johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,616
- 141,445
Naibu waziri wa Tamisemi anayeshughulikia miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari mwalimu Mwita Waitara amesema maana ya Elimu Bure ni wanafunzi kulipiwa ada na serikali.
Waitara amedai kuwa wananchi wengi wanachanganya mambo kwa kudhani kuwa ujenzi wa miundombinu ya elimu yakiwemo madarasa, maabara, madawati, vyoo nk ni sehemu ya mpango wa elimu bure na hivyo hawapaswi kuchangia.
Naye kada wa CCM ambaye ni afisa wa polisi mstaafu mzee Mwamakula amemshangaa waziri Waitara na kusema kwa hakika mawaziri wa awamu ya 5 hawana maoni kabisa.
Mzee Mwamakula amesema anashindwa kuelewa majukumu ya waziri wa Utawala Bora endapo hata swala la ujenzi wa madarasa ya watoti linakuwa na mjadala wa kitaifa wakati linaeleweka kabisa ni jukumu la nani.
Chanzo: Malumbano ya Hoja ITV