Uchaguzi 2020 Mwita Waitara na mwenzake watoa milioni 30 kwa viongozi UVCCM Tarime kuwasaidia kushinda kura za maoni, hali zao ni mbaya

MWENYEKITI UVCCM TARIME APEWA MILIONI 30 KUFANYA ZIARA KUMBEBA MWITA WAITARA NA GERALD MARTIN KUELEKEA KURA ZA MAONI TARIME MJINI NA VIJIJINI

Uongozi wa UVCCM Tarime umeamua kuchukua mkondo wa kuegemea kwa watia nia, na tayari wameunda timu yao wanayoiita chaguo la vijana kuelekea mchakato wa uteuzi wa wagombea Ubunge katika majimbo ya Tarime Mjini na Tarime Vijijini.

Ili kufanikisha nia yao wameanza ziara ya kuzunguka na kukagua uhai wa jumuia ya vijana, kuwa ni kuwaandaa kuelekea kura za maoni ndani ya chama. Ziara hiyo imezua sintofahamu kwa jinsi inavofanyika kwani haijalenga kukutana na wanachama wote wa UVCCM bali imelenga kukutana na wajumbe wanaoingia mkutano mkuu katika kura za maoni za kuchagua wagombea.

Vijana wengi wameshitukia tabia za Mwenyekiti UVCCM Tarime, Ndugu Godfrey Francis kuwatumia vijana hao au umoja huo ili kujipatia kipato, na fahamu ya kuwa Mwenyekiti huyo hana kazi ya kujiingizia kipato na amegeuka dalali wa watia nia ili walau apate kipato cha kuendesha familia yake, na hata gari anayoendesha kanunuliwa na watia nia, maana hana hata genge la kuchoma mahindi yeye, wala mke wake, kiufupi anategemea siasa ili kuendesha maisha yake.

Vijana wa UVCCM Tarime wameshitukia michezo ya huyo Mwenyekiti maana ni muda mrefu amekuwa akiitisha makongamano na kuomba pesa ili kuwawezesha vijana na zinaishia mfukoni mwake yeye, katibu wake, Katibu Hamasa, ambaye naye hana kazi ya kufanya naye anategemea siasa ili mkono uende kinywani.

Katika kundi kundi la UVCCM Tarime, mwanachama mwenye namba 0622348451 (Daniel Mkiriti) amehoji, namnukuu “Viongozi wa wilaya jumuiya ya vijana tunaomba mtuwekee ratiba ya ziara yenu ili kila kata ijiandae mbona mnaificha?, kushitukiza watu sio vizuri na sisi tuandae walengwa manake hamuwezi kuja kukaa na viongozi tu” mwisho wa kunukuu.

Katika ziara hiyo kuna mtu wa Mwita Waitara na wa Gerald Martin, ambao viongozi wa UVCCM Tarime wakishazungumza na hao wajumbe basi watu hao huwaita pembeni na kuwapa viongozi hao pesa kama kishawishi cha kumpigia kura Mwita Waitara na Gerald Martin.

Milioni 30 alizopewa Godfrey, ni kwa ajili ya kusaidia ziara hiyo katika kata zote za Wilaya ya Tarime, pia kwa ajili ya posho yake, Katibu wake Newton Mwongi na Katibu Hamasa, Pascal Mkapa. Na kila wakifika katika kata wawakilishi wa watia nia hao, huwapa posho za 30,000 kwa kila kiongozi ambaye anaingia mkutano wa wilaya/jimbo.

Hata hivyo, ziara hiyo imewagawa wanachama wa UVCCM kwanza kwa viongozi wao kuamua kubagua wagombea wengine na kuamua kuwa madalali, pili kwa viongozi hao kuitumia jumuiya hiyo kwa ajili ya kujinufaisha wao wenyewe. Na wengi wamedhamiria kutowaunga mkono wagombea hao ambao viongozi wao wamewabatiza kuwa ndio viongozi wa vijana.

Na nakishauri Chama kiangalie mienendo ya hawa viongozi wa UVCCM Tarime kwani wanatumika kukigawa chama kwa maslahi yao binafsi.

Ni mimi,

Venance Marwa

Mwanachama – UVCCM Tarime.
Hongera Mwita kwa Rushwa hiyo utapita mkuu
 
Hapo Takukuru wanasubiri maelekezo ya bwana mkubwa Wa magogoni.Asipotoa maneno nao kiimya...
 
Hahahha, unamjua huyu masikini mnafiki?
jamaa sio kabisa. kichwa buldozer akili kisoda. kuna prado moja huwa anaendesha basi ukikuta kaweka kishoka utasema kiongozi makini. ngoja aanze kuongea, ndio utajua ni kiazi mbatata. Fikiria kiongozi wa vijana anasema ameajiri vijana wa kwenda kuwakomoa mabaamedi wa chadema (nilishindwa kuelewa anawatambuaje kuwa hawa ni chadema na hawa ni ccm). Nikawaza, hii ina tija gani kichama? nikakosa majibu
 
Uewa mdogo kabisa
 
Bado sana hali za wagombea wa ccm zitakuwa mbaya sana kampeni zikianza. Inashangaza lakini inafurahisha kuona jinsi CCM wakihangaika wakati akina Mbowe na Lissu wakijiuguza, je watakapoanza kuzungumzwa sijui itakuwaje.
Suala la kujiuguza hata Mbowe lina muhusu ? Kwani ukipiga faru John na ikakuzidi unajiuguza ? Hongereni Chadema kwa maendeleo hayo ya Kichama.
 
Wakati wa kuwapiga Hela umewadia

Ova

Hata atoe pesa kiasi gani, Mwitra hashindi ubunge Tarime. Tunza maneno yangu, utaniambia mchakato ukiisha.

Huyu mpenda vyeo kafika stesheni ya mwisho, hana ujanja.

Mwenzake Kitila Mkumbo kashushuliwa na viongozi CCM. Akaulizwa unataka kugombea jimbo gani?- Jibu, Singida - lile la Waziri. Akafukuzwa na kuambiwa, rudi na ukachague Jimbo lenye mbunge mpinzani hili lina mwana CCM. Hatushindani CCM na CCM, bali CCM na Upinzani. Anahangaika Dar kutafuta Jimbo lenye Mpinzani. Kakalia kuti kavu!
 
Keshaliwa kichwa asubirie viti maalumu
 
Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom