Mwisho mbaya wa aliyekuwa Rais wa Sierra, Leone Valentine Esegragbo Melvine Strasser

Valentine Strasser alikua rais a Sierra Leone kati ya mwaka 1992 hadi 1996.

Strasser alizaliwa mwaka 1967, April 26 mjini free town, alimaliza sekondari mwaka 1986 akiwa na miaka 18. Walimu wake wanasema alikua mzuri sana kwenye hesabu na kemia.

Strasser baada ya kumaliza elimu ya sekondari alijiunga na jeshi mwaka 1987, hadi mwaka 1992 alikua na cheo cha cadet officer jeshini.

Mwaka 1991 kundi la waasi la Revolutionary United Front likaanza mashambulizi dhidi ya serikali ya Sierra Leoni iliyokua inaongozwa na Rais Joseph Momoh.

Serikali ya Rais Momoh ilikua na hali mbaya sana kiuchumi, ilishindwa kulipa mishahara ya watumishi wa umma, wanajeshi, ikashindwa kuwapa wanajeshi viatu na kombati na mahitaji yote ya kijeshi ili kuwawezesha kupambana na waasi wa RUF.

Mashariki wa mji wa Free Town, mji mkuu wa Sierra Leoni kulikua na kambi ya kijeshi ambayo Strasser alikua amepangiwa kazi ya kuongoza wenzake kupambana na waasi wa RUF.

Mwaka 1992, April 29 baad ya vitisho vyote kwa serikali na mazungumzo yote na serikali kuwapa mahitaji muhimu wanajeshi kushindikana, Straaser akaongoza kikosi cha vijana wenzake wasiozidi 9 kutembea kwend Ikulu kumuona Rais Momoh ili asikilize shida zao na magumu wanayokutana nayo vitani.

Rais Momoh kuona wanajeshi wanatembe kwenda ikulu, akaikimbia ikulu, Strasser na wenzake wamefika ikulu rais amekimbia, Strasser akajitangaza kua rais na mkuu wa nchi akiwa na miaka 25 siku tatu tu tangu asherehekee siku yake ya kuzaliwa. Strasser akawa rais mdogo zaidi Duniani mwaka 1992.

Baada ya Strasser kushika madaraka kwa miezi 8 uchumi wa Sierra Leoni ukaimarika, watu wakashangilia utawala wa vijana, vijana Strasser na wenzake wakaja na mambo mapya.

December 1992 strasser akaanza kuvaa sura ya kidikiteta, mwezi huo huo akawaua hadharani katika fukwe ya bahari watu 29 aliowatuhumu wahaini, alipoulizwa na wanahabari ushahidi wa uhaini wao, alijibu, "https://jamii.app/JFUserGuide off man, In Texas they kill people everyday".

Strasser na vijana wenzake wakaanza kuishi maisha ya kifahari, magari ya kifahari, starehe na kuwashughikia wote waliowapinga, maisha wa wa Sierra Leoni yakazid kua magumu, wakarudi enzi za Rais Momoh.

Mwaka 1993 Strasser akahudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za madola nchini Cyprus, akaenda amevaa jinzi na Tisheti imeandikwa " sunny days in cyprus" na miwani mieusi.

Mwaka 1996 Strasser akatangaza uchaguzi na yeye akajiweka kati ya wagombea, hili likawaudhi watu hivyo kupeleke makamo wa rais wa Strasser bwana Maada Bio kumpindua Strasser. Mada Bio alikua na miaka 32.

Baada ya kupinduliwa Strasser akakimbilia Uingereza kusoma, akajiunga na chuo kikuu cha Warmick kusomea sheria, baada ya maandamano ya vyama vya kutetea haki za binadamu uingereza kupinga uwepo wake pale, Strasser akakosa ufadhili, akaacha chuo akaanza kunywa pombe.

