Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!



Very diplomatic. Sophia Simba sijui ni member hapa JamiiForum asome hii? :)

Hata akisoma... kwa personality yake [na baadhi ya wale wanajiita wenye chama na wenye nchi], hataelewa... KUNA MHADHIRI MMOJA ALISEMA WATU KAMA SOPHIA WAKO KWENYE STATE YA POLITICAL CORRUPTION - KESHALEWA YULE

HIVI SI KUNA WAKATI KIRANJA WETU M.M.MWANAVILLAGE ALIMTETEA HUMU JAMVINI!!!? I HOPE ALIPITIWA TU

DUH
 
Vita iliyopo ndani ya CCM ni ya kuwadhofisha na kuwasambaratisha CCM.
Hakuna mfumo wa aina yeyote Duniani ujiwekao imara na kujiendesha bila kutengeneza chanzo cha kifo chake. Meaning nothing will last forever.
Wana CCM na viongozi wake wamekuwa na mapenzi na pochi kwa muda mrefu sana na kusahau misingi iliyojenga umoja wao.
Kitendo hicho cha kuweka pembeni kanuni za kujenga umoja wa kweli ndani ya chama pekee yake kinatosha kuunda mfumo wa kifo cha CCM.
Mpaka dakika hii Viongozi wengi wanashindwa kuondoka ndani ya CCM kwa sababu kitendo hicho kitawanyima Fedha ya bure, lakini wanajua wazi kwamba CCM haiwezi kujiponya na ngendembwe ndani ya mfumowake dume.
Wafanya biashara nao wanashindwa kuipa Bye CCM kwa sababu ilisha watangazia wazi kwamba njea ya CCM hakuna Biashara.
Watakuletea watu wakague biashara yako hata mara 7 kwa mwezi, wata kusingizia kwamba unashirikiana na majambazi usiku na mengine mengi machafu.

Tatizo si kwamba CCM iko imara, tatizo ni sisi wananchi kushindwa kuamini kwamba CCM ndo inaelekea kaburini hivyo kuchukua nafasi hiyo kuweka mambo sawa.
Wananchi bado tunaamini kwamba HAKUNA BADALA CCM,CCM WAPO NA WATAKUWEPO.
kwa nini tunaamini hivyo,
Tunaamini hivyo kwa vile wananchi tumenyanyasika kwa muda mrefu na mfumo huu uliofuga Wala rushwa,wezi, wazinzi wakubwa na majambazi, hata nzi wakipitapita juu ya vichwa vyetu tu hofu inatujaa mpaka makalioni kwa kuamini nzi hao si nzi bali ni Unmanned devices za kupiga Rec za usalama wa Taifa, wapi bwana, kumbe ni nzi tu.

Unyonge wetu hautapata nguvu kwa kuendeleza unyonge mara 2 zaidi ya huu tulio nao bali utatoka tu kwa kutumia unyonge wetu kama jumping stone.mnyonge mmoja akimpa nguvu mnyonge mwingine hutokea wanyonge wawili wenye nguvu.
Wanyonge wawili wenye nguvu ni bora kuliko wanyonge wote Tanzania waliojaa hofu mpka kwenye meno.
Kwenye ile Riwaya ya Tende Hogo mwandishi Kaduma alibainisha wazi kwamba.
HAFIFU NA HAFIFU NI SAWA NA BORA NA BORA. wengi tulisoma Riwaya hiyo na kuacha palepale shuleni ndani ya chumba cha kidato cha 3.

Maana yake riwaya hii ni,akina Sekalinga, Gwimile, Madilu, Haggai Semfukwe,Pa tebo Mwamukonda, Nshomile Lushakuzi Babangu Mushi, Sekibaha,Dzudzu wa MWanza na Mobitelinauyuatoking kutoka Mtwara na Watanzania wote wanyonge wakiungana pamoja umoja wao unanguvu zaidi ya akina
Lowassa,Rostamu,Chenge, Pinda,Kikwete, Mwiru,Manji,Idrissa na Matapeli na Mafisadi wote pamoja wakiungana.

Alutye pe ndi nywaa ulasi... Mapambano bado hata hajaanza.
 
Last edited:
Kwa nilivyomuelewa SS, Janet Kahama alikuwa anapambana na nguvu kubwa sana kule UWT, ule uenyekiti asingeweza kuupata, nampa pole kwa mitusi aliyopokea
 
Jamani haiwezekani kwa jinsi yoyote na kwa namna yoyote kuwa hawa wote JK, PINDA, MENGI, sofia simba lao moja??

NAJUA SHERIA ZA BARAZA LA MAWAZIRI, kuwa hawatakiwi kupingana katika statement zao, so aidha Sofia alikurupuka, au Pinda! maana statement za hwa mawaziri mara nyingi zinakuwa zimekaliwa kikao prior to release!

sasa nachanganyikiwa ina maana baraza la mawaziri Tz halina disprin kiasi hiki? wanatueleza nini wananchi??
 
Naomba mnisaidie. Zaidi ya mara moja, nimeona sura ya Sofia Simba akikalia makochi ya kanisa la Mama Lwakatare huko Mikocheni B. Kama ndiye, je ameokoka, na ameanza kuokoka lini, ama huenda kama Mgeni rasmi?

Mie nadhani Sofia Simba hakutumwa na Baraza lolote la Mawaziri bali amekurupuka mwenyewe tu na mipasho yake ya watoto wa mjini. Inadhihirisha ni mapungufu ya aina gani waliyonayo wateule ambao hawana uwezo na hawajui wanapaswa kufanya nini! HEKIMA NI MUHIMU!

Mungu Ibariki Nchi Yetu! ...... Wabariki Viongozi wake...., Hekima, Umoja na Amani....!
 
Safari bado ndefu

Ikulu yamuonya Reginald Mengi

*Yamtaka aheshimu vyombo vya dola
*Yasema athibitishe tuhuma alizotoa
*Yakanusha taasisi zake kumuandama
*Jeshi la Polisi latamka kumchunguza

Na Waandishi Wetu

SIKU moja baada ya mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Reginald Mengi, kutoa madai mazito ya kuandamwa na baadhi ya viongozi wa serikali na taasisi za dola, Ofisi ya Rais Ikulu, imetoa tamko la kumuonya, ikimtaka aviheshimu vyombo vya dola.

Imesema Mengi anapaswa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili viweze kufanyia kazi tuhuma za ufisadi alizozitoa katika vyombo vya habari dhidi ya wafanyabiashara watano kati ya kumi aliodai kuwa ni mapapa wa ufisadi hapa nchini.

Aidha, Ikulu imekanusha madai ya Mengi kuandamwa na baadhi ya viongozi wa kiserikali pamoja na taasisi zake, na kueleza kuwa, anapaswa kutoa ushahidi na vielelezo vya tuhuma alizozitoa dhidi ya wenzake, ili ziweze kufanyiwa kazi.

Msimamo huo wa Ikulu dhidi ya kauli za Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, ulitolewa jana na Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, Premi Kibanga, katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima Jumatano kupitia simu yake ya kiganjani.

“Mengi anavyosema ameandamwa sasa, ameandamwa vipi? Alitoa sijui tuseme ndiyo kashfa au tuhuma za ufisadi, kwa hiyo ulikuwa ni wajibu wa vyombo vinavyohusika kumwita ili atoe ushahidi na vielelezo vyake ili viweze kufanyiwa kazi.

“Hakuitwa yeye tu, ameitwa pia Rostam Aziz, katika idara zote hizo. Hawa wote walitoleana kashfa za ufisadi na wote waliitwa ili watoe ushahidi wao. Sasa kwanini Mengi anasema ameandamwa?” alihoji Kibanga.

Akizungumzia kauli ya Mengi kuwa anamtegemea Rais Kikwete kumnusuru, Kibanga alisema kama anadai hivyo basi anao wajibu wa kumsaidia katika vita ya ufisadi.

Alisema anapaswa kutumia nafasi hiyo si tu kwa kuwataja mafisadi, bali pia kwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vyote vya dola vilivyo chini ya Rais Kikwete, ili viweze kuufanyia kazi ushahidi wake na kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya wahusika, ikiwa watathibitika kufanya ufisadi.

‘‘Vyombo vya dola havimwandami mtu. Na anaposema rais atamlinda, ni vema akaelewa kuwa Rais Kikwete ni rais wa wananchi wote. Rais Kikwete halindi mtu mmoja mmoja, analinda Watanzania wote.

‘‘Kama yeye ni rafiki wa Kikwete, basi autumie urafiki huo vizuri kama anavyofanya katika vita ya ufisadi. Lakini sasa asiishie tu katika kuwataja mafisadi, maana sasa kila mtu tu akitaja fulani fisadi kutakuwa na utulivu kweli? Yeye aviheshimu vyombo vya dola na amsaidie rafiki yake (Kikwete), kwa kuvipa ushirikiano vyombo hivyo,” alisisitiza Kibanga.

Naye Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, alipohojiwa na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu madai ya Mengi kuandamwa na taasisi za dola, likiwamo Jeshi la Polisi, alisema anachojua ni kwamba, polisi wanamchunguza Mengi, lakini hawamuandami.

Manumba alikataa kuzungumzia suala hilo kwa undani, kwa maelezo kuwa msemaji wa jeshi hilo kuhusu suala hilo ni mkuu wa jeshi hilo, Inspekta Jenerali Said Mwema.

Gazeti hili lilipomtafuta Mwema kupitia simu yake ya kiganjani, ilipokelewa na msadizi wake ambaye alikataa kutaja jina lake na kueleza kuwa yupo katika kikao.

Hata hivyo, alipoulizwa kama anaweza kuzungumza lolote kuhusu madai yaliyoelekezwa kwa jeshi hilo na Mengi, alisema si madai ya kweli, kwa sababu jeshi hilo halina kawaida ya kufanya kazi zake kwa kumwandama mtu.

‘‘Hakuna chombo cha dola kinachomwandama mtu. Jeshi la Polisi linafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria, kanuni na maadili yanayoliongoza, lakini kama unataka kupata taarifa zaidi kuhusu kinachofanyika kwa sasa, wasiliana na Kamishina wa Utawala na Rasilimali Watu, CP Clodwig Mtweve.

Kamishina huyo alipotafutwa, hakuweza kupatikana na simu yake ya kiganjani ilikuwa haipatikani.

Jumapili iliyopita, wakati Mengi akizungumza katika ibada iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Kisereny wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, alisema baada ya kutaja majina ya mafisadi papa, alianza kuandamwa na baadhi ya mawaziri, vyombo vya dola na taasisi za serikali.

Huku akishangiliwa na umati wa waumini wa kanisa hilo lililopo katika eneo la kijiji alichozaliwa, Mengi alimtaja waziri wa kwanza kumwandama kuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba.Mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dk. Norman Sigalla na Mbunge wa Hai, Fuya Kimbita (CCM).

Mengi alimtaja waziri mwingine aliyemwandama baada ya kutaja mafisadi papa kuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, aliyesema alimwita mbaguzi wa rangi.

Alisema mbali ya mawaziri hao kutoa kauli hizo, pia wahariri wa magazeti yake anayoyamiliki, walihojiwa na Msajili wa Magazeti wa Idara ya Habari.

Huku waumini wa kanisa hilo wakiwa kimya, Mengi alisema yeye mwenyewe pia aliitwa na kuhojiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ikidai alivunja sheria ya utangazaji kwa kutaja majina ya watu kuwa ni mafisadi papa, na kwamba hatua hiyo iliashiria ubaguzi wa rangi.

Mengi ambaye alikuwa mgeni mwalikwa kwenye hafla hiyo, alivitaja vyombo vingine vya dola vilivyomwandama kuwa ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ikimtaka apeleke vielelezo.

Pia alisema aliitwa na maofisa wa Jeshi la Polisi, linaloongozwa na IGP, Said Mwema, chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, inayoongozwa na Laurence Masha, wakimtaka apeleke vielelezo vya tuhuma zake.

“Nimeitwa na Kamati Ndogo ya Ulinzi na Usalama wa Taifa ili kuhojiwa juu ya tamko langu kuhusu ufisadi. Yote haya yamefanyika pamoja na kwamba kuna kesi mahakamani juu ya jambo hili.

“Tukumbuke kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alikwishatoa tamko bungeni kuwa wote waliotajwa, kama wanaona hawakutendewa haki, waende mahakamani. Sasa ni nani ana tamko la mwisho katika hili? Ni mawaziri, taasisi za serikali, vyombo vya dola ama Waziri Mkuu?

“Kama raia wa Tanzania, vyombo vya dola ni moja ya mategemeo yangu ya kunilinda mimi na mali zangu, kama raia wengine, lakini pamoja na kusakamwa na vyombo hivyo, nasema siogopi. Ulinzi wangu unatoka kwa Mwenyezi Mungu, pili utatoka kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye naamini hatakubali kuona sitendewi haki, na tatu ulinzi wangu utatoka kwa Watanzania wanaochukia ufisadi, hasa masikini na wanyonge.

“Hawa hawana fedha nyingi, ama madaraka, lakini wana nguvu ya sala na umoja bila kujali dini zao,” alisema Mengi na kushangiliwa na waamini wa kanisa hilo.

Alisisitiza kuwa, hatarudi nyuma katika msimamo wake wa kupiga vita ufisadi, kwani anaamini rushwa ikiachwa bila kukemewa, wananchi watagawanyika katika makundi mawili; la watu wenye kipato na madaraka na la watu masikini.

