Mwita Waitara: Huwezi kushindana na wakenya kwa bandari ya Dar es Salaam, option ni kwenda Bagamoyo

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
Mwita Waitara: Ukitaka kushindana na watu wa Mombasa, bandari ya Mombasa ni kubwa kwelikweli, unganisha zote hapa Tanzania hatuwafikii kwa ukubwa wa eneo hata mizigo inayotua pale.

Hata kama tumeongeza Mtwara bado hapa hatuwezi kutanua zaidi, tunataka tuweke utaratibu wa bandari ambao tutashindana na Mombasa

Ili ushindane na Mombasa na ujenge bandari ya kisasa ya mahitaji yote duniani, option the best ni kwenda Bagamoyo

Sasa habari ya nini kilifanyika, ni mambo gani yapo, hayo masharti ni ya kuzungumza ndio maana mheshimiwa Rais akasema tupitie lakini hakuna ambayo utafanya ushindane na Mombasa mizigo isiende pale kwasababu ya space yetu ya bandari ya Dar es Salaam

Huwezi kushindana na wakenya kwa bandari ya Dar es Salaam
 
Naona huyu Mwita ndio zamu yake kuongea kuhusu bandari ya Bagamoyo, waje na mkataba wa hiyo bandari kwanza kabla ya kuendelea na hizi kelele, na habari ya kusema hata mkataba wa SGR haufahamiki isiwe sababu ya kutooneshwa mkataba wa Bagamoyo, two wrongs can't make it right.
 
Aliyemuelewa huyu Mh anisaidie...
Je, bandari ni warehouse or godown la kuhifadhia mizigo?
Je, efficiency ya bandari inapimwa kwa holding space?
Je, diversification ie Tanga, Mtwara and DSM, is not better than concentration ie Mombasa?
What is the trend of waiting ships outside DSM port relative to Mombasa, due to small space for docking?

Politics will kill me!
 
Hivi kumbe bandari ya Bagamoyo inapigiwa upatu kwa lengo la kushindana na Kenya? Waitara bure kabisa.
 
Sasa kama suala ni sisi dhidi ya majirani na kadhalika kwanini tusijenge wenyewe, maana hapa inaonyesha mizigo ipo tatizo letu ni udogo wa hizo tulizonazo.
Naona hadithi inabadilika
 
Mbona hiyo Bagamoyo wameshindwa hata kuiweka kwenye Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka mitano uliozinduliwa hivi majuzi na Mhe, Rais?
 
Bandari ya Mtwara au Tanga ingeebdelezwa mbona inaweza kuwa maarufu kuliko Mombasa?
 
Kwani tunashindana kuhusu nini?
Tutachotakiwa ni kutengeneza uwezo wa kutosha kupokea mizigo inayohitajika kuingia kupititia bandali yeu na sio kushindana.
Kwani tunashindana ili iweje?
 
Mkuu ukiwaita vilaza umewaheshimu, hawa ni wapumbavu kabisa. Kwanini huo mradi usitekelezwe Tanga?
Wanatuona wote hatuna akili. Kumbe wengi wao hawajiwezi. Rarely they engage their minds in thinking. Bulldozing people to believe in some of these political projects, might backfire. Muda mwalimu mzuri....Kama IPTL ambavyo imeharibia watu sifa zao... 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Back
Top Bottom