Mwaka 2000 baada ya maisha kua magumu Uingereza, Strasser akakimbilia Gambia kwa mchizi wake Professor Doctor Alhaj Field Marshal Yahaya Jameh. Baad ya kukaa kwa muda Gambia akatuhumiwa kwa kosa la kutaka kumpindua Field Marsh Jameh, akatimuliwa Gambia.

Strasser baada ya kufukuzwa Gambia akakosa pa kwenda akarudi nyumbani kwa mama yake na kuishi kwenye nyumba aliojenga maa yake maana yeye hakuahi kujenga hata kibanda.

Hapo kwa mama yake nje Strasser amefungua kibanda anafundisha tuition ya computer kwa watoto wa mtaani.

Hayo ndio maisha ya Bwana Valentine Strasser ambae alipokua rais Siku ya Valentine ilikua sikukuu nchini Sierra Leoni.

Angalia picha zake.
wpid-captain-valentine-strasser-27-leader-of-the-provisional-ruling-council-b3r27y.jpg
wpid-img-20150705-wa0133.jpg
sub-buzz-14717-1475183239-3.jpg
wpid-img-20150706-wa0014.jpg
 
Mkuu pamoja na Africa kupita katika njia ngumu sana kuelekea demokrasia lakini pia katika njia hiyo tulipata viongozi kadhaa wazuri ambao hawakuingia madarakani kwa njia ya sanduku la kura. Ila kwa bahati mbaya sana viongozi hao hawakudumu madarakani pamoja na nia hao nzuri ya kuwafumikia wananchi wao. Waliondolewa na mabeberu ambao waliona mirija yao ndani ya bara la africa imezibwa. Viongozi hao ni kama Tom Sankara na huyu Valentine Stresser. Wengine waliingia madarakani wakiwa na nia njema ila wakaa madarakani kwa muda mrefu na kujisahau kabisa na kuanza kuwa miungu watu; hawa ni kama akina Col. Gaddafi, Master Sergeant Samwel Doe na sasa tunamuona huyu Yahya Jammeh. Mwisho wa hawa wa kundi la pili huwa mbaya sana. Bado tunasubiria mwisho wa Yahya Jammeh na akina Blaise Compaore.


We ni noma mkuu..
Ulimtabiria Jammeh
 
Mkuu wangu siwezi kumsahau Capt. Thomas Isidore Noel Sankara (RIP) aliyempindua Jean Baptiste Ouedraogo mwaka 1983 wakati huo Capt. Sankara akiwa na umri wa miaka 33. Hakuwa na miaka 25 mkuu. Alikuja kupinduliwa na rafiki yake aitwaye Blaise Compaore mwaka 1987. Mkuu simpendi Compaore na natamani niuone mwisho wake.
Mungu ni mkubwa kwani niliuona mwisho wa Compaore pale alipofukuzwa kama mwizi toka Ikulu aliyoikalia kwa miaka 27 baada ya kumpindua Sankara.
 
Mkuu pamoja na Africa kupita katika njia ngumu sana kuelekea demokrasia lakini pia katika njia hiyo tulipata viongozi kadhaa wazuri ambao hawakuingia madarakani kwa njia ya sanduku la kura. Ila kwa bahati mbaya sana viongozi hao hawakudumu madarakani pamoja na nia hao nzuri ya kuwafumikia wananchi wao. Waliondolewa na mabeberu ambao waliona mirija yao ndani ya bara la africa imezibwa. Viongozi hao ni kama Tom Sankara na huyu Valentine Stresser. Wengine waliingia madarakani wakiwa na nia njema ila wakaa madarakani kwa muda mrefu na kujisahau kabisa na kuanza kuwa miungu watu; hawa ni kama akina Col. Gaddafi, Master Sergeant Samwel Doe na sasa tunamuona huyu Yahya Jammeh. Mwisho wa hawa wa kundi la pili huwa mbaya sana. Bado tunasubiria mwisho wa Yahya Jammeh na akina Blaise Compaore.
Tabiri
 
Back
Top Bottom