Elections 2015 Mwita Waitara aitingisha Ukonga wakati akirejesha fomu za kugombea Ubunge CHADEMA

Ilikuwa ni mtikisiko siku ya Alhamisi Jimboni Ukonga.Umati mkubwa wa watu ulimsindikiza Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kivule Mwita Mwikabe Waitara wakati akirejesha fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge jimboni Ukonga kupitia CHADEMA.

Ulikuwa ni msafara wa magari,bodaboda,baiskeli na watembea kwa miguu kutoka Kivule mpaka Gongolamboto kwenye ofisi ya jimbo.

Wananchi kadhaa wakihojiwa kwanini wanamuunga mkono Waitara kwa kiwango hicho walisema ni utumishi uliotukuka aliouonyesha tangu amechaguliwa kwa kura nyingi mwishoni mwa mwaka jana kuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Kivule.

Waitara amekomesha kabisa tabia ya waliokuwa viongozi wa serikali ya mtaa kutoza wananchi fedha wanapofika ofisini kwa matatizo mbalimbali.

Kwa muda mfupi aliokaa tayari amekuwa akiweka hadharani mapato na matumizi ya mtaa wa Kivule.Kwa Kivule Waitara ni zaidi ya Kiongozi.

Mara baada ya kukabidhi fomu huku Umati ukimshuhudia aliondoka kwa maandamano kuelekea Majohe ambapo alifanya mkutano mkubwa wa hadhara.

Mm namuunga mkono Waitara,na kura yangu tayari ni yake.
Pia namuomba amuonye mwenyekiti mwenzie wa Msongola,kwani pana malalamiko ya watu kutozwa fedha tena nyingi tu
 
wana ukonga mara zote mmeongozwa na wabunge legelege sana , sasa Mungu amewasikia amewaletea kamanda wa ukweli ndugu waitara .
 
Uthibitisho Mwita Mwikwabe alivomaliza UDSM alipewa ukatibu wa CCM Mkoa Tanga aligombana na Mkama baada ya kuungana na Nape kuhusu jengo la UV CCM
Akaambiwa arudi Lumumba aandalie mabosi chain ndo akatimkia Chadema
Mwita Mikwabe hakufanya chochote daruso zaid ya kufunga ndoa akiwa pres wa Daruso
 
Back
Top Bottom