Mwl.Nyerere alifanya jambo hili mbele yangu mwaka 1998

Ana bahati enzi hizo hakukua na "polisi jamii" otherwise wangem Barlow.
 
Mwalimu alikuwa yeye, na hakujifanyisha, kujiigiza wala kujifananisha, alichokuwa anakisema ndicho alichokuwa ana kiishi, yeye alikuwa ndiye yeye yule na si mwingine kwa mema, mazuri na mapungufu, kama mungu alivyo mjalia ndiyo maana anaheshimika, na ataendelea kuheshimika kwa wote wanao penda na wasio penda, ukweli utabaki kuwa ukweli, nao ni kwa mungu tu.
 
Hakuwatendea waislam mambo mema. Aliwabagua, kuwahujumu miundo mbinu yao (sera ya uchumi ulikuwa ni kuwanyang'anya mali waislamu waliokuwa matajiri wengi, kuwanyang'anya mashule yao, kuua taasisi zao na kuutukuza ukatoliki), na kufanya serikali nzima iwe inafanya kazi kwa interest za viongozi wa kanisa katoliki huku ikiendeleza kuwanyonya waislamu na wakristo wengine walio wakatoliki. Dhambi hii aliyoitendea jamii ya watanzania ndi inafanya tumkumbuke kwa kueleza wasifa wake huu ambao wengine wasiopenda mabadiliko kuyaita "negative". Huu ndo wasifa wa JK Nyerere! sio kama wengi mlivyo aminishwa!

Meza tu kwa ujinga wako wa kutofikiri mara mbili....... Nyerere alitahifisha mali za wakristo ili msome leo mnamwona hafai....... Ni bora kumfadhili punda kuliko we mwenyw
 
Hahahaaaa! Watu ugaidi wameanza kitambo kumbe! Mama anajifungua, wanfunga vioo vya magari, alafu AC hazikuwepo, Kuona mkuu wa kaya kasimaa basi brake zinapishana tu hapo!!! Kujikomba bwana kumbe kumeanza LONGIIII! "Kwendeniii huko, huyu mama hamkumuona hapa?" Walisonyaje kimya kimya!
 
Siamini kwamba "waislamu" hawana Elimu. Mfano mdogo tu wa haraka haraka hawa wafuatao ni waislamu na wana elimu Mohamed Bakari (Mhadhiri Mzumbe) Bashiru Ally (Mhadhiri UDSM) Professa I.A. Lipumba (Mwanauchumi aliyebobea) Mohamed Shein (Bingwa wa Metabolism Duniani) Gharib Bilal (Bingwa wa Hisabati na Fizikia), Twaha Taslima (wakili Maarufu) Professa Safari (Bingwa wa Lugha na Isimu za Lugha) hawa kwa uchache ni wale tunaowafahamu wote bado wale ambao nawafahamu mimi wewe huwajui.

Mbona Uislamu wao haukuwazuia hawa kuwa wasomi? Mfumo Kristu ulikuwa wapi wakati hawa wanasoma?
 
Unamkumbuka mwalimu Malalika wa alliance miaka hiyo ya 90?

Ha ha ha Gagnija unataka nideclaree interest?.... Ungewakumbuka pia akina MDM Wandiba, Pcb Matovu, The late Kanyabuhura, Fundisha, Mwombeki, Rugaimukamu, Mmari na wengine!
 
Kama ulikua unawaza mawazo yangu, ameelezea kirefu kama vile aliendelea kuwepo eneo hilo na kuyafuatilia yote aliyoyasema Mwalimu. Pia hao aliowambia waende eti hawakua wanamuona huyo mama, inamaana yeye mwalimu aliwaona wakiwa wanampita huyo mama bila kutoa msaada???
Kila alichokisema mwl akiwa serious kilikuwa na fundisho ndani yake.Wakati ule nikiwa na miaka 16 ningeweza kufikiri namna hiyo,lakini leo naweza kupata tafakuri nzuri sana ya maneno yake hayo.Kwangu mimi ni kwamba alitaka kuonyesha kuwa ni wangapi walipita pale na hawakutoa msaada kwa yule mama.Lakini pia aliamini kuwa hata hao waliosimama kwa ajili ya mwl wasingeweza kusimama kumsaidia yule mama.Mimi binafsi nilikaa sehemu ya tukio hadi landrover inarudi na kumchukua mwl.Nilikuwa natoka kazini na hivyo sikuwa na haraka.Ukizingatia ilikuwa mara yangu ya kwanza kumwona mwl, na aina ya tukio.
 
