Mwisho wa mwaka huu, uwe ni mwanzo wa baraka kwetu

DAFU NA NDIMU

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
3,456
2,000
Habari wana JF wenzangu! Najua tunaendelea na maandalizi ya sikukuu vema kabisa.

Napenda kutoa wito kwenu ndugu zangu kuwa Tunapoelekea kusherehekea sikukuu hizi, tujiepusha na matendo mabaya/maovu(dhambi)

Matokeo ya dhambi ni laana kwa mtenda dhambi,kizazi chake(3&4), nchi yake, n.k. Tukijitenga na dhambi tutapata baraka na neema kutoka kwa Mungu, kuanzia kwa mtenda mema, kizazi chake(3&4) na nchi yake.

Mistari hii inaweza kutusaidia kufanya matendo yenye baraka na neema kwetu.

KUMB: 27:15-26
15.Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote waseme, Amina!
16. Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina
17. Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina!
18. Na alaaniwe ampotezae kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina!
19. Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina!
20. Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya baba yake. Na watu wote waseme,Amina!
21. Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina!
22. Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina!
23. Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina!
24. Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme, Amina!
25. Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumuua asiye na makosa. Na watu wote waseme, Amina!
26. Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina!

Kama nimekukwaza, nisamehe bure.

Nakutakieni sikukuu njema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom