Mwisho wa utata wa Vazi la Taifa 2020 Tanzania huu hapa

FrankLutazamba

JF-Expert Member
Aug 9, 2018
449
408
Nimewaza na kuona ikiwa wizara ya utalii na utamaduni itapitisha basi ndiyo tutakuwa tumepata vazi LA taifa 2020, nitaomba ktk hafla niwepo na nitafurahi kumuona Mh. Rais Dr. Magufuli amevaa na waheshimiwa wengine. Tazama vazi hilo katika nembo ya taifa hapo chini.

ngao.png
 
Nimewaza na kuona ikiwa wizara ya utalii na utamaduni utapitisha basi ndiyo tutakuwa tumepata vazi LA taifa 2020,nitaomba ktk hafla niwepo,na nitafurahi kumuona mh.Rais Dr.Magufuli amevaa na waheshimiwa wengine.tazama vazi hill ktk nembo ya taifa hapo chini..View attachment 1505526
Kwa hio unataka wanume na wanawake wavae Magauni?tutembee kifua wazi pamoja na baridi.Sidhani kama hapa kunamchakato wa vazi la taifa.

Binafsi nafikir vazi la Taifa linapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

Aina ya Kitambaa,Uvaliwaje wake,Adaptation pamoja na material zingine zinahusiana na mavazi.

Ni lazima liwe tofauti lakini lisihame sana kutoka kwenye trending fashions.
 
Nimewaza na kuona ikiwa wizara ya utalii na utamaduni itapitisha basi ndiyo tutakuwa tumepata vazi LA taifa 2020,nitaomba ktk hafla niwepo,na nitafurahi kumuona mh.Rais Dr.Magufuli amevaa na waheshimiwa wengine.tazama vazi hilo ktk nembo ya taifa hapo chini..View attachment 1505526
Jambo ambalo serikali itapoteza mwelekeo ni kujaribu kutafuta kitu kinachoitwa "Vazi la Taifa". Kimsingi, vazi la taifa halitafutwi na halijawahi kutafutwa! Wamasai walitafutiwa na nani? Nchi ambazo huwa zinatolewa mfano; kama Ghana, Nigeria, Afrika Kusini au China hawajawahi kuwa na kamati ya kutafuta vazi. Kwanza si kweli kwamba wana mavazi ya taifa, hayo tunayodhani kuwa ni ya taifa ni mavazi yanayovaliwa na makabila makubwa. Nina wasiwasi kwamba tunatumia muda na fedha nyingi katika kitu kisicho na tija kwa maana kuwa mwisho wa yote vazi halitakuwepo.

Huwa sikubaliani na sababu zinatolewa eti 'vazi hili litazidisha uzalendo, litaleta maendeleo, litatangaza utamaduni, vivutio na utambulisho wa nchi'! Nijuavyo, vazi la taifa kama ni utamaduni basi utamaduni hauundiwi mezani kama tunavyotaka kuaminishwa. Nadhani tungezingatia katika kuibua mjadala zaidi kuangalia namna nzuri ya kurudisha maadili, uzalendo na kuutangaza utamaduni wetu katika kazi za sanaa na changamoto zinazotukabili juu ya namna ya kukuza au kudhibiti wimbi la mapokeo ya sanaa zinazokiuka mila, desturi na maadili yetu ya Ki-Tanzania, badala ya kufikiria kuwa vazi pekee litatusaidia. Hebu tujiulize ni nchi gani duniani ambayo kuendelea au kutokuendelea kwake kumetokana na kuwa ama kutokuwa na vazi la taifa? Je, ni kitu gani cha muhimu ambacho kama taifa tumekikosa kwa zaidi ya miaka 50 kwa sababu ya kutokuwa na kipande cha nguo kinachoitwa vazi la taifa? Ni kweli uzalendo umepungua nchini kwa sababu ya kukosa vazi la taifa? Je, vazi la taifa ni sawa na vazi la heshima ambalo ndicho kitu cha msingi sana kama tunaangalia udumishaji wa mila?

Nafikiri tuna changamoto nyingi ambazo hata tukileta hilo vazi haliwezi kuziondoa, tunapaswa kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kwenye jamii yetu ambao unaletwa na utamaduni tunaoiga toka nje, huku wizara inayoratibu mchakato wa kitambaa kinachoitwa cha taifa ikiwa kimya na haijawahi kuunda kamati kuushughulikia. Tunashuhudia mmomonyoko mkubwa katika jamii hii kupitia nyimbo za matusi, filamu zenye hadithi za kuiga zinazonakili vitendo na maudhui ya jamii za nje...
 
Kaka Bishop Hiluka umeongea madini ya hatari sioni cha kukosoa, kupunguza wala kuongeza. Ni kweli kabisa vazi la Taifa halitafutiwi mezani, umetoa mfano wa Wamasai ni kweli kabisa hawakutafutiwa na mtu ilo vazi hata wajapani na kimono (vazi lao la kitamaduni) na wahindi pia hawa wote hawakutafutiwa.

