Dig the EA
JF-Expert Member
- Dec 7, 2017
- 277
- 270
- Thread starter
- #61
Na mimi sikumaanisha tunda la kati huko Eden, Mimi nilimaanisha kitendo cha kufanya ngono/mapenzi na baadaye mimba kutungwa kwa mwanamke na mtoto binadamu kuzaliwa duniani, hiki kitendo ndo kinaleta tafrani na shida kwa watu hao hao, bora kuacha tendo hilo ili namna nyingine ya dunia ije !
Shida watu huwa mnadhani tunda walilokula Adam na Eva ni ngono;
Tunda walilokula ni tunda halisi la mti uliokuwepo kwenye bustani ya Edeni.
Mungu aliwaagiza kuzaana mara tu ya kukamilisha uumbaji wa wote wawili, ina maana aliwaruhusu kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya kukamilisha uumbaji wao na SI KWAMBA walianza kufanya tendo la ndoa baada ya uasi wa sheria (kula tunda walilokatazwa na Mungu)
Msiwe hivyo jamani, tunda hilo katika maandiko siyo fumbo bali ni lugha Moja kwa moja na dhahiri kabisa.