Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Zamani wakati nilipokuwa mtoto, ilikuwa ni aibu kubwa mtu kuambiwa amefumaniwa. Kama ni vijijini, wapiga ngoma wa kijijjini wakiongozwa na Manju wao walitunga nyimbo kuzungumzia jambo hilo. Kufanya mapenzi kiholela, iwe mjini au vijijini, lilikuwa ni jambo linalotazamwa kwa jicho la bezo.
Leo hii, kujamiiana kunachukuliwa kama moja ya burudani muhimu sana. Kwa hiyo watu kutoka nje ya ndoa zao, ni jambo ambalo linafanyika kama kwamba, ni sifa muhimu sana. Siku hizi mtu anaweza kufanya jambo hilo na yeyote, mradi tu amepata nafasi ndogo ya kujificha.
Labda hata wewe unaweza kushangazwa na jambo hili, kuna wakati mwanaume anaanza uhusiano wa kimwili na mke wa mtu, huku akijua hilo ni kosa. Lakini baadae mwanaume huyo huanza wivu kwa mwanaume halali wa mke husika . Ajabu eh!.............. Je unadhani huyu mwizi ni kichaa? Hapana, inakuwa hivyo na ndio maana watu hufumaniwa!
Wataalamu wa saikolojia wanasema, kwa mfano, mtu anapofikia mshindo wakati wa tendo, anakuwa ameingia kwenye ukaribu wa kiwango cha juu na mtu aliyeshiriki naye tendo. Baada ya tendo hilo choyo huanza, na hapo muhusika anaanza kuingia kwenye hofu ya kuachwa na hivyo anajikuta akitaka kudhibiti mienendo ya huyo mke wa mtu, jambo ambalo linaweza kupelekea kufumaniwa kwa urahisi Kwa hiyo ukiingia kwenye uhusiano na wake za watu, basi ujue ipo siku utafumaniwa tu