Utamaduni kwa kifupi ni mazoea ya kufanya kitu/jambo na kurudia jambo hilo mara kwa mara hivyo huwezi kukaa mezani na kusema kuanzia leo, huu utakuwa utamaduni wetu. Kuhusu vazi la taifa ni kuwa tuboreshe viwanda vyetu vya nguo (kama vipo) na pia tuwaunge mkono na kuwahamasisha wataaalamu wa mavazi ili waweze kubuni na kushona mavazi ya kupendeza na kukubalika miongoni mwa jamii yetu.

Ikiwa mavazi yatakayobuniwa na wabunifu wetu yatakubalika na kuzoeleka katika jamii yetu hayo sasa ndiyo yatakuwa mavazi ya Taifa. zaidi ya hapo ni kujilisha upepo.
 
Vazi la Taifa Ni Mgolole na sample Ni hiyo imevaliwa na huyo kijeba hapo juu mbona hili sio gumu
 
Kwa hio unataka wanume na wanawake wavae Magauni?tutembee kifua wazi pamoja na baridi.Sidhani kama hapa kunamchakato wa vazi la taifa.

Binafsi nafikir vazi la Taifa linapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

Aina ya Kitambaa,Uvaliwaje wake,Adaptation pamoja na material zingine zinahusiana na mavazi.

Ni lazima liwe tofauti lakini lisihame sana kutoka kwenye trending fashions.

Kwa wanawake naunga mkono sana na kila ikiwa imeshuka zaidi katika kifua ndio nzuri zaidi.
 
Nimewaza na kuona ikiwa wizara ya utalii na utamaduni itapitisha basi ndiyo tutakuwa tumepata vazi LA taifa 2020, nitaomba ktk hafla niwepo na nitafurahi kumuona Mh. Rais Dr. Magufuli amevaa na waheshimiwa wengine. Tazama vazi hilo katika nembo ya taifa hapo chini.

Mbona kwenye nembo, hicho kinyago cha mwanamke kinazidi tu kuwa kisichana?

Hivi hakuna mchoro rasmi, au kila mtu anatoka na wake ili mradi tu ni bibi na bwana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jambo ambalo serikali itapoteza mwelekeo ni kujaribu kutafuta kitu kinachoitwa "Vazi la Taifa". Kimsingi, vazi la taifa halitafutwi na halijawahi kutafutwa! Wamasai walitafutiwa na nani? Nchi ambazo huwa zinatolewa mfano; kama Ghana, Nigeria, Afrika Kusini au China hawajawahi kuwa na kamati ya kutafuta vazi. Kwanza si kweli kwamba wana mavazi ya taifa, hayo tunayodhani kuwa ni ya taifa ni mavazi yanayovaliwa na makabila makubwa. Nina wasiwasi kwamba tunatumia muda na fedha nyingi katika kitu kisicho na tija kwa maana kuwa mwisho wa yote vazi halitakuwepo.

Huwa sikubaliani na sababu zinatolewa eti 'vazi hili litazidisha uzalendo, litaleta maendeleo, litatangaza utamaduni, vivutio na utambulisho wa nchi'! Nijuavyo, vazi la taifa kama ni utamaduni basi utamaduni hauundiwi mezani kama tunavyotaka kuaminishwa. Nadhani tungezingatia katika kuibua mjadala zaidi kuangalia namna nzuri ya kurudisha maadili, uzalendo na kuutangaza utamaduni wetu katika kazi za sanaa na changamoto zinazotukabili juu ya namna ya kukuza au kudhibiti wimbi la mapokeo ya sanaa zinazokiuka mila, desturi na maadili yetu ya Ki-Tanzania, badala ya kufikiria kuwa vazi pekee litatusaidia. Hebu tujiulize ni nchi gani duniani ambayo kuendelea au kutokuendelea kwake kumetokana na kuwa ama kutokuwa na vazi la taifa? Je, ni kitu gani cha muhimu ambacho kama taifa tumekikosa kwa zaidi ya miaka 50 kwa sababu ya kutokuwa na kipande cha nguo kinachoitwa vazi la taifa? Ni kweli uzalendo umepungua nchini kwa sababu ya kukosa vazi la taifa? Je, vazi la taifa ni sawa na vazi la heshima ambalo ndicho kitu cha msingi sana kama tunaangalia udumishaji wa mila?

Nafikiri tuna changamoto nyingi ambazo hata tukileta hilo vazi haliwezi kuziondoa, tunapaswa kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kwenye jamii yetu ambao unaletwa na utamaduni tunaoiga toka nje, huku wizara inayoratibu mchakato wa kitambaa kinachoitwa cha taifa ikiwa kimya na haijawahi kuunda kamati kuushughulikia. Tunashuhudia mmomonyoko mkubwa katika jamii hii kupitia nyimbo za matusi, filamu zenye hadithi za kuiga zinazonakili vitendo na maudhui ya jamii za nje...
Mkuu heshima yako!

Uliyoyasema yana mantiki.

Minyimbo yenye maudhui ya matusi yamenifanya nichukie na kuacha kusikiliza bongo fleva kabisa.

Hivi wizara ya utamaduni sanaa na michezo, hakuna kifimbo cheza wa kurekebisha huu uozo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom