Mwisho kulia kisa mapenzi ilikuwa lini?

Sollie

Senior Member
Aug 21, 2020
120
1,000
Mpaka namaliza form four nilikuwa sijawahi kuwa na mahusiano nilikuwa mdada mpole sana mwenye nidhamu na ambaye nafanya vizuri kwenye masomo, ishu za mahusiano sikuwahi kabisa hata kutest.

Baada ya kumaliza form form nilifaulu nikapangiwa shule ya Wasichana Ruvu. Nakumbuka nilipelekwa na Baba na mama stendi nikapandishwa gari la Dar ili nishuke kwa uncle wangu chalinze nilale kisha yeye angenipeleka shule.

Kwenye siti nilikaa na kaka mmoja mtanashati na kwa sababu nilikuwa nimevaa uniform alianza kunihoji pia alijitambulisha kuwa yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili UDSM, kiukweli yule kaka nilikuwa namuona kama profesa flani yani mtu kuwa chuo kikuu tena mwaka wa pili niliona kitu kikubwa sana