeee tu hana noma. Inanikumbusha hotuba za mkapa saaaana. Kwanza alikuwa na sauti iliyotulia wala siyo ya kujitahisi kumuiga mtu jamaa alikuwa akianza kusema unajua anachosema ni kweli na anatekeleza.

  Na nadhani watu wa karibu kabla ya kumpelekea jambo walikuwa wanaangalia uwezekano woote kuwa lile jambo ni feki haupo kuwa kitu kipo vizuri. Basi tena ndo hivyo.
   
 9. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimekuelewa vizuri kama watanzania na wafanyakazi wote wataungana kumtoa huyu jamaa pale magogoni.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Interesting..lakini siku zote watu mlikuwa wapi? Mnngeanza mapema mwaka huu wa uchaguzi ingekuwa kumsukuma mlevi tuuu..
   
 11. O

  Omumura JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Alichoongea kikwete ni mipasho ya kijinga aliyojifunza kuiimba yeye pamoja na kapuya na hawa ghasia.
   
 12. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  "Kama mnamtaka KIKWETE mkanywe nae chai" Bila shaka hii inamaliza maneno yote.Mzee alikua anaona mbali kweli kweli.
   
 13. MANI

  MANI Platinum Member

  #13
  May 5, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Hakuna marefu yasiyo na mwisho.Sasa wale wazee wa ccm waliokuwa wanashangalia kila kitu hii barua ya mwaliko wa tucta serekalini iliyowataka wafike saa nane na nusu wakati jamaa alidai wamechelewa kwani walitakiwa waje saa nne wameiona jana?Huyu bwana huwa hajitayarishi atazungumza nini na kupitia ushahidi gani ndio maana anasaini mpaka sheria batili kwa mbwebwe. Lakini ndio safari yake inazidi kuiva kuondoka magogoni.
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ni dhahiri hakufikilia na kama kudanganywa si kidogo Mfanyakazi anategemewa na watu wangapi hasimami kama yeye pekee Ni kweli kachemka !
   
 15. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  kwani kuna anauwezo na kitu kingine??? Labda kucheka ndo kilichobaki....

   
 16. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  "ANAYETAKA ALIPWE SHILINGI 315,000/= AACHE KAZI KWANI KUNA WATU WENGI MTAANI WANAONGOJA KUAJIRIWA" Shime Madaktari wa binadamu na wa wanyama kuna kazi kule Botswana, Zimbabwe, Namibia, South Africa nk ambazo mshahara wake ni kuanzia USD 2500 kwa mwezi, unapewa nyumba na gari, tumuachie JK kazi zake awaajiri hao madaktari walio mtaani. Tumechoka kunyanyaswa na kudharauliwa na muajiri mkuu na waajiri wadogo. Shime twendeni tukafanye kazi nchi za watu zinazolipa zaidi ya hio 315,000/= ambayo presdaa anaona ni nyingi sanaaa.
   
 17. F

  Froida JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ukiona Raisi wa Nchi amenza mashindano na wananchi wake,ujue huyu kashindwa kazi hafai anapaswa kuonddoka tuu,Kama Viongozi wengine wa serkali hawakutaka kuungana na wafanyakazi wengi wao pale kwenye uwanja wa Uhuru iweje Lukuvi aliende kuhutubia mkutano wa wafanyakazi wa Benk na waajiri,manake nini Anataka kuingiza Nchi kwenye
  Machafuko ambayo hayajawi kuwepo,Mkuu wa Mkoa si lazima aripoti kwake kitu atakachofanya na yeye akaridhia.

  Zaidi ya hapo anaitisha wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam anaanza kutisha na kuponda wafanyakazi eti wako laki tatu na sitini na ushee, manake nini, amekosea sana sana; hivi haoni hasira za watanzania watu wanataka kuzuia greda lisibomoe ofisi ya mtendaji wao wanakuja na mapanga yamenolewa kama vile kuna vita haoni hii nchi iko kwenye hatari ya kuingia kwenye machafuko makubwa ambayo hakuna askari wala jeshi litayazuia,mshauri wake haswa ni nani ni huyo Salva banyamulenge,au Kapuya Mtaalamu wa Sayansi.

  Watanzania tusipoangalia huu uongozi wa safari hii utatuingiza mahari ambapo itakuwa kazi kurudi tuliko toka,wanachukulia vitu kijumla mno hawsomi alama za nyakati Tanzania na Wakazi wake wa leo sio ile ya Jana,Sisijui nani amrudi Aaache kiburi chake hicho
   
 18. w

  wasp JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magezi, nakubaliana nawe. Lakini katika Africa kura za wananchi hazina mantiki yeyote. Mkwere atamuita Jaji Makame na atamuamuru atangaze kwamba yeye ndio mshindi wa Urais. Watajenga jukwaa haraka haraka pale magogoni na Jaji Augustino Ramadhani ataitwa kumwapisha. Ndio maana amesema hahitaji kura za wafanyakazi ifikapo mwezi October 2010. Tafakari tafadhali!
   
 19. m

  manyusi JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2010
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 274
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Na misafara yake ni ya kishikaji zaidi,na inatumia pesa nyingi sana.Watanzania bado hatujapata Raisi mzalendo huyu nae ungwe yake ya mwisho ipite ili tujue moja kama watanzania tutakuwa tumefunguka tutaangalia MTU na si chama cha siasa.
   
 20. m

  manyusi JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2010
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 274
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kipindi cha mkapa makusanyo ya lipanda kwa kasi na inasemekana huyu muheshimiwa alikuta pesa nyingi tu za kuanzia lakini lini tangu aanze kutawala ametanganza kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kama ilivyokuwa kwa Mkapa?hizi ziara zinazoonekana ni baadhi tu kuna ziara ambazo sinasitishwa kwa ukosefu wa fedha.
   
Loading...