“Watanzania wenzangu wanaochukia umaskini, wanaochukia ufisadi, ndugu zangu waumini, nawaomba mniombee na tuimbe wimbo namba 59 katika kitabu cha ‘Mwimbieni Bwana’, usemao ‘Kazi ni yako Bwana’,” alisema.

Hatua ya Mengi kutoboa siri ya kusakamwa kwake mara baada ya kutaja majina ya aliowaita mafisadi papa, ilitokana na mahubiri ya Mhashamu Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shayo, aliyeunga mkono harakati zake katika vita dhidi ya ufisadi.

Askofu huyo alimtaka Mengi asikatishwe tamaa na wajanja wachache, ambao wamekusudia kurejesha nyuma juhudi za kujiletea maendeleo.

“Taifa letu limegubikwa na mafisadi wachache, wapo Watanzania wenzetu kama Mengi, wamekuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya kifisadi, lakini wanakwamishwa na baadhi ya viongozi walioko madarakani, tukemee kwa pamoja.

“Mwaka huu na mwaka ujao, ni vipindi vya uchaguzi mbalimbali, kuna watu wamejaa choyo, wivu, chuki na ubinafsi miongoni mwetu, hakika watu hao ni wabaya kwa maendeleo ya taifa, msiwachague,” alisema.

Alisema, Mengi hataki urais wala hana nia ya kuwania kiti hicho, wala uongozi wa aina yoyote, lakini amejitoa kusaidia wanyonge, na rafiki zake ni masikini, walemavu, wajane, wanaoishi na virusi vya VVU pamoja na wenye matatizo mengine ya kijamii.

Source: Tanzania Daima
 
Last edited:
kazi hipo kweli kweli.hivi kwanini ikulu hawakutumia vyombo vya habari zote kutoa taarifa hii mpaka wameenda kutumia tanzania daima tena kwa kupitia simu ya mkonononi kuwapa habari tanzania daiama.kuna ugumu gani wa kuitisha mkutano na vyombo vya habari?
 
kazi hipo kweli kweli.hivi kwanini ikulu hawakutumia vyombo vya habari zote kutoa taarifa hii mpaka wameenda kutumia tanzania daima tena kwa kupitia simu ya mkonononi kuwapa habari tanzania daiama.kuna ugumu gani wa kuitisha mkutano na vyombo vya habari?
Kumbuka,

Tanzania Daima hawa hawa ndio waliandika habari kwa kumwandama Mwakyembe huku wakidai waliongea na dereva wa Lori (ambaye hata hivyo hajakamatwa na wala hajulikani alipo) kwa simu na simu hiyo wanayodai walipigiwa na dereva wa lori lililosababisha ajali bado ilikuwa ni Private number, sasa jiulize, Tanzania Daima wanaandika habari za credibility kweli?

Kwanini watumiwe sasa? Mbowe vipi? Kuna mwandishi mmoja namfahamu ambaye huwa anampoteza step Martin Malela naye anaingia kichwa kichwa.

Tanzania Daima wanapoteza mwelekeo, wanatakiwa kujiangalia upya.
 
Tanzania Daima ni gazeti la serikali? Lile gazeti la CCM, 'Uhuru' bado lipo? Naona Tanzania Daima linaongea kwa maslahi ya watu fulani fulani wanaohusishwa na ufisadi. Wangebadili jina na kuliita "Tutainyonya Tanzania Daima"!
 
Tanzania Daima linatia aibu sana siku hizi! Si mie tu lakini wapo wasomaji wenzangu kadha wa kadha ambao wameishaona mabadiliko makubwa kuhusu waandishi wa gazeti hilo akiwemo Mhariri Mkuu wa gazeti hilo. Hata kwa mtu asiyekuwa na akili ya kikachero ataweza kugundua kwamba hawa jamaa huenda kwa namna moja ama nyingine wamenunuliwa ama wanaandika kutokana na shinikizo fulani!

Inasikitisha!
 
Haya magazeti yakisiasa yanaandika ujinga. I'm glad I'm not currently privy to their dauly publications at least not more than the online versions lakini naona the quality of the work is low and most of the news is either not news at all or is so speculative and unauthoritative that it screams dessacration of the media to anyone with a due level of respect for respectible journalism.
 
Hivi ni kweli mawaziri wanaweza kuja na kusema hayo waliyosema bila ya kuona haya?. Nashindwa kuelewa na kuamini walipataje uwaziri. Wanasema Kwamba Mh. Mengi hana haki ya kuwataja mafisadi aliowataja kwani nani katika Tanzania ya leo asiyejua kwamba waliotajwa na Mengi ni mafisadi?. Alichofanya Mengi ni kuonesha ujasiri wa kuwataja hadharani lakini 98% ya watanzania tunawajua na tulikuwa tunajua kwamba waliotajwa na Mengi ni mafisadi. Na hawa mawaziri wawili toka lini wamekuwa wasemaji wa serikali?. Kwanini kimbelembele?.

Mawaziri wote wanaotetea ufisadi wamenufaika nao kwa asilimia 100,sasa wasipofanya utetezi watahojiwa na mafisadi waliowaweka madarakani ili kulinda ufisadi its that simple and clear to most of us.
 
  1. Imekuwaje tena whistle blowing ikawa ni sawa na kuhukumu mtu?
  2. Hivi kazi ya vyombo vya sheria sio kuchukua tetesi na kuzichunguza?
  3. Iweje tena mtoa tetesi aanze kusimangwa na serikali badala ya kupewa ulinzi ili asaidie uchunguzi?
  4. Kama hata mtu kama Mengi shutuma zake juu ya ufisadi zinamgeuzia kibao yeye mwenyewe, ni nani tena atakayethubutu kufungua mdomo unless iwe ni mitandaoni (JF) n.k?
Hii ni wazi kuwa serikali yetu iko madarakani kutokana na nguvu za kifedha za hao mafisadi.


Huo ndio ukweli halisi.


Swali langu ni kuwa kwa nini Bunge letu ambalo ndilo chombo pekee chenye uwezo wa kumchukulia JK hatua, linaendelea kuwa kimya wakati ni wazi kuwa JK ndiye anayewalinda wanaoimaliza nchi?

Bunge letu limekwenda likizo na hata kama linafanya kazi halina meno kwani wabunge walio wengi ama wamefaidi matunda ya ufisadi kuwawezesha kufika bungeni au wanamatamanio hayo.Na kama hali ndiyo hii unategemea wataweza kumwajibisha JK wakati makakati wao wote ni kuwalinda mafisadi.

Kama sio kweli haya tuyasemayo basi Bunge lionyeshe linauwezo wa kumwadhibu mkuu wa kaya kwa kuwalinda mafisadi halafu tuone itakuwaje.Siasa za Tanzania ni kama mchezo wa kuigiza na hali hii inasikitisha sana. Tanzania ya leo imekosa mwelekeo.
 
matatizo makubwa sio kwa wabunge wala mawaziri bali ni mkuu wa nchi, frank speaking mkulu angetoa kauli positive kuhusu mafisadi hakuna hata waziri mmoja ambaye angeongea ujinga, ni kama kwenye familia kiongozi akiwa kimya basi familia lazima itetereke kwa sababu kutakuwa hakuna mtu wa kuwakemea,hakuna kiongozi ambaye angekumbukwa tanzania kama kikwete akichukua uhamuzi sahihi wa kupapmbana na hao jamaa, mimi na uhakika angepata support ya watanzania wote na tayari watu wangekuwa tayari kufa kwa sababu hiyo, anachotakiwa kufanya ni kitu kidogo tu, kuweka urafiki na uswahiba pembeni kisha afanye kitendo
 
Pole Mzee mengi lakini mwaka huu Utakijuwa kilicho mfanya kuku kunywa maji shingo juu .umechokoza dola kubwa ambalo hata hao waliokupa ule utambulisho wa Dr Martin Luther King wanaelewa kishindo chake. Rostam sio wa kuchezewa na Wa TZ
 
watasema mpaka ithibitishwe na vyombo yva sheria kwamba wana hatia ndio serikali ichukue hatua. inakuwa je hii?
 
kazi hipo kweli kweli.hivi kwanini ikulu hawakutumia vyombo vya habari zote kutoa taarifa hii mpaka wameenda kutumia tanzania daima tena kwa kupitia simu ya mkonononi kuwapa habari tanzania daiama.kuna ugumu gani wa kuitisha mkutano na vyombo vya habari?


Wahenga walinena, penye njaa penyeza rupia!!!!
 
Humu ndani mnaboa na hawa MASIHA FEKI wenu....wote hawa lao ni moja...kuokoa uhalali (legitimacy) wa tabaka tawala....kulinda mfumo fisadi wao......kutudanganya eti CCM yaweza kubadilika.....kupigania nguvu za ushawishi ndani ya Madhabahu yao ya ufisadi.....

Kung'ang'ania uokozi kutoka kwa MASIHA FEKI hawa ni alama za uoga wa ninyi binafsi kuwa sehemu ya mabadiliko...ni uoga wa kujiangalia mapungufu yenu yanayolea na kuendeleza uhalali wa mfumo huu fisadi...

Watanzania tunaweza kufanya makubwa zaidi ya huu ushabiki pofu unaondelea...

omarilyas
 
Back
Top Bottom