siamini kwamba "waislamu" hawana elimu. Mfano mdogo tu wa haraka haraka hawa wafuatao ni waislamu na wana elimu mohamed bakari (mhadhiri mzumbe) bashiru ally (mhadhiri udsm) professa i.a. Lipumba (mwanauchumi aliyebobea) mohamed shein (bingwa wa metabolism duniani) gharib bilal (bingwa wa hisabati na fizikia), twaha taslima (wakili maarufu) professa safari (bingwa wa lugha na isimu za lugha) hawa kwa uchache ni wale tunaowafahamu wote bado wale ambao nawafahamu mimi wewe huwajui.

Mbona uislamu wao haukuwazuia hawa kuwa wasomi? Mfumo kristu ulikuwa wapi wakati hawa wanasoma?

ni kwa sababu waj******nga wanawaongoza waj*****nga wenzao
 
Ha ha ha Gagnija unataka nideclaree interest?.... Ungewakumbuka pia akina MDM Wandiba, Pcb Matovu, The late Kanyabuhura, Fundisha, Mwombeki, Rugaimukamu, Mmari na wengine!
Malaika asante sana mzee,Wandiba ni ndugu tumbo moja na babangu,ni baba mdogo.Baadae alihamishiwa Nyambuleti(ngoreme) kama mwl mkuu,kisha Nyanduga(tarime),baadae Lyamungo na hivi majuzi kahamishiwa shule moja hivi,nimeisahau,ipo arusha ama moshi.
 
Malaika asante sana mzee,Wandiba ni ndugu tumbo moja na babangu,ni baba mdogo.Baadae alihamishiwa Nyambuleti(ngoreme) kama mwl mkuu,kisha Nyanduga(tarime),baadae Lyamungo na hivi majuzi kahamishiwa shule moja hivi,nimeisahau,ipo arusha ama moshi.

Namfaham huyo bwana kwa makoko na matandu, mtu wa kazi sana. Pamoja mkuu
 
Siku moja Mwalimu aliagiza waitwe viongozi wakuu wa nchi wakati huo. Rais wa JMT alikuwa ni Ally Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar Salimin Amour na Waziri Mkuu John Samweli Malecela. Kwa kawaida Mwalimu alikuwa ana tabia ya kulala mchana saa 8 na kuamka kati ya saa 10 hadi saa 11 jioni. Siku hiyo saa kumi hivi viongozi hao waliwasili.

Mwalimu ndiyo alikuwa ametoka kuamka na alipoambiwa kwamba aliowahitaji wamefika aliionyesha kufurahi sana. Mwalimu aliwaita bustanini kwake na kuwakabidhi wote watatu kila mmoja Papai kubwa moja na kuwaambia "haya ni matunda toka bustanini kwangu asanteni kwa kuja". wakubwa wale waliondoka Msasani wakiwa na sintofahamu kubwa sana. Inaa maana Mwalimu alituita kuja kutupa mapapai?

Kisa hiki kinawahusu watu watatu ambao wote wako hai. Kama una udadisi nacho kawaulize Mwinyi, Amour na Malecela ili usije sema ni uzushi wakisha ondoka duniani!!

Hapo Mwalimu alikosea sana kama nia yake ilikuwa kuwafundisha jambo fulani hao viongozi! Mwalimu pengine aliwaza kuwa hao wanafunzi wake wataelewa dhumuni la huo mwito.

Kwa upande mwingine, hayo yalikuwa matumizi mabaya ya mali za umma; kwa sababu safari za viongozi watatu wakubwa kama hao ziligharimu pesa nyingi za watanzania. Sasa kuwaita na kuwapa mapapai, kisha kuwaacha warudi mwakwao, ilikuwa ufujaji wa mali.
 
Itachukua miaka mingi kumpata Nyerere mwingine Tanzania! Ametoweka kimwili lakini mawazo yake yataishi milele! Vichwa nazi watayakanyaga sasa, but his ideas will stand test of time and space! RIP Mwalimu!
 
Back
Top Bottom