Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Sofia aliwagawia akina mama wenzie kiasi cha fedha kadha je inapokuwa wakati wa kuhonga akina baba nadhani huwapa mamilioni.....!!!!, lakini mnamjua Sofia tangu alipoanza kusoma cheti cha sheria hata kwenda mlimani kuchuakua sheria. Watanzania tunajua mengi lakini itafika wakati babu atataka kusema.

KAHINDA Hapa ni JF we talk openly,
Tafadhari sana huyo babu muache aseme, tunataka tujue huvu vuperege vunavo anza kutetea mapapa ya ufisadi, Hata hao mapapa yalianzia hatua za perege-kambale.., kwa kuanza kuona ufisadi ni jambo sahihi, bila aibu wala woga kusimama mbele ya kadamnasi kuutetea!

Ili tusivuruge mada, tafadhali huyo bubu kama anajua lolote aweke kwenye thread yake tuchambue kama karanga!

Kakitikisa kiberiti wacha kimuwakie, hakujua yupo kwenye nyumba ya vioo kaanza kurusha mawe... lete dozi kamili babu.
 
Omulangi, nakubaliana nawe sana. Wale wote wanaowatetea hawa mafisadi watuambie kwanza, je ni kweli shutuma zinazoelekezwa kwao ni sahihi au zimetungwa? Inachekesha pale unaposikia baadhi ya viongozi fulani Serikalini wakidai kuwa hawamjui mmiliki wa Kagoda, alkini hapo hapo wanadai kuwa Kagoda wamerudisha kiasi fulani cha pesa, hivi huyu Kagoda ni jini? Anuani za usajili wa Kagoda zinaonesha ni za mtu fulani, alkini watanzania hawajaambiwa mpaka leo, mwenye anuani hizo kasemaje kutumika kwa anuani zake ktk usajili wa kampuni tata ya Kagoda? Tunaambiwa Richmond haina uhusiano na Dowans, lakini aliyekuwa anafuatilia masuala yoote ya hela Bank za Richmond ndio yule yule aliyekuwa anafuatilia hela za Dowans, hapa ni nani anadanganywa? Tufike sehemu tuseme kwa dhati ya moyo wetu kuwa, "Enough is Enough"
 
Manyerere anasema ktk makala yake kuwa mzee Mengi aligombana na magwiji wa habari, akamtamka Salva Rweyemamu... Jackton, are you serious na ulimi wako kweli? Hapa umepotoka, nakushauri uachane na suala hili kwani ulikoegemea sio kwenyewe kabisa, unapoteza umaarufu wako na kuonyesha udhaifu wako dhidi ya mafisadi wanaolihujumu Taifa hili huku ndugu zako wakiteseka kwa shida kijijini.
 
Kuna mambo fulani si vizuri kuyaacha yakifanyika nasi tukajifanya hatuyaoni au business as usual. Ndugu zangu watanzania, tutadumaa ktk hali hii na kutengeneza primacy itakayokuja kutumaliza kama ugonjwa wa kipindupindu. Tujenge tabia ya kukemea ujinga wowote unaoletwa mbele ya Taifa letu, tusikae kusubiri mpaka jambo limeharibika ndio tuanze kusema. Wahenga walisema, kinga ni bora kuliko tiba. Mengi ameanza, nasi inabidi tumuunge mkono kwa maslahi ya nchi. Sofia na George, nawashauri muwaombe radhi watnzania, ama sivyo, tunawasubiri mwakani, tuone mutatokea wapi.
 
Mimi naona tuyapime maneno yake yupo "right", si tunakubaliana kuwa sheria za nchi zifuatwe, na shera zetu si zipo wazi kuwa " mtu hataonenakana kuwa amefanya kosa mpaka pale mamlaka yenye uwezo (mahakama) itakapotamka hivyo, baada ya kuthibitishwa pasipo shaka yoyote..."sasa "Maza" anasema kwa tuhuma kama hizo alizotoa Mengi, yeye hakuwa na mamlaka hayo. Ukizingatia kuwa kati ya aliowataja, wana kesi hizohizo mahakamani ambazo zinaendelea.
Tukubalini kuwa mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Na kwa hoja ya "Maza" ni kuwa kwanini Mengi awataje wafanyabiashara tu?
Au kwa nini kama kweli anauchungu wa uovu huu, asingeendelea kuwataja na wengine, si alisema hawazidi kumi?

Mkuu,
Hayo maneno niliyoyakuza hapo juu yana maana kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku. Endapo hatutaweza kusimamia katika sheria na utawala ulio bora katu kasi yetu ya maendeleo na mabadiliko itakuwa duni. Haiwezekani hata kidogo tuna-advocate for changes halafu tunashindwa kusimama katika misingi ya kutufikisha huko. Naendelea kusisitiza kuwa huyu Mzee hajawatendea haki aliowataja hadharani bila ya kuwasilisha vielelezo na ushahidi katika mamlaka husika.

Nakupa zawadi kutoka kwa Joe Navarro hapo chini:


"The majority of individuals view their surroundings with
a minimal amount of observational effort. They are
unaware of the rich tapestry of details that surrounds
them, such as the subtle movement of a person's hand
or foot that might betray his thoughts or intentions."
— Joe Navarro: Former FBI agent and expert on nonverbal language

Ni vema kabisa kila mmoja wetu apime mambo kutokea kwenye angle ya kisheria na kutambua ni zipi haki na wajibu wake katika jamii.
 
Mh. Mengi sio wa kwanza kuwataja hawa jamaa, Mtikila alianza zamani sana na hata akawaita Magabacholi, mwembe yanga pale Mh. R Slaa aliwaorodhesha haohao pia, swali ni nini kinachowauma hao mawaziri uchwara, Mengi alishatoa go ahead kwa yoyote kati ya ho Mafisadi papa akijisikia aende mahakamani
Mama SSimba kapata hicho cheo kwa kutumia mamilioni ya fedha na swali la kujiuliza hizo fedha alipata wapi na kwa maslahi ya nani na atalipaje fadhila, kwa hiyo kulalamika kwake si bure naona anaanza kulipa fadhirav au anajiandaa nkutafuta fedha za kampeni, lakini kwa upande wa pili kwa sisi watu wa kawaida ndio nafasi yetu murua ya kujua nani yupo upande upi (Wananchi au Mafisadi) na kwa maslahi ya nani
 
Jana Lipumba alimshambulia Mengi kwamba alikosea kuwataja mapapa wa ufisadi. Pia alisema kuwa Mengi alionekana kujikomba kwa JK kwa sababu matatizo yote ya ufisadi yanatokea na kuendelea kwa sababu ya udhaifu wake JK. Na kwamba kama JK angekuwa imara kazi ya kupambana na ufisadi ingekuwa imeisha siku nyingi.

Nakubaliana na Lipumba kwenye hoja yake ya pili ila sikubaliani naye kuhusu suala la Mengi kuwataja mafisadi. Kazi ya Mengi hadi sasa inaonesha kuzaa matunda kwani imedhihirisha jinsi hawa mapapa wanavyoongoza serikali ya JK na kuipelekesha wanavyotaka. Hadi sasa mawaziri walioongea, wameonekana kama vile ni watumishi wa RA na mapapa wenzake. Mengi anastahili pongezi kwa kazi nzuri. Pia nadhani suala la kumpamba JK ni mbinu tu ya kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Jambo lilo wazi ni kuwa Mengi ameianika juani serikali ya JK na jinsi inavyotawaliwa na mafisadi, yeye mwenyewe (JK) akibaki kuwa kuwadi tu wa hao mapapa. Hata hivyo siwezi kushangaa kwa sababu taarifa nilizowahi kupata ni kuwa Lipumba ni mtu wa usalama wa Taifa. May be yuko kazini kupunguza hasira za umma!
 
Mengi amefanya vizuri Ufisadi ulikuwa umeanza kusahaulika. Sasa umerudi upya. Kwa walioangalia baadhi ya television jana zilioji watu kila mtu anasema mengi kafanya sawa. Hii inatoa picha kuwa sasa watz wanafuatilia mambo kwa ukaribu kuliko inavyodhaniwa.

Pia Huyu jamaa amesema kuwa mengi analeta ubaguzi!! Katika nini? Kwani si kweli kuwa uchumi umeshikiliwa na hawa ngozi nyeupe kwa kuwapa mlungula watumishi maskini wa serikali ili wawezi kufanikisha mambo yao? Kikwete katajwa ili kupoteza lengo sidhani useme kuwa CCM ina Mafisadi na raisi ametoka humo harafu iwe yeye rais ameenguliwa! Hiyo haiwezekani jamaa katumia ujanja.

Huyu Lipumba naona naye anatumia mwanya huu ili asikike kuwa yupo sidhani kama kuna jipya pale kwani yote walishaongea mawaziri. Hivyo marudio.
 
Lipumba angetuambia Mengi alichokosea ni nini, kuwataja hawa jamaa au kumsaidia Mkwere katika hii vita, kama Mengi anatafuta Umaarufu kwa Mkwere basi Nae Lipumba anatafuta umaarufu kupitia Mengi
 
Katutokea wapi naye huyu saa hizi? Hajui hiyo ilikuwa kazi yake kama opposition leader? Mbona Mzee Slaa Alivyotoa List of shame yeye alibaki mdomo wazi ? Asituzuge sisi.

Tuna hasira na hao wanaotufanya maskini kwenye nchi yetu. Na Lipumba kama hajui tunamtegemea front line basi amshachelewa kuilijua . Bora ubaki huko nyuma nyuma katika mapambano haya forever. you may wish to greet your fans with that.
 
ahahaha..duu ..ebwanaeeee...

mbona mie naona lipumba anamatatizo ambayo hata yeye mwenyewe hajijui kuwa anayo...mengi HAKUNA ALICHOKOSEA...sana sana mengi anamsaidia raisi wetu aliyezidiwa nguvu na mafisadi ambao ndio walimuweka ikulu na ameshindwa kuwatoa.

wamefikia hatua ya kuingia chumbani kwake na kulala kitandani pake ilihali yeye analala chini..ITS A SHAME kwa raisi wetu kushindwa kuwaambia washkaji zake kuwa WIZI WENU BASI..mpaka anatokea NYERERE WA PILI..ndg MENGI ..kukemea uchafu huo.

kama mengi kakosea basi lipumba amepatia kuingia upande wa pili wa shilingi ambao ni wa MAFISADI...then halitakii mema taifa letu na hatumuhitaji rais wa aina yake (lipumba)
KWA kasi hii ya mengi kuiweka nchi mbele ... anastahili pongezi na heshima ya kipekee..naomba nimwite 2ND FATHER OF OUR NATION.....hatuhitaji mbwa asiyebweka..au paka asiyekamata panya...na mbwa wako asipobweka unatakiwa..UBWEKE WEWE ULIYEMFUGA...

raisi wetu kwa kutokubweka tunatakiwa tubweke sisi tuliomfuga (mpigia kura kuingia ikulu)....ITS A TIME FOR SOME SERIOUS ACTIONS....tumtoe na kumtimua mbwa asiyebweka, au tuwatimue paka na pamaya wote kwa pamoja...STREET JUSTICE WORKS BETTER HERE...ni maoni tuuu..we dare to talk openly
 
Hongera mzee Mengi!!!!
Mzee ka-prove kuwa ni miongoni mwa watu wenye uchungu na nchi hii na hekima katika fikra zao.

ikumbukwe kuwa siku mengi alipotoka mahakamani kushitakiana na manji, kesi ambayo manji aliifuta, siku hiyo mengi hakujulishwa lolote kabla na walipokuwa mahakama Manji hakutokea ila mawakili wake.jambo lile lilimuuzi mengi kwamaba mshitaki wake anaendelea na shughuli na yeye kusumbuliwa kwenda mahakamani ilhali isingelazimu kwake kwenda siku hiyo.Mengi akauliza 'Hivi watanzania wataendelea kudharauriwa hadi lini? Ni nana anayempa kiburi hiki cha dharau? kwanini tunawaandaa watoto wetu kudharauliwa kwa sababu ya pesa?"

