Mwita Waitara athibitisha taarifa za kuumwa, amelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa, hajui ni ugonjwa gani

Aibu, kupenda kushabikia habari za uzushi zinazobandikwa twitter na mtu usiyemjua, maana kama habari ni ya kweli anapaswa kujitambulisha.

Kama kweli anaumwa wewe yakuhusu nini au ndio ushabiki wa kijuha na kitoto! Watu wazima hovyo!Umemjibu ipasavyo.
Ha haha, eti mtu usiye mjua? We kwani tunakujua? Mbona unataka tukuamini hapa?

Kigogo2014 hatumjui lakini tunamuamini maana anatoa hoja zake kwa vielelezo vya nyaraka zenu. Tofauti na nyie mnaobwabwaja kwa hisia tuu kuhusu Chadema na viongozi wake. Wizi wa viongozi wenu anashusha nyaraka zisizo shaka. Ufuska na matumizi ya madaraka kwa kupenda ngono anashusha nyaraka.

Mfano mambo ya Gekule na KM Bashiru utabisha nini? Anaomba mkopo 50 anapewa 70 kwa sharti la kichapo kwa raha zake! Tabia mnazianzisha za kushambulia watu tena mnatumia na chombo cha umma Bunge, yakiwarudia mnalialia.

Ebo, Mara buku!
 
Ufafanuzi wa hii taarifa ni muhimu zaidi ili isaidie namna ya kuwakabili watetezi wa CCM mitandaoni
Anaumwa Mwita Waitara, mbunge wa ukonga. Amelazwa Dodoma Gen hospital.

Tatizo la upumuaji
 
Taarifa zimesambaa kupitia mtandao wa Twitter kuwa Waitara amelazwa jijini Dodoma ambapo imedaiwa anaugua maradhi ya Corona.

Wacha tusubiri lakini hii ya kulazwa labda inaweza kuwa ni kweli, ila kuhusu aina ya ugonjwa, muda utathibitisha.
Ajabu nini? Nani huwa Haumwi? Unadhani corona ni ugonjwa wa zinaa? Ukue kijana
 
Wanasiasa ni wanadamu kama wengine nje ya siasa hutenda kama wanavyotenda wengine!

Kama ambavyo Mbowe alilewa na kuvunjika mguu ndivyo ambavyo Waitara anaweza kuugua ugonjwa wowote kama wanavyo ugua wanadamu wengine;

Nb:
siasa zisitutoe ufahamu kiasi hichi!
 
Hapo alipolazwa kuna ventilators kweli??... Incase ikihitajika, itapatikana kirahis?, tusije mpoteza mweshimiwa waziri
 
Hakuna aliyemdhihaki Mbowe, kosa la Mbowe ni kusema uongo kusingizia serikali. Angekaa kimya haya yote yasingetokea. Sasa ona alivyoumbuka.
Narudia Tena ndio maana Jamii inafurahi ccm mkipatwa na matatizo Sasa maana ya kuwa mkubwa ninini? Mkubwa ni jalala mlipaswa kutumia busara Kama mbowe aliisingizia serikali mlipaswa kumsahihisha kwa upendo staha na heshima sio Kama mlivyomfanyia kumkejeli kalewa kapigwa na kimada na maneno mengine ya dhihaka Yani nyie CCM ni wakubwa Ila hamna hekima.

Na ndio maana mnajiongezea maadui wengi kila uchao mnaligawa sana taifa hamjui tu hamna busara na laiti mngejua mnaipeleka nchi kubaya mngejirudi tunakoelekea tutakuwa Kama zanziba miaka ya nyuma hatutazikana kwenye misiba ya CCM walahi nawaambia mna unyama usiomfano lisu mlichomfanyia ni ushetani usio wa kawaida Yani mnaleta siasa mpaka kwenye uhai wawatu kwakweli patweni tu nashida mtajuana wenyewe hamna hekima the hatered you create deserves a resiprocated action.
 
FV0A1901-1.jpg


Mheshimiwa Mwita Waitara amethibitisha taarifa zilizokuwa zikizunguka mtandaoni kuwa anaumwa, lakini amekanusha kuwa ni ugonjwa wa COVID-19.

Amesema hayo akihojiwa na East Africa Radio asubuhi hii. Mheshimiwa Waitara amenukuliwa akisema "Naumwa na nimelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, kusema naumwa nini sijui kwa sababu sijapata taarifa ya wataalam, kwahiyo aliyeandika mnaweza kumhoji anaweza akawaambia aliongea na mamlaka zipi, lakini mimi taarifa za Corona sina."

"Hali yangu haikuwa nzuri sana ila kuanzia jana nimeanza ku-improve, kabla ya hapo nilikuwa siwezi hata kuongea na simu, nipo Hospitali karibia wiki sasa, naumwa tu kawaida kwani tangu nimekuwa Naibu Waziri nimezunguka sana sijawahi kuchukua likizo"
 
Back
Top Bottom