BrAsMaRiLiSaShElMa
Senior Member
- Sep 23, 2016
- 149
- 181
Mambo ya namna hii ni ukatili na udhalilishaji uliokithiri kwa watoto wanaofanyiwa hayo na waalimu wao. Jamii na Taifa pia linaathirika maana watoto hawa ni nguvukazi ya Taifa.Marupurupu ya maticha hao
Taarifa zilizopo kuhusu tukio hili ni kwamba, aliyekuwa akiyafanya hayo kwa wanafunzi wale siyo Mwl. Mkuu Mambosasa peke yake; bali Mwl. Mkuu Msaidizi pamoja na Mwalimu wa Nidhamu, nao walikuwa washiriki wa mchezo huo mchafu dhidi ya watoto wale!!
Mwl. Mkuu, Msaidizi wake na Discipline Master, wanahusika kuwanajisi watoto hadi kuwapa mimba!!
Jamani, watoto hawa wako exposed kwenye hatari kiasi gani?
Ni mtu kutukana na kukufuru madaraka aliyopewa na umma; na haikubaliki.
Mwl. Mkuu ni kiongozi mwenye dhamana kubwa sana katika jamii; ndiyo maana Serikali inawalipa mishahara na Posho ya Madaraka, maana inatambua wajibu mkubwa wanaoubeba.
Baadhi ya shule zina watoto zaidi ya elfu moja, majengo, samani, fedha, miundo mbinu mbalimbali, waalimu na watumishi wengine; vyote hivi viko chini ya Mwl. Mkuu, ikiwa ni pamoja na kusimamia utendaji wa waalimu, taaluma ya watoto na mambo mengine mengi yahusuyo kituo husika. Ni wajibu mkubwa, Mwalimu anayekabidhiwa ukuu ni dhamana kubwa, yapaswa kuheshimiwa.
Kama unaona huwezi kumudu Ualimu Ukuu, kwa nini unakubali na kukiri uteuzi? Ni heri kukataa uteuzi, kuliko kuupokea kisha unakwenda kuwabikiri mabinti zetu; wengine tunasikia mpaka mnawafumua marinda ili kukwepa mimba; pumbavu sana, shwain!!