Hekima inavyosema, kama unagundua baba ameshirikiana na ndugu zako na majirani kuihujumu mali ya familia.wew unaswa kumshambulia kwa kauli zenye ukweli ndugu yako na jirani mbele ya baba yako kuwa wao ndiyo kiini cha tatizo huku ukisema wao ni kikwazo cha baba.

Baba akiwa na akili hatajenge chuki kubwa kwako kwasababu hujamdhalilisha mbele ya wengine. Lakini ukweli kaupata.dozi ileile iliyomfikia ndugu yako na jirani ndiyo imempata na yeye.

Mengi kapiga kwa staili hiyo hiyo.

watajipanga wenyewe:
1. Sophia Simba
2. Ibrahimu Lipumba
3. ...................
4. ................... endeleza list

Sophia Simba anasahau watu wanajua fedha alizomwaga kwenye kampeni ya kugombea uenyekiti wa UWT zilitoka wapi na wageni waliokuwa wanafika kwenye nyumba yake ya Gezaulole ni wakina nani.

Lipumba mwanasiasa asiye na jipya wa kuanzisha jambo mwenyewe, bingwa wa kudandia hoja,mbinafsi, mwenye uchu wa madaraka katika ambalo hakuna analolifanya. Mwoga.
Wenzake[viongozi wa kisiasa] walipoanza kuwashambulia mafisadi ya kakaa kando sasa anawapiga vita wazalendo wenye kuwataja waziwazi.
Huyu naya nafikiri kavuta ndiyo maana anataka kubadili mwelekeo wa hoja.

Bravo Slaa, bravo Mengi
 
Hayati Baba wa Taifa wakati fulani alisema .....Tunahitaji Rais ambaye atathubutu kuwaambia marafiki zake tena wa karibu pale wanapotenda kinyume kwamba hapa mmekosea, awe na uwezo wa kuwakemea...Sasa JK hilo halipo kwake. Nguvu za mamba ziko mkiani, na nguvu za RA zipo kwa JK na viongozi wote wa serikali waliopata nafasi hizo kwa mgongo wa RA. MENGI endelea tupo nyuma yako tumeshika vijinga vya moto.
 
Shutuma za Lipumba kwangu mimi naona hazina msingi zaidi ya yeye kujitafutia umaarufu kupitia mafisadi na vyombo vya habari wanavyomiliki!

Kudai Mengi anachochoe ubaguzi wa rangi, haina mantiki yoyote,mafisadi papa anaowafahamu Mengi ndo hao aliowataja, sasa asiwataje eti kwa sababu wote ni wahindi? Serikali kama inadhamira ya kweli kupambana na ufisadi, ingeanzia hapo kuwafuatilia vizuri na wao walitarajiwa kuipa ushirikiano ili kuijiridhisha kuwa wao si mafisadi papa, kinyume cha hapo Lipumbe hana mpya.

Nilichotegemea kutoka kwa Lipumba baada ya Mengi kutaja mapapa, yeye kumchallenge kwa kutaja MAFISADI PAPA WAKIBONGO(WEUSI) sasa yeye kacritisize tu bila hata kutaja jina moja la mswahili fisadi....wakati yeye kwa nafasi yake alitegemewa awataja hata wale watano ktk 10 fisadis, yeye anakuja kuongelea mambo ya kibaguzi etc........utadhani na yeye ni CCM vile (angalau) ...very tired na viongozi wetu!

Kuhusu kumsifia JK, anaukweli fulani hapo, lakini kwa mtu mwenye akili timamu, Mengi is like alimtaja indirectly kama ni Fisadi No.1....ukichukulia the fact kwamba RA anadiwa kufadhili mbio zake za kwenda ikulu 05....sasa kama kaingizwa ikulu na mafisadi, yeye mwenyewe si msafi ni fisadi pia, kama watu wanafanya ufisadi na yeye yuko kimya.....yeye si kiongozi bora, ni mchafu....hili anatakiwa alijue! On another hand, kama kweli ana dhamira ya kupigana na ufisadi atachukua hatua kali dhidi ya hao the big 5!

Nilitegemea Lipumba kuongeza nguvu zaidi kwa kuleta orodha nyingine ya mafisadi badala ya kutumia muda mwingi kuponda mwananchi aliyetoa list ya mafisadi, hivyo kudhorotesha zaidi nguvu za wapambanaji!

Lipumba anapaswa ajiulize, Yeye amefanya nini cha pekee katika vita dhidi ya Ufisadi kama Kiongozi wa chama cha upinzani na kama Mtanzania mwenye uchungu na nchi hii?
 
Katutokea wapi naye huyu saa hizi? Hajui hiyo ilikuwa kazi yake kama opposition leader? Mbona Mzee Slaa Alivyotoa List of shame yeye alibaki mdomo wazi ? Asituzuge sisi.

Tuna hasira na hao wanaotufanya maskini kwenye nchi yetu. Na Lipumba kama hajui tunamtegemea front line basi amshachelewa kuilijua . Bora ubaki huko nyuma nyuma katika mapambano haya forever. you may wish to greet your fans with that.

Mkuu Mf., Lipumba si wakuwekewa tumaini wala kutegemewa. katika CUF unaweza zungumzia Duni na Maalimu. huyu ananini? Ni bora aendelee kukaa kwenye tafakari za uchumi.

To prove kuwa hafai kuwa frontliners, tafuta jambo alilolisimamia kidete lenye manufaa kwa UMMA hata MOJA kama mpiganaji wa uhakika ikiwa utalipata.
 
Lipumba hana jipya kwani yeye kazi yake kutumiwa tu na Seif; Kiongozi gani makini hana hata mbunge mmoja toka kwao bara na ndio maana wapemba wanamfanya ***** wao "mzigo mzito mpe mnyamwezi".!!! Hakuna FISADI PAPA mswahili sasa ndio iwe sababu ya kutowataja mafisadi papa wahindi kuogopa kuitwa mbaguzi?
 
sijaona kosa la LIPUMBA mimi..from the best of my knowledge, a mistake is taken into record if committed by someone who is CAPABLE OF DOING THE SAME....nafuatilia siasa za BONGO tangu miaka ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi..ajitokeze mtu anikumbushe LIPUMBA kaongeza nini cha maana kwa WATANZANIA,na pia kwa USOMI wake kama 'MCHUMI ALIYEBOBEA' ametoa mchango gani hata wa kuamsha UMMA juu ya matatizo MAKUBWA yanayoendelea katika nchi yetu..KUNA MTU AMEFIKA NYUMBANI (kijijini) ANAPOTOKA LIPUMBA? haihitaji ushahidi wa ziada kwa nyinyi wadau kufahamu kwamba LIPUMBA is just another LI-PUMBA in TANZANIA,hana mchango wowote wa ziada,ni aina ya wanasiasa uchwara walioingia kwenye siasa UKUBWANI kwa SHAUKU na si MIKAKATI..he is a good chap in HATE-POLITICS (AM TEMPTED TO LABEL HIM A RELIGIOUS FUNDAMENTALIST).USHAURI WANGU KWAKE NI RAHISI SANA,2010 ATULIE, AJARIBU KUGOMBEA UBUNGE NYUMBANI KWAKE, AKAPAMBANE BUNGENI SO THAT WE MAY PROVE IF AT ALL HE IS WORTH ANYTHING...ndugu zangu CUF wanatakiwa wawe makini na huyu mheshimiwa, otherwise their diminishing chances of reviving dwindling popularity in the MAINLAND shall never be realized...

KWA MAMA YANGU SOPHIA SIMBA.....
"POLITICS IS A DIRTY, VERY DIRTY GAME...FROM WHAT I CAN SEE IN YOU, YOUR NOT ENTITLED TO EAT EVEN WITH THEIR HOUSEGIRL...namaanisha, if at all wanakutumia, amini kwamba hawana COMMON GOAL na wewe, utadondoshwa njiani"

MY HONOURABLE PRESIDENT:
"LET ME TELL YOU ONE THING; EVEN THE LAYMEN, OR TERM THEM SOLID MAJORITY, KNOW WHO IS WITH YOU AND WHO'S NOT WITH YOU IN YOUR VERY OWN CABINET...2010 SIO MBALI, UKIMYA NA UPOLE WAKO UNATUTIA MASHAKA MAZITO SANA WHEN CONSIDERING THE FATE OF OUR BELOVED MOTHERLAND...HIVI TUPO PAMOJA KWELI!??..."

am out....
 
Mhh.. Majina Mengine bwana ebu angalia hapa

Lipumba= Na usomi wake wote kaja na pumba tupu

Ghasia = Ghasia zake hadi masikio yamechoka zisikia
Mengi =Kwa hili kaleta mengi, hadi tunaweza kuchora mstari yupi yuko upande gani
Slaa = Slaa zake wote tuna zishuhudia hadi keko imepata wasio tarajiwa kuwko, na
bado itaendelea kupokea

Endelezeni, it sound like a joke but it makes sense somehow!
 
Mwambieni Mengi ataje wale wengine watano alafu tutamuunga mkono kweli kwa sababu watamtesa sana.
 
sijaona kosa la LIPUMBA mimi..from the best of my knowledge, a mistake is taken into record if committed by someone who is CAPABLE OF DOING THE SAME....nafuatilia siasa za BONGO tangu miaka ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi..ajitokeze mtu anikumbushe LIPUMBA kaongeza nini cha maana kwa WATANZANIA,na pia kwa USOMI wake kama 'MCHUMI ALIYEBOBEA' ametoa mchango gani hata wa kuamsha UMMA juu ya matatizo MAKUBWA yanayoendelea katika nchi yetu..KUNA MTU AMEFIKA NYUMBANI (kijijini) ANAPOTOKA LIPUMBA? haihitaji ushahidi wa ziada kwa nyinyi wadau kufahamu kwamba LIPUMBA is just another LI-PUMBA in TANZANIA,hana mchango wowote wa ziada,ni aina ya wanasiasa uchwara walioingia kwenye siasa UKUBWANI kwa SHAUKU na si MIKAKATI..he is a good chap in HATE-POLITICS (AM TEMPTED TO LABEL HIM A RELIGIOUS FUNDAMENTALIST).USHAURI WANGU KWAKE NI RAHISI SANA,2010 ATULIE, AJARIBU KUGOMBEA UBUNGE NYUMBANI KWAKE, AKAPAMBANE BUNGENI SO THAT WE MAY PROVE IF AT ALL HE IS WORTH ANYTHING...ndugu zangu CUF wanatakiwa wawe makini na huyu mheshimiwa, otherwise their diminishing chances of reviving dwindling popularity in the MAINLAND shall never be realized...

KWA MAMA YANGU SOPHIA SIMBA.....
"POLITICS IS A DIRTY, VERY DIRTY GAME...FROM WHAT I CAN SEE IN YOU, YOUR NOT ENTITLED TO EAT EVEN WITH THEIR HOUSEGIRL...namaanisha, if at all wanakutumia, amini kwamba hawana COMMON GOAL na wewe, utadondoshwa njiani"

MY HONOURABLE PRESIDENT:
"LET ME TELL YOU ONE THING; EVEN THE LAYMEN, OR TERM THEM SOLID MAJORITY, KNOW WHO IS WITH YOU AND WHO'S NOT WITH YOU IN YOUR VERY OWN CABINET...2010 SIO MBALI, UKIMYA NA UPOLE WAKO UNATUTIA MASHAKA MAZITO SANA WHEN CONSIDERING THE FATE OF OUR BELOVED MOTHERLAND...HIVI TUPO PAMOJA KWELI!??..."

am out....

Mdau,

Ahsante sana kwa mchango wako. Lakini bado nina swali ambalo sijapata mtu wa kunisaidia. Je, ni kweli kwamba Lipumba ni kijana wa usalama wa Taifa?
 
Back
Top Bottom