Mwitikio wa kutisha mgombea wa CHADEMA alipotangaza nia Arumeru Mashariki

Ndg wana JF, tar11/02/2012 siku ya jumamosi nilifanikiwa kuhudhuria hafla fupi pale Kibo P
alace Hotel Arusha, wakati Kijana Machachari wa Chadema Arumeru Mashariki Kamanda na mpambanaji Joshua Nassary alipotangaza nia yake ya kuomba kuteuliwa na Chama chake cha Chadema aweze kupeperusha bendera ya chama hicho ktk kinyang`anyiro cha uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni hapo.
Mwitikio niliouona umenifanya nishawishike kushiriki nanyi kilichojiri,
1. Idadi ya watu waliojitokeza kumuunga mkono ilikuwa ni nyingi mno tofauti na matarajio ya wengi, kinababa kinamama bila kujali itikadi zao za chama,vijana wa kiume na kike walijitokeza kwa wingi kumuunga mkono, watumishi mbalimbali wa serikali walijitoa kwa hali na mali na kuahidi kuwa naye bega kwa bega hadi wahakikishe wanaupata ukombozi kamili,
2. Michango ya papo kwa hapo ilifanyika na ndani ya dakika chache zikapatikana kianzio cha zaidi ya Tsh 11,000,000/= Milioni kumi na moja ikiwa ni cash na ahadi, Magari nane yenye uwezo wa kwenda sehemu korofi pamoja na mafuta yake kwa wakati wote wa kampeni yalipatikana kama kianzio , Vyombo vya Kupazia sauti vya uhakika kwa muda wote wa kampeni, watu mbalimbali walijitolea nyumba na vyakula sehemu tofauti tofauti, pia walijitolea vijana wa kike na kiume, wababa na wamama kwenda kuweka kambi vijijini kwa muda wote wa kampeni hadi wakati wa kumalizika uchaguzi na kutangazwa matokeo. hii imeonyesha ni jinsi gani watu wanamkubali huyu kujana na ni wazi watu wameichoka CCM hata vijijini.[/QUOTE

Kweli CCM imechokwa lakini sasa mtupe takwimu za nyuma hapo Arumeru uchaguzi wa 2010 CDM ilipata kura ngapi? Maake nasikia marehemu hakufanya kampeni lakini alishinda.Tupeni takwimu isije ikawa yale yale ya uzini.
 
Kuna chombo kingine kitaingia kwenye kinyanganyiro hivi punde kupitia ChaDema kama sijakosea! Ni mama mmoja anaitwa Anna mtamsikia muda si mrefu ni mama mpiganaji pia na uzoefu makini!
 
mpaka kufikia march this year ntakua ARUMERU TAYARI KUWASILISHA MCHANGO WANGU AMBAO SIPENDI KUUWEKA WAZI HAPA COZ MAGAMBA WANAWEZA KUNICHAKACHUA...NIKAMA ULEEEHHH NLOMPA WENJE NA KUMNPINDUA MASHA...4SURE ARUMERU NI MALI YETU CDM NA NTATOA USHUHUDA APA SK YA MATOKEO,,,,LV CDM SO MUCH
 
Duble Chris,
Kwanza unatakiwa hujue kuwa JF sio mali ya Chadema..

Vile vile haiwezekani members wote wa JF wawe Pro-Chadema, lazima mkubaliane na fikra tofauti kwa hiyo mambo ya blog sio muhimu nadhani JF inatosha.
mkuu ninachoongelea mimi ni wazi hujanielewa ni kweli kabisa JF si ya CHADEMA na JF haina chama hapa zinaletwa mbalimbali kutoka vyama vyote Sasa. mlichopaswa kukifanya hapa wewe na genge lako ni kuleta hoja ZURI, BORA za chama hapa ilizijadiliwe kwa ufasaha

Ndiyo maana nikasema Nape alikuwa analeta hoja/taarifa za chama hapa vizuri tu nanyi mwaweza fanya hivyo kwa kuzileta hata za kutoka ofisi ya wilaya/mkoa vile hamleti zenu na mnakazana kuponda tu wenzenu chama chenu mnakiua wenyewe na siyo Chadema

mfano mngeleta ya mkutano wa DODOMA mkaupamba na kusimamia hoja mngeonekana wa maana sana
 
sisiem wakichukua arumeru narudisha kadi ya uanachama ya cdm

Mkuu wangu kwa kuangalia kwa umakini uchaguzi utakua mgumu kwasababu idadi kubwa ya vijana ambao ni wapiga kura wa CDM hawataweza kupiga kura kwasababu hawako ktk daftari la kudumu la wapiga kura. Na CCM kwa kutambua kwamba wamepoteza mvuto kwa vijana,serikali imesitisha zoezi la kuandikisha wapiga kura wapya kwa kisingizio cha ukosefu wa pesa. Vijana watakao athiriwa ni pamoja na wanavyuo,wanafunzi wa sekondari,wafanyakazi na wafanyabiashara waliohamia baada ya uchaguzi wa 2010. Hii ni changamoto kwa Bavicha na vijana wote nchini. NEC ameondoka Makame na Kiravu wameingizwa makada wengine akina Lubuva. Hakuna mabadiliko yoyote chanya yataonekana.
 
napenda sana kusikia mambo aya,pia nina imani kuwa mgombea wa chadema aliyepambana na mh.shomari,RIP...anaweza kuleta raha endapo atateuliwa na cdm,pia ntafurahi sana endapo kampeni na uchaguzi wa arumeru utakuwa wa amani,pia huru na haki.
 
Mimi nazidi kuwashauri Chadema, Tambo na majigambo sio mazuri kwani huo ni uchaguzi na siku zote una pande mbili kushinda na kushindwa.

sasa jipimeni msije pata aibu na fedheha kama ile ya Uzini.
 
napenda sana kusikia mambo aya,pia nina imani kuwa mgombea wa chadema aliyepambana na mh.shomari,RIP...anaweza kuleta raha endapo atateuliwa na cdm,pia ntafurahi sana endapo kampeni na uchaguzi wa arumeru utakuwa wa amani,pia huru na haki.

Katangaza kuchukua form ya kugombea leo
 
Back
Top Bottom