Mwisho wa enzi za Babu Loliondo umefika, lakini makovu yamebaki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwisho wa enzi za Babu Loliondo umefika, lakini makovu yamebaki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ms Judith, Mar 7, 2012.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  [TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  Na Mwema Vedasto

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]IMANI ni fumbo kubwa ambalo limemzunguka mwanadamu tangu mwanzo wa historia yake. Watu wanatafuta majibu ya maswali yasiyoelezeka kisayansi, watu wanautazama ulimwengu jinsi ulivyo, watu wanataka kujua asili ya ulimwengu wanamoishi, asili yao wenyewe, na zaidi wanataka kujua mustakabali wao ni wapi. Baada ya maisha haya kuna nini? Imani inajaribu kujibu yote haya.


  Tunajua kwamba kila mtu anao uhuru wa kuamini. Na kila mtu anapaswa kuheshimu anachoamini mwenzie. Inakera sana kusikia kashfa dhidi ya imani za watu wengine. Tena ingefaa hatua kuchukuliwa haraka juu ya mihadhara ya kashfa na vituo vya upashanaji habari vinavyoeneza sumu ya kushambulia dini za watu wengine.


  Lakini pamoja na heshima itupasayo kwa imani za watu, na pamoja na ukweli kwamba imani ni fumbo ambalo halina majibu katika maabara ya kemia au fizikia, tuharakishe kuonya kuwa, imani sharti iende sambamba na fikra. Tukisema kwamba imani ni fumbo, kamwe hatumaanishi kuwa imani haielezeki ama hatupaswi kuhoji kuhusu imani.


  Imani bila fikra (reason) ni sawa na ndege mwenye ubawa mmoja. Kamwe hawezi kuruka, hata kama ubawa huo ungekuwa mkubwa sana.
  Ni hatari sana kukaa kimya bila kuhoji kuhusu mambo kadhaa yanayofanyika chini ya kivuli cha imani. Ni hatari kukaa kimya kwa sababu kuna imani potofu zinazomaliza watu.


  Hata kama tunaheshimu imani hizo, tunao wajibu wa kuhoji pale ambapo kuna upotofu wa waziwazi. Wakati wa biashara ya Loliondo, niliandika makala, “Dawa ya Loliondo: Fides et ratio”.


  Nilitaka tu kusema imani sharti iende sambamba na fikra, kwamba watu wahoji na watazame jambo katika ukweli, wajitahidi kupembua hisia zilizochanganyika na imani.


  Janga hilo la Loliondo liliendelea kwa muda, likaathiri watu wengi, na sababu ya msingi ni hii.


  Watu waliamini bila kufikiri. Watu walitazama kwamba huko Loliondo wameenda wanasiasa maarufu, wameenda viongozi wa dini, wameenda hata na watu wan chi za nje.


  Hisia hizo zikaitimishwa kuwa Babu wa Loliondo ana muujiza wa uponyaji kwa kila mmoja. Watu wakatumia akiba yote, wengine wakakopa, wakaenda Loliondo, na katika hisia za kufikirika, (illusion) baadhi ya waliokwenda huko wakatangaza kila mahali kuwa wamepona.


  Inaumiza sana kutangaza kuwa umepona ugonjwa sugu, kisha unajigundua kuwa kumbe hukupona kweli. Inaleta msongo, na utahangaika kutafuta uongo wa kuthibitisha kuwa umepona.


  Wapo ndugu zetu waliokwenda huko na wakatangaza kuwa walipona lakini kitambo kifupi tu kilitosha kuthibitisha kuwa si kweli.


  Baada ya maafa hayo ya Loliondo, hatimaye mwisho wa enzi za Ambilikile Mwasapila ulifika. Lakini makovu yamebaki. Yamebaki katika familia zilizopotelewa na wapendwa waliofia maporini na kuzikwa (wengine kutupwa) hukohuko, makovu yamebaki kwa walioacha kutumia dawa za maradhi yao kwa kuamini kuwa walikuwa wamepona, kumbe ugonjwa ukawa sugu zaidi baada ya kusitisha madawa, na ilipobidi kutumia dawa, ilibidi wazitumie kwa kiwango cha juu zaidi.


  Makovu mengine ni kwa wale waliotumia akiba yote ya familia, lakini mbaya zaidi wale waliokopa, na sasa wanapaswa kulipia mkopo uliokuwa na hasara tupu. Makovu ni mengi, hatuwezi kuyaandika yote hapa, mengine yameandikwa katika mioyo ya hao waliodanganywa katika huo “muujiza” wa uponyaji.


  Sasa janga la Loliondo limekwisha, kwa nini kuendelea kuliandika? Lazima tulitazame kusudi tusijikwae tena na kuingia tena katika imani uchwara za sampuli hii.


  Na nasikia mzee amesema anakuja na toleo jipya la muujiza. Lazima kulitazama, na ninaamini ilibidi lifanyiwe tathmini ya kisayansi na wataalamu, (kama mgomo wa madaktari unavyopaswa kufanyiwa tathmini), kusudi kujua namna tulivyopetuka katika ujinga, na sasa tutazame, tusirudi huko. Walau tuweze kujifariji kuwa kosa zaidi ni kurudia kosa.


  Lakini zaidi ni lazima kulitazama kwa sababu tuna “viloliondo” vingi vinaibuka kila uchao. Mtu kuibuka tu na kutangaza hadharani na kubuni vyombo vya utangazaji, kuajiri watangazaji wa habari, wakipiga mbiu kwamba katika nyumba fulani yupo mtu mwenye uwezo wa kuponya.
  Lakini hawa huenda mbele kumshinda Yule wa Loliondo, kuwa, muujiza wao sio wa kitabibu tu, bali hata Baraka juu fedha hufanyika, uchumi wa muumini utatengemaa. Yaani fedha ziongezeke bila uzalishaji! Na tunakwenda huko. Kumbukeni kilichotokea huko Pwani, kesi iko mahakamani.


  Tunawajibika kukemea imani zisizo na maelezo ya kutosheleza, kwa sababu tunaona mateso ya hao wanaohangaika, mara huku, mara kule, wakitafuta kuponywa, wakiacha dawa za hospitali, na baadaye wakikumbwa na msongo wa mawazo baada ya kugundua kuwa hawaponi.


  Hawa wapo, ninawafahamu. Wasingedanganywa, hata kama wasingepona hospitalini, wangekufa katika utulivu. Imani za aina hii ni janga.
  Kweli tunahitaji faraja katika machungu yetu. Lakini faraja ya kweli sio porojo, sio kumsubiri Mungu aje kutuletea kila kitu wakati alishaweka akili katika vichwa alivyotupa.


  Nimalizie kwa kusema kuwa naamini kuwa miujiza hutokea, ila siamini kuwa miujiza ni mtindo wa maisha. Miujiza ni nadra.


  [​IMG]

  mwemav@yahoo.com
  0712576562


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  chanzo: Mwisho wa enzi za Babu Loliondo umefika, lakini makovu yamebaki
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  viongozi wetu wa kitaifa ndio waliooasisi hili janga.

  ccm bwana?
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,045
  Likes Received: 6,486
  Trophy Points: 280
  asante malenga wetu.
   
 4. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  we kirukanjia ni mganga wa kienyeji aliyekosa wateja

  au ni mchungaji uchwara aliyekosa sadaka?


  umekua ukimsakama babu kwa muda mrefu sasa


  nini kinakukera juu ya babu?
   
 5. s

  sawabho JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Maisha ni mtihani, ushinde.
   
 6. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tatizo hawa jamaa wanaamini kila kitu!
   
 7. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Mkuu tofautisha IMANI na UJINGA!  ​WAJINGA NDIO WALIWAO!
   
 8. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135

  mpendwa,

  asante kwa kashfa zako. ila ukipata muda jaribu kutafakari hizo quotes hapo chini.

  ubarikiwe sana

  Glory to God!   
 9. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wapendwa,

  kwa kweli ule ulikuwa "UJINGA" tu na kamwe sio IMANI.

  samahani kwa niliowakwaza,

  Glory to God!
   
 10. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa,

  kwa hili tuko pamoja.

  kiongozi anapaswa kuonyesha njia na kuwa kioo cha jamii. inapofikia hatua ya kiongozi kuonyesha njia ya kwenda " KUPATA KIKOMBE CHA BABU LOLIONDO" ujue tanzania tuna viongozi wa aina yake!

  ubarikiwe sana

  glory to God!
   
 11. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Ms judith are u married??
   
 12. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Enzi za miujiza zilishapita karne nyingi!hivi sasa tupo enzi za utapeli kwa kwenda mbele.
   
 13. uronu

  uronu Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 5
  Tusomeni maandiko matakatifu,
  maana yote haya ni dalili za nyakati hiz mbaya na za kuogopa, ila Yesu kristo alisha tuonya mbele.
  Kwa walio wa kristo,
  soma kitabu cha matayo 24:1-51. Tusienende kama watu wamataifa, na tuishi kwa kumtumain MUNGU siku zote, maana watakuja wengi na kutudanganya....
  Yeremia 17 : 5 -11, asomae na afaham

  MBARIKIWE wasomaji
   
 14. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nafikiri hili halihusiki hapa,

  ubarikiwe mpendwa

  yeah, you have a very good point!

  wapendwa, tujihadharini sana na utapeli wa kisasa kupitia watu wanaojiita wachungaji, maaskofu nk.

  ubarikiwe sana

  ni kweli kabisa mpendwa,

  hizi ni nyakati za mwisho. kweli kabisa, ASOMAYE NA AFAHAMU!

  mbarikiwe sana wapendwa wote

  Glory to God!
   
Loading...