Mwita Waitara athibitisha taarifa za kuumwa, amelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa, hajui ni ugonjwa gani

Amethibitisha

1592203436649.png
 
Siamini kabisa mwamba kama yeye kuumwa wkt mtetezi wa wanyonge anampa back up ya kutosha,anatembea kwny li v8,Jeshi la polisi linamtetea kwny kila hali..

Watu wa hivyo nilijua hua hawaumwi kabisa aisee.
Yeye ni gwiji wa kutukana na kupambana na chadema ,atumie hiyo hiyo nguvu ikiwezekana hata kwa msaada wa jeshi la polisi.
 
View attachment 1479030

Mheshimiwa Mwita Waitara amethibitisha taarifa zilizokuwa zikizunguka mtandaoni kuwa anaumwa, lakini amekanusha kuwa ni ugonjwa wa COVID-19.

Amesema hayo akihojiwa na East Africa Radio asubuhi hii. Mheshimiwa Waitara amenukuliwa akisema "Naumwa na nimelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, kusema naumwa nini sijui kwa sababu sijapata taarifa ya wataalam, kwahiyo aliyeandika mnaweza kumhoji anaweza akawaambia aliongea na mamlaka zipi, lakini mimi taarifa za Corona sina."

"Hali yangu haikuwa nzuri sana ila kuanzia jana nimeanza ku-improve, kabla ya hapo nilikuwa siwezi hata kuongea na simu, nipo Hospitali karibia wiki sasa, naumwa tu kawaida kwani tangu nimekuwa Naibu Waziri nimezunguka sana sijawahi kuchukua likizo"
Mungu wa mbinguni amfanyie wepesi apone haraka!
 
Umelazwa hospital wiki nzima halafu hujaambiwa Una umwa nn na wataalam , Kama sio uongo nn, wiki nzima bila majibu ni kwel hiki?
 
Funzo ninalolipata ni kuishi bila kukwaza watu. Kwa nini kuumwa kwa mtu iwe issue sana Kwani wanaumwa wangapi? Mtu mpaka unafikia kuombewa kifo si jambo zuri.
Mkuu Acha kujidanganya,hata uwe unaamka asubuhi na kwenda kugawa pesa kwa watu tambua kuwa wako watakaokuchukia na wapo watakao kupenda,ishi kwa kadiri uwezavyo na usiishi kwa kuigiza ili kuwafurahisha watu.

Mtu kuombewa kifo sio jambo la kusitaajabisha,usikute hata mtoto wako wa kumzaa akawa anakuombea ufe .

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom