Mwitikio wa kutisha mgombea wa CHADEMA alipotangaza nia Arumeru Mashariki

Ndg wana JF, tar11/02/2012 siku ya jumamosi nilifanikiwa kuhudhuria hafla fupi pale Kibo Palace Hotel Arusha, wakati Kijana Machachari wa Chadema Arumeru Mashariki Kamanda na mpambanaji Joshua Nassary alipotangaza nia yake ya kuomba kuteuliwa na Chama chake cha Chadema aweze kupeperusha bendera ya chama hicho ktk kinyang`anyiro cha uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni hapo.
Mwitikio niliouona umenifanya nishawishike kushiriki nanyi kilichojiri,
1. Idadi ya watu waliojitokeza kumuunga mkono ilikuwa ni nyingi mno tofauti na matarajio ya wengi, kinababa kinamama bila kujali itikadi zao za chama,vijana wa kiume na kike walijitokeza kwa wingi kumuunga mkono, watumishi mbalimbali wa serikali walijitoa kwa hali na mali na kuahidi kuwa naye bega kwa bega hadi wahakikishe wanaupata ukombozi kamili,
2. Michango ya papo kwa hapo ilifanyika na ndani ya dakika chache zikapatikana kianzio cha zaidi ya Tsh 11,000,000/= Milioni kumi na moja ikiwa ni cash na ahadi, Magari nane yenye uwezo wa kwenda sehemu korofi pamoja na mafuta yake kwa wakati wote wa kampeni yalipatikana kama kianzio , Vyombo vya Kupazia sauti vya uhakika kwa muda wote wa kampeni, watu mbalimbali walijitolea nyumba na vyakula sehemu tofauti tofauti, pia walijitolea vijana wa kike na kiume, wababa na wamama kwenda kuweka kambi vijijini kwa muda wote wa kampeni hadi wakati wa kumalizika uchaguzi na kutangazwa matokeo. hii imeonyesha ni jinsi gani watu wanamkubali huyu kujana na ni wazi watu wameichoka CCM hata vijijini.

Ninapo ona taarifa hii napata picha ya namna wananchi wanao tafuta tiba ya maradhi'political,economical na social healing'.USE YOUR HEART WITH INTELIGENCE FOR INTELIGENCE SPRINGS YOUR LIFE VALUES.NGUVU YA UMMA.......
 
Duble Chris,
Kwanza unatakiwa hujue kuwa JF sio mali ya Chadema..

Vile vile haiwezekani members wote wa JF wawe Pro-Chadema, lazima mkubaliane na fikra tofauti kwa hiyo mambo ya blog sio muhimu nadhani JF inatosha.

Kwani inatakiwa msuli kujua hilo? JF is 4 great thinkers na great thinkerz wote wako CDM.
 
Mungu ibariki Chadema na wafuasi wake wote,nilitamani sana kijana huyu apite,na sasa yametimia. Tatizo moja ni kwamba wale wananchi wa kule wengi hawajafunguka,wanaiabudu sana SISIEM,sijui kama uchaguzi huu watafunguka.Nassary anasera nzuri sana na anaonyesha mtekelezaji na pia ni kijana,lazima utendaji wake utakuwa makini pia.
 
Natumaini kutakuwa na upinzani mkali zana kuqahi kutokea katika siasa za Bongo. Kila mmoja anausaka ushindi kwa udi na uvumba, itabidi nihamie Arusha kampeni zikianza kwa ajili ya kutoa updates.

PakaJimmy na kundi lako naomba ushirikiano hasa mtu anyeitwa Crashwise.



Karibu sana, karibu sana. Utalala nyumbani hapa Kaka.
 
Huyu kijana inaonekana ataiteka Arumeru kwa kishindo kikubwa sana. Sasa Dr wa ukweli na rais wa mioyoni mwetu WPS kuwa makini sana kuhakikisha taratibu za kidemokrasia zinafuatwa kumteua agombee, na aspirants wengine wasikilizwe ili Nassay akichaguliwa na chama asisababishe manung'uniko kama yanayotokea kwa jamaa wa maghamba kuanza kususiana na kuunda upinzani ndani ya chama. Kijana amenihamasisha sana...
 
Ritz ya chadema waachie pro-chadema. Wewe shughulikia ya *******. Wabunge wako wanalilia posho na baba mwanahawa kawawekea ngumu.
Mkuu unamaana ya Baba MwanaAsha yule aliyeibuka kidedea mkiani katika shule fulani!!
 
Natumaini kutakuwa na upinzani mkali zana kuqahi kutokea katika siasa za Bongo. Kila mmoja anausaka ushindi kwa udi na uvumba, itabidi nihamie Arusha kampeni zikianza kwa ajili ya kutoa updates.

PakaJimmy na kundi lako naomba ushirikiano hasa mtu anyeitwa Crashwise.

Tahadhari kwa CCM, nawasihi wasijaribu kufanya uhuni wowote wa kuchakachua matokeo wala kuiba kura,kumwaga pesa kununua watu au kufanya hujuma yeyote kwa hili jimbo maana wakifikiri wanatengeneza wanaweza wakawa wanajitafutia mauti yao wenyewe! CCM wakicheza rafu hapa wanaweza wakajikuta mapinduzi yasiyoisha yanaanzia hapa maana kama hawajawasoma Wameru ni kwamba wamechoka na ccm, halafu pia huwa wana asili ya kutotaka kudhalilishwa, ccm wanawezajikuta wanatengeneza mauti yao kuanzia Kaskazini. Wajue kuwa kati ya kabila lisiloogopa Polisi,Jeshi,FFU ni hili kabila, wakumbuke vizuri au wamuulize mrema aliwezaje kuizima vita ya Meru. Tumeamua ni wakati wa mabadiliko na tutasimamia kile tunachokiamini pasipo kununuliwa,kuibiwa wala kunyang`anywa. CCM kuweni makini mjapo Arumeru mjue huku siyo Zanzibar wala Igunga.
A%20S-danger.gif
A%20S-danger.gif
A%20S-danger.gif
DHULUMA HAITAKIWI ARUMERU MASHARIKI! Tutailinda haki na heshima yetu kwa namna yeyote.
 
Kuna Njia Ilitumika Igunga Kuiba Kura Igunga ambayo ni wachache Waliigundua ila mimi nimeipata kutoka Jikoni!! Waliweka Mabox Yenye Kura zilizochakachuliwa Chini ya Mlima!! Na walipofika Juu Dereva aliandaliwa kuzima Gari na Kusema Samahani Gari imezima Naomba Mshuke Msukume ili liweze Kuwaka!! Then Wote waliitikia na Kushuka na Kusukuma Gari!! Then Dereva akashtua na kuteremka hadi Bondeni!! Then wale mawakala wakaachwa Mbali Kidogo wakawa wanakuja kwa Miguu!! Wanafika mabox yameshabadilishwa na kuwekwa mengine Yaliyochakachuliwa!! Naandika Haya ili lisije Kujitokeza tena kwa Arumeru!! Hi ni njia ambayo ni hatari sana kuua Demokrasia!!
 
Back
Top Bottom