Mwizi wa kuku kuuawa ni halali kwa taratibu za tanzania

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,861
1,302
Nimefuatilia kesi mbalimbali za matukio ya wizi, na ufuatao ni muhtasari mfupi wa mtiririko:
Ukiiba billion 40 - hakuna kesi, hakuna anayekufuatilia, unakuwa free man. Rejea suala la Kagoda.

Ukiiba kati ya billion 3 - 20 Utafunguliwa kesi ambayo baadae utaachiwa kwa kukosa ushahidi au kukiukwa taratibu au itachukua muda mrefu hadi inasahaulika. Fuatilia kesi za Mramba na wenzake uone mwisho wake, rejea pia kesi ya ile nyumba ya balozi Italia na ya Nalaila Kiula.

Ukiiba kati ya million 100 - 2.9 billion Utafunguliwa kesi na kuna uwezekano wa kufungwa kwa kifungo kisichozidi miaka mitano. Rejea kesi kama ya Kasusura.

Ukiiba kati ya Million 10 - 100 kuwa na uhakika asilimia 85 wa kufungwa. Hizi ndizo kesi nyingi zilizo mikoani na wilayani.

Ukiiba chini ya million 10 likely utapata adhabu kubwa zaidi maana mara nyingi hela hii ni kidogo ukianza kuhonga.

Unaweza kuona basi kuwa kadri unavyoiba kidogo ndivyo adhabu inavyoongezeka. The lesser yo steal the more severe the penalty and vice versa. Hivyo kwa kosa dogo kama la kuiba kuku basi adhabu kali ni kuuawa!!

Hata katika rushwa wanasema eti rushwa ndogondogo ni mbaya sana kuliko rushwa kubwakubwa - logically therefore wanachosema ni kwamba rushwa ndogo ibebe adhabu kubwa na rushwa kubwa ibebe adhabu ndogo.
 
Back
Top Bottom