Mwita Waitara athibitisha taarifa za kuumwa, amelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa, hajui ni ugonjwa gani

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,987
144,316
Taarifa zimesambaa kupitia mtandao wa Twitter kuwa Waitara amelazwa jijini Dodoma ambapo imedaiwa anaugua maradhi ya Corona.

Wacha tusubiri lakini hii ya kulazwa labda inaweza kuwa ni kweli, ila kuhusu aina ya ugonjwa, muda utathibitisha.

--- UPDATE---

waitara ed.jpg

Mheshimiwa Mwita Waitara amethibitisha taarifa zilizokuwa zikizunguka mtandaoni kuwa anaumwa, lakini amekanusha kuwa ni ugonjwa wa COVID-19.

Amesema hayo akihojiwa na East Africa Radio asubuhi hii. Mheshimiwa Waitara amenukuliwa akisema "Naumwa na nimelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, kusema naumwa nini sijui kwa sababu sijapata taarifa ya wataalam, kwahiyo aliyeandika mnaweza kumhoji anaweza akawaambia aliongea na mamlaka zipi, lakini mimi taarifa za Corona sina."

"Hali yangu haikuwa nzuri sana ila kuanzia jana nimeanza ku-improve, kabla ya hapo nilikuwa siwezi hata kuongea na simu, nipo Hospitali karibia wiki sasa, naumwa tu kawaida kwani tangu nimekuwa Naibu Waziri nimezunguka sana sijawahi kuchukua likizo"
 
Mambo CCM mnayofanyia wenzenu ndio maana mkipatwa na shida watu wanalipuka kwa furaha imagine sarakasi mlizomfanyia Lisu haya kama haitoshi mbunge mwenzenu Mbowe kapatwa na matatizo badala ya kutumia hata busara kidogo kumpa pole.

Maana ndio utu wema aliotuachia Nyerere nyie mnamdhihaki acheni wenzenu wafurahi mkipatwa na shida hata Mimi naona nisawa nawaunga mkono maana nyie CCM ndio mnashangilia shida za wenzenu.
 
Sasa haja gani kuleta mafumbo?,kama hujiamini bora uache kubreaknews za aina hii,maji ukiyavulia nguo huna budi kuoga,sio unafika bafuni unanawa uso na kutoka
 
Ili kupunguza maneno na vilimilimi vya watetezi wa CCM mitandaoni ni vyema uweke wazi jina la mtu anayeumwa na mahala alipolazwa hapo utakuwa umewaepuka wakorofi wa CCM, toa ufafanuzi wa kina inasaidia hata sisi wapinzani kwenda nao sambamba bampa to bampa
 
Ukitaka CCM wakae kimya kwa Aibu mtaje anayeumwa weka wazi kama ni mkuu wa wilaya au mkurugenzi au katibu Tawala watu wajue vizuri kazi ya kuwasakama CCM ifanyike kwa bidii zaidi
Hakuna mwanCcm anayeumwa usiku huu
 
Inamaana watu kuumwa na kufa imeanza mwaka 2020 kwamba hapo kabla magonjwa hayakuwepo tuache kucheza ngoma tusio ijuwa
 
Back
Top Bottom