MWISHO wa UKAWA

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,409
0
Ukawa itasambaratishwa kwa kutumia pesa tu.

Ukitoa ngono, hakuna kitu tunacho kiabudu watanzania kama pesa haijalishi pesa ni halali au haramu.
Kwa kutambua hilo, CCM itatumia pesa kulitawanya genge hili la vijana na wazee. Kwa bahati mbaya
si vijana wote au wazee wote watapata hizo pesa bali ni wale wachache wenye nguvu kubwa ndani
ya genge hilo.

TUWAOMBEE UKAWA, washinde jaribu la pesa ili waokoe kizazi cha sasa na kijacho.
 
duanzi

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
16,446
0
UKAWA mbona imeshasambaratika siku nyingi baada ya mbowe na slaa kula pesa ya wafadhili
 
bato

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
3,506
2,000
Maalim Seif bado anazo nguvu za maamuzi kwa upande wa CUF Taifa? Mtu mwenye ushawishi na rahisi kurubuniwa kwa vipande vya fedha ni Mh Seif S. Hamad.Prof Lipumba hana tamaa,ila ana ushawishi mdogo CUF. Kwa CHADEMA alikuwa Mh ZZK,kwa sasa hana ubavu.
 
MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,938
2,000
Hakuna pesa itakayotumika kusambaratisha UKAWA. Hawa watasambaratishwa na tamaa zao za kugombea madaraka.
 
Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,288
2,000
Ndoto za mchana kama wameshindwa kuisambaratisha cdm na cuf wataweza vipi baada ya kuunganisha nguvu?
Waje na hizo pesa kama hawajafilisika na ukawa ikazidi kuimarika
 
Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,383
2,000
Ukawa itasambaratishwa kwa kutumia pesa tu.

Ukitoa ngono, hakuna kitu tunacho kiabudu watanzania kama pesa haijalishi pesa ni halali au haramu.
Kwa kutambua hilo, CCM itatumia pesa kulitawanya genge hili la vijana na wazee. Kwa bahati mbaya
si vijana wote au wazee wote watapata hizo pesa bali ni wale wachache wenye nguvu kubwa ndani
ya genge hilo.

TUWAOMBEE UKAWA, washinde jaribu la pesa ili waokoe kizazi cha sasa na kijacho.
Unakula ugali kwa mboga ya serikali saa tano usiku, kwanini usiote ndoto kama hizo. Halafu ukishaota ndoto unajiita nabii; kisha unatabiri nakuamini utabiri huu na kujaribu kutuaminisha. Yaani umeshasahau kuwa msingi ni ndoto iliyotokana na kula ugali kwa mboga ya serikali saa tano usiku. Kuwa makini ndugu!

Any way kukusaidia tu (maana najua umetuwa na Kinana na Nape) UKAWA ndo mambo yote kwa sasa, hata ufanyeje!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom