Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli

Unajua ndg hata Mimi kwa Mara ya kwanza nilikua namheshimu sana, ila alipofika mahali akashindwa kuheshimu wenzake nami kuanzia hapo nikaondoa heshima yangu. KUMBUKA JIHESHIMU NAWE UTAHESHIMIKA. Akiwashimu wenzake nae ataheshimika.
 
Wanabodi,

................... hivyo Magufuli naye ana madhaifu yake ikiwemo kupenda misifa, kuropoka na kufanya maamuzi ya papara na kukurupuka ila kwa vile ndie kiongozi wetu Mkuu, kuna mambo ambayo hatupaswi kuyasema hata kama ni kweli, ikiwemo kumuita rais ni muongo hata kama ni kweli sometimes ni muongo hatupaswi kusema rais ni muongo.

Mungu Ibariki Tanzania.

Pasco.

mkuu, naona hapo (kwenye red) umemwita mkulu kwa staha sana.

asante kwa hili somo.
 
Magufuli si malaika ! ni binadamu kama wengine ! Anawaza,analala,anakula nk kama wengine tu ! Cha msingi tujaribu kumsoma kiongozi wetu kuwa nini ilikuwa dhamira yake kwenye jambo fulani ! Rais anaweza akawa na dhamira fulani njema juu ya jambo fulani lkn akateleza tu ktk namna kuliwasilisha kwa wahusika,Rais ni binadamu kama wengine tu jamani,Cha msingi ni sisi kujiongeza kwa kumuelewa rais wetu anataka nini na nini dhamira yake juu ya jambo fulani tutaishi kwa amani sana.
Dhamira yake nikuhakikisha CCM inatesa watu...
 
Nakumbuka GOD bless Lema aliwai pandisha huzi kuwaonya watoto wa ufipa kua Rais haziakiwi nazani siku ile LEMA alikua hajavuta.. Maana juzi nimeshangaa huyu alietoa ushauri kwa vijana wa ufipa na yeye amepita mulemule
Rekebisha hizo herifu kwanza Ndio mazo ya MULUGO nini...badala yakuandika nadhani...unaandika NAZANI
 
Nimeusoma uzi mpaka mwisho
Nikaurudia tena mwanzo mwisho
Hivi nataka nianze kuusoma tena
--kwa kifupi SIJAELEWA mkuu pasco unamaanisha nini, yani nisaidie kwa kifupi watanzania tunatakiwa tufanyeje?
 
Hiyo ni dhana ya kutimiza takwa la demokrasia.

Hata kwenye nchi kama Uingereza kuna sehemu/constituents ambazo zinafahamika ni ngome ya chama fulani au mtu fulani lakini haijatokea wakaacha kufanya uchaguzi kwa sababu eti ni kupoteza muda na pesa pamoja na kwamba hata kabla ya kufanya kampeni na uchaguzi wanakuwa wanafahamu mshindi ni nani au chama gani.

Rule of law is much more likely to be shaped by local culture as well as history.

Local culture and history is a source of selective law.
Luna ulazima nasisi kuiga hayo? Mbona tunaiga yaKIJINGA na mazuri wanayofanya hatuigi
 
Pasco wacha nyeupe iitwe nyeupe na bluu iitwe bluu. Wewe mwenyewe ni kama umepigia mstari yale yote unayoyakataza kwa sababu hakuna namna ndiyo ukweli wenyewe
 
Magufuli si malaika ! ni binadamu kama wengine ! Anawaza,analala,anakula nk kama wengine tu ! Cha msingi tujaribu kumsoma kiongozi wetu kuwa nini ilikuwa dhamira yake kwenye jambo fulani ! Rais anaweza akawa na dhamira fulani njema juu ya jambo fulani lkn akateleza tu ktk namna kuliwasilisha kwa wahusika,Rais ni binadamu kama wengine tu jamani,Cha msingi ni sisi kujiongeza kwa kumuelewa rais wetu anataka nini na nini dhamira yake juu ya jambo fulani tutaishi kwa amani sana.
Busara ni kumwambia umeteleza na siyo kukaa kimya au kumsifia. Kumwambia kiongozi kuwa kateleza ni vizuri kwani atajua kuwa nia yake njema haikutekelezwa. Hivyo atapata nafasi ya kujiuliza "kwa nini?"
 
Pasco, kila kukicha unadhihirisha jinsi ulivyo intellectually weak. Hii tabia ya kujikomba imelitia taifa kilema ambacho inashangaza kuona mtu kama wewe unatumia nguvu kubwa kukipalilia.
Kwa nini usimshauri yeye kwanza awe na lugha ya staha na nidhamu hasa akitambua kuwa anapaswa kuwa mfano nambari moja?
It's hard to respect a polarizing figure.
 
Asante mkuu Pasco umelifafanua hili vizuri sana. Hiki ndo wakosoaji wengi wameshindwa na kufanya hoja zao zionekane mfu maana hawafanyi constructive criticism wamekazana tu na character assasination sasa hii inawashushia credibility maana kila wanachosema mbele ya watu wenye akili kubwa wanaishia kudharauliwa na kupuuzwa..
 
Pasco, kila kukicha unadhihirisha jinsi ulivyo intellectually weak. Hii tabia ya kujikomba imelitia taifa kilema ambacho inashangaza kuona mtu kama wewe unatumia nguvu kubwa kukipalilia.
Kwa nini usimshauri yeye kwanza awe na lugha ya staha na nidhamu hasa akitambua kuwa anapaswa kuwa mfano nambari moja?
It's hard to respect a polarizing figure.
Mnataka awe na lugha za staha wakati nyie ndo mlianza provocation. Hebu jaribu kuvuta kumbu kumbu ya matukio ya wakati wa lile sakata la UDOM. Mnafanya character assassination badala ya kufanya constructive critisism..Mlitaka kumjaribu sasa mmeshindwa kwa nia yenu ovu mkiwa mnatumiwa na wafanyabiashara mafisadi...
 
Huyu Pasco alishanijibu hoja yangu kuhusu kuvuga uchaguzi, akaniita kuwa at I ni Mwendawazimu na Mropokaji. Anatmiaga kale kakitabu kakuukuu ka kuita MTU uliyemshindwa kwa hoja kichaa, mgonjwa etc! Na ukisikiliza Kampeni za CCM hawana mtaji mwingine. Huyu Pasco anasaka tonge kwa mtindo huu.
 
Nikuulize Pasco nani Kakupa Mandate ya kumonitor watu hapa, jinsi gani watoe mawazo yao au hisia zao kwa Magufuli? Kama Magu ni Mungu wako Katengeneze sanamu yake uiweke chumbani mwako na ukitaka hata usiku ukilala ihamishie kitandani mwako. Ila jiepushe na kutaka watu wafanye, wawaze au waseme utakavyo wewe.

Kwangu Mimi MTU mnafiki anayesema Mwingine akiumwa aachwe are kisa hajampa mkono, MTU mwenye hila za wazi, Sina haja ya kumzungumzia Kiungwana. Kwangu Mimi kaheshima kadogo kalikobakia kwangu juu ya Magufuli ni Juu ya hicho Kiti alichokalia na sio kwake yeye. That man is hypocrite, the man is sneaky, a liar, Vindictive, oppressor and do not have a pint of respect to the constitution. To hell will all dictators what good are they?
 
yaani tufanye "a constructive criticism" kama kuna mahali amekosea, au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme kwa lugha ya heshima na staha, kisha tuweke na ushauri wa the right thing to do, hivyo ukosoaji huu utakuwa unamsaidia rais wetu na kuisaidia nchi yetu.
Rai nzuri sana kwa nchi kama yetu inayoendeshawa kidemokrasia na utawala bora na kuheshimu haki za msingi wa kutoa mawazo na maoni kwa kila raia. Lakini kutokana na karne za utawala wa " iron rule" na hivyo kufanya taasisi nyengine hasa za usalama na utengemano kujengeka na imani ya kuchukia ukosoaji wa aina yeyote,na kwao huona ni tishio tu.Katika hali kama hii iliozoeleka ni vigumu kukosoa kwa dhati na nafasi bila ya kuiweka nafsi yako katika wasiwasi. Mpaka hapo taasisi hizi zitakapoelimishwa na kuelemika itakuwa vigumu kwa mtu mwenye akili timamu kuogelea kwenye bahari yenye mkondo huu.
 
Mie naona kama anajificha nyuma ya'Satire'
Hii nimeiona hata kule kwenye issue ya Majina ya Mwigulu Nchemba
Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli
Pasco unaandika unatetea weeee mambo ya ajabu kabisa unayatetea, alafu unangoja uzi unakuwa mrefu, watu wakikukosoa sana unaanza ku-'insinuate' kwamba watu hawajakuelewa, kwamba hawajui kusoma between the lines, yani kwamba ujumbe unaoutoa uko between the lines za kwenye post yako, Why!
Hapana naanza kupata wasiwasi kwamba unajificha nyuma ya 'satire'. Kwenye mitandao unataka watu wakuelewe 'in between the lines", lakini kwa wale unaowatetea unawatumia ule ujumbe original ulioko kwenye actual lines za hizi post zako.
Noooooo pasco... too unatractive
 
You can't constructively criticize a person who can't think constructively. Sijui umenipata hapo?
Mnataka awe na lugha za staha wakati nyie ndo mlianza provocation. Hebu jaribu kuvuta kumbu kumbu ya matukio ya wakati wa lile sakata la UDOM. Mnafanya character assassination badala ya kufanya constructive critisism..Mlitaka kumjaribu sasa mmeshindwa kwa nia yenu ovu mkiwa mnatumiwa na wafanyabiashara mafisadi...
 
Back
Top Bottom