Mwisho wa mwaka ATCL itazindua safari za kuelekea Uingereza; Je wanaotudai watakamata ndege zetu huko?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,983
20,631
Kwa hali ilivyo, miba imetegwa kila mahala, taarifa zilizopo ni kwamba ATCL watazindua safari kuelekea kwa Bibi(Uingereza) mwishoni kwa mwaka huu.

Wadeni wetu wametapakaa huko duniani na nyaraka za mahakama, na wametega miiba na misumari kila mahala, mali pekee inayovuka Boda ni ndege zetu za ATCL, pale Benki Kuu, hawawezi kufika kujichotea fedha wanazotudai.

Kilichobaki wanachotaka kugawana ni ndege zetu

Je wanasheria na wanausalama wamejipangaje kudhibiti hali hii? Wanafanya analysis za hali ya mambo au mpaka yatokee?

Kwa hali hii ni sasa na kufungua biashara karibu na nyuki waliochokozwa,muda wowote wanakugonga mwiba
 
Serikali inamadeni mengi sana, hata hawa wakandarasi wa barabara wasiolipwa wanaweza amua kukimbilia kuomba msaada wa kimahakama zikakatwa zote.
 
Ndege ni za ccm, bora zikamatwe zote zipigwe mnada itasaidia kupunguza madeni maana hapo zilipo zinazidi kuitia nchi hasara.
 
Back
Top Bottom