Mwizi asalimisha maisha yake kwa Yesu Kanisani baada ya kuponyoka kipigo

hasason

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
1,648
1,538
Mtu mmoja ambaye alikuwa akishiriki vitendo vya wizi alijikuta akimpa Yesu maisha yake hapo jana mara baada ya kukimbilia kanisa la The Oasis Healing Ministries lililopo nyuma ya jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam, mara baada ya mwizi huyo kukimbilia kanisani hapo akisalimisha maisha yake baada ya kuiba alikotoka.

Mwizi huyo ambaye hata hivyo GK haikupata jina lake, mara baada ya kukimbilia kanisani hapo, aliweza kuhubiriwa neno la Mungu ambalo alilipokea na kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake na kuahidi kuendelea kumshika na kumkiri Yesu, hata kokote atakapopelekwa na jeshi la polisi ambao walifika kanisani hapo kumchukua mwizi huyo.

Tukio la mwizi huyo kumpokea Yesu lilipokelewa kwa shangwe na waumini wa kanisa hilo ambao walishindwa kuzuia furaha hiyo hata mwizi huyo alipopandishwa kwenye gari ya polisi, ambapo mchungaji alimuombea huku mwizi huyo akionekana mwenye utulivu.

attachment.php

Mwizi akifanyiwa maombi akiwa ndani ya gari la polisi.

attachment.php

Waumini wakifurahi tukio lililotukia.

attachment.php

Maisha yake amempa BWANA.
 

Attachments

  • kibaka.jpg
    kibaka.jpg
    38.6 KB · Views: 390
  • kibaka 2.jpg
    kibaka 2.jpg
    41.4 KB · Views: 383
  • kibaka3.jpg
    kibaka3.jpg
    36.4 KB · Views: 384
Wakati wananchi wanamdundaaa kwa mawe , aliona mkono wa " mzungu" unamuita kutoka mawinguni akiwa sero ndio alisikia sauti ya bwana ikimwita SASA KAOKOKA
 
Lazima muwe waangalifu matapeli kibao. Yametukuta kanisani kwetu. Likarudi kuiba hapo hapo kanisani. Limepotea
 
Back
Top Bottom