Mwizi mwenye aibu asiye na huruma

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
1,879
1,126
Asalam wakuu,

Napenda ku share nanyi tukio lilonikuta leo. Nikiwa katika harakati za matibu katika moja ya hospitali kubwa hapa nchini kwa bahati mbaya, lakini pia uzembe wangu uliosababishwa na taharuki ya kuhakikisha mgonjwa wangu anapata matibabu niliisahau pochi/wallet yangu katika moja ya eneo hapo hospitali iliyokuwa kiasi cha fedha 205,000, pamoja na vitambulisho vyangu zikiwemo kadi za ATM.

Mwenye bahati mmoja alifanikiwa kuinasa wallet hiyo na kuchukua fedha zote. Nachoshukuru hakuthubutu kuondoka na wallet pamoja na hizo IDs.
hiyo ndiyo aibu pekee aliyokuwa nayo.

Lakini alishindwa kuwa na huruma kwa maana sehemu tuliyokuwepo ilikuwa nikupigania uhai, sijui yeye alikuja kwa lengo gani. Namuona ni kama msaidizi wa israeli mtoa roho.

Hakudhani pengine hiyo ndiyo ilikuwa fedha pekee ya matibu kwangu, nauli n.k. Apate anacho staili kwa wizi wake huo. Hata kama hali ni ngumu, upendo na uadilifu udumu baina yetu kama binadamu na zaidi tukiwa Watanzania.
 
Tena huyo jamaa ni mstaarabu mno! Kakuachia hadi I'd! Wengine hawanaga moyo huo! Ningekuwa Mimi hata hizo I'd zako ungezigomboa kwa hela! Mjini hapa!
 
Wallet za kiume uwa tunaweka mfukoni mwa suruali tunaitoa pale tunapochukua fedha ama kitambulisho na kuirudisha tena kwenye mfuko sasa wewe ulibeba wallet ya kike hadi umesahau kizembe hivyo maana huwa wanazishika mikononi!
 
Watu wanakula mingo mpaka makanisani, we unaduwaa hosii? Hii dunia tulipofikia walimwengu wacha tu
 
Pesa ilivyokuwa ngumu hata ukifukia na maiti kaburini watu watafukua
 
Unaambiwa maradhi yote umwa lakini kuchacha usiombee, sasa hiyo naye alikuwa anaumwa maradhi ya kuchacha kaja hospitality kutafuta tiba .
 
Huyo mwizi atakuwa na ujamaa na Sizonje tu, huruma kwake haipo wala haujui ubinaadamu.


Ndukiiiii
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom