Elections 2015 Mwita Waitara aitingisha Ukonga wakati akirejesha fomu za kugombea Ubunge CHADEMA

Greenwhich

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
1,337
968
Ilikuwa ni mtikisiko siku ya Alhamisi Jimboni Ukonga.Umati mkubwa wa watu ulimsindikiza Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kivule Mwita Mwikabe Waitara wakati akirejesha fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge jimboni Ukonga kupitia CHADEMA.

Ulikuwa ni msafara wa magari,bodaboda,baiskeli na watembea kwa miguu kutoka Kivule mpaka Gongolamboto kwenye ofisi ya jimbo.

Wananchi kadhaa wakihojiwa kwanini wanamuunga mkono Waitara kwa kiwango hicho walisema ni utumishi uliotukuka aliouonyesha tangu amechaguliwa kwa kura nyingi mwishoni mwa mwaka jana kuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Kivule.

Waitara amekomesha kabisa tabia ya waliokuwa viongozi wa serikali ya mtaa kutoza wananchi fedha wanapofika ofisini kwa matatizo mbalimbali.

Kwa muda mfupi aliokaa tayari amekuwa akiweka hadharani mapato na matumizi ya mtaa wa Kivule.Kwa Kivule Waitara ni zaidi ya Kiongozi.

Mara baada ya kukabidhi fomu huku Umati ukimshuhudia aliondoka kwa maandamano kuelekea Majohe ambapo alifanya mkutano mkubwa wa hadhara.
 
Nikiwa kama mkazi wa jimbo hili naamini Ukawa ina asilimia kubwa ya kulichukua. Kikubwa ni kutoa elimu ya uraia hususani maeneo ya chanika, ambayo bado yapo nyuma ukilinganisha na maeneo ya majohe, kitunda mpaka ukonga.

All the best Mwita ututetee Ukonga sio kama marehemu aliyepita hakuchangia lolote na alitutelekeza. Mwita jipange kuna huyu Jerry Silaa anajifanya leo ana uchungu na Ukonga wakati hajafanya lolote akiwa kama diwani.
 
Nikiwa kama mkazi wa jimbo hili naamini Ukawa ina asilimia kubwa ya kulichukua. Kikubwa ni kutoa elimu ya uraia hususani maeneo ya chanika, ambayo bado yapo nyuma ukilinganisha na maeneo ya majohe, kitunda mpaka ukonga. All the best Mwita ututetee Ukonga sio kama marehemu aliyepita hakuchangia lolote na alitutelekeza. Mwita jipange kuna huyu Jerry Silaa anajifanya leo ana uchungu na Ukonga wakati hajafanya lolote akiwa kama diwani.

Mkuu nilikuwepo siku ya tukio barabarani kushuhudia umati uliomsindikiza huyu mtu.Hakika Ukonga imeiva kwa mabadiliko.

Jerry Silaa hana chochote cha kujivunia kwani kama Meya wa Ilala angeweza kufanya mambo makubwa huku Ukonga ikiwa Manispaa ya Ilala anayoongoza Jerry.

WanaUkonga watasahau yote lakini kamwe hawawezi kusahau mateso wanayopata kipindi cha mvua kwa kutembea kwa miguu kwa kukosa barabara ya lami hata moja kwa jimbo zima.Huku Meya Jerry akijitapa kutokea Ukonga.Aibu kubwa kwake!
 
Jamaa alikuwa Rais wangu UDSM, na hivi sasa najivunia kuwa na mwenyekiti sehemu nayoishi, maana ile barabara ya kuanzia mazizini mpaka bomba mbili ilikuwa inatutesa sana, lakini nadhani sasa upele umepata mkunaji,
Wish you all the best Mwita, Naamini hata Thom Nyahende mko pamoja katika hili
 
Kamanda Mwita Waitara ana sifa zote na uwezo wa kuwa mgombea bora na wa uhakika wa Chadema/Ukawa katika Jimbo la Ukonga.

Wanasema aliye mwaminifu kwa jambo dogo atakabidhiwa kubwa zaidi.

Waitara kwa kipindi cha miezi 6 tu amefanya mabadiliko makubwa akiwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kivule.Hakika kura zaidi ya 1500 alizopatiwa mwaka jana hazikupotea bure.

