Mwizi wa kura ni sawa tu na mwizi wa kuku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwizi wa kura ni sawa tu na mwizi wa kuku

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by H6MohdH6, Nov 5, 2010.

 1. H

  H6MohdH6 Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwizi wa kura ni sawa tu na mwizi wa kuku. Amri ya saba inasema USIIBE. Haijasema usiibe kuku lakini kura iba tu!

  Mwizi anashughulikiwa kwa staili yake. Binadamu tuna staili yetu na kuku wana staili yao.

  Kuna mwizi wa kuku anaitwa kunguru. Huyu huiba vifaranga vya kuku. Lakini kufanikiwa kwake inategemea mama mwenye vifaranga anafanyaje. Kuna kuku mwenye vifaranga ambaye akiona kunguru anaiba vifaranga vyake analia tu na kulalamika. Hii haimzuii kunguru kupora vifaranga na ataviiba kimoja kimoja hadi vyote vimeisha.

  Lakini kuna kuku mwingine mwenye vifaranga ambaye kunguru akitaka kuiba watoto wake anamrukia juu kwa juu na kujibu mashambulizi hadi kunguru anakimbia. Kunguru anaogopa sana kumwibia kuku huyu na anaacha watoto wake salama.

  Ukitangaza mapema kuwa kunguru akitaka kuiba kuku wako hutachukua hatua za kumzuia si utakuwa umemwambia aibe kwa muda wake?
   
 2. F

  Fishyfish JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  No, a chicken thief is more honorable than CCM.
   
Loading...