Ada zote za manyanyaso kwenye Serikali ya Mtaa wa Kivule ni marufuku chini ya utawala wa Waitara.Wananchi wa Kivule wamemshuhudia Mwenyekiti wao akichimbua mitaro na mifereji mwenyewe bila kuringia cheo chake.
 
Jamaa alikuwa Rais wangu UDSM, na hivi sasa najivunia kuwa na mwenyekiti sehemu nayoishi, maana ile barabara ya kuanzia mazizini mpaka bomba mbili ilikuwa inatutesa sana, lakini nadhani sasa upele umepata mkunaji,
Wish you all the best Mwita, Naamini hata Thom Nyahende mko pamoja katika hili

Sifa kubwa ya Waitara ni kwamba haogopi madaraka ya mtu hata kama ni Rais wa nchi.

Anapokuwa anafuatilia maslahi ya watu wake hatishwi na yeyote.Kwa wale wote waliosoma na yeye UDSM watashuhudia haya alipokuwa Rais wao wa chuo.
 
Acheni sifa za uongo; Mwita Waitara alikuwa rais wa hovyo kupata kutokea Daruso, toka day one kaingia madarakani alikuwa busy kutafuta pesa tu kwa deal,kuangalua maslahi yake binafsi na akasahau kabisa utumishi kwa watu, kama ulikuwepo wakati huo utakuwa shahidi.
Akiwa na mwenzake Tweve, watu walioingia madarakani kama wapiganaji na walipofika madarakani wakaishia kuwa busy na ufisadi.

Watanzania wengi uwa hatupendi kueleza ubaya wa mwenzetu anapotafuta kitu lakin wengi hapa waliokuwa UDSM wakati huo wanajua jinsi alivyokuwa hovyo wakatu huo ila tunafunika kombe,ya kale yamepita.
 
Acheni sifa za uongo; Mwita Waitara alikuwa rais wa hovyo kupata kutokea Daruso, tika day one kaingia madarakani alikuwa busy kutafuta pesa tu,kuangalua maslahi yake binafsi na akasahau kabisa utumishi kwa watu kama ulikuwepo wakati huo utakuwa shahidi.

Watanzania wengi uwa hatupendi kueleza ubaya wa mwenzetu anapotafuta kitu lakin wengi hapa waliokuwa UDSM wakati huo wanajua jinsi alivyokuwa hovyo wakatu huo ila tunafunika kombe,ya kale yamepita.

Kwa uandishi wako hapa jamvini nina uhakika umefeli Form Four shule za Kata.

Kuzungumzia Chuo kikuu ni level kubwa sana kwako.Pole.
 
Masonjo tuwe wakweli jamaa alikuwa vizuri na aliiacha DARUSO ikiwa salama., Daruso ilikuja kuharibika alipoachiwa Magesa Mwita, ila Mwita Mwikabe alikuwa mzuri sana, na kwa kuongezea hivi sasa tuna Daraja pale Mazizini yote hii ni kutufanya wakazi wa kivule tu enjoy mazuri ya uongozi wake,
 
Ndugu zangu, kama nilivyosema Watanzania tuna tabia ya kusameheana.

Mr Suggestion, labda hukuwa unafuatilia utawala wa daruso wakati huo au ulikuwa ndio kwanza unaingia, waulize wenzio waliokuwa wakongwe kwako watakwambia, mie sizungumzie Magesa ambaye nae aliishia kuwa fisadi tu, nazungumzia Mwita Mwikwabe Waitara, aliyeingia madarakani kwa kusaidiwa na mpiganaji wa wakati huo Tweve.

Naamini waliokuwa UDSM wakati huo japo wanaweza kumsamehe ni mashahidi hapa, utawala wa mwita ulidissappoint sana watu maana watu walijua wameingiza wapiganaji kumbe wameingiza mafisadi na wezi, jamaa walikuwa busy kupiga deal na kula pesa tu, kila kitu kwao ilikuwa biashara.

Msifieni kwenye mengine ila mkitaka kumsifia kuhusu urais UDSM mtaharibu maana wengi wanaufahamu utawala wake pale.

Back
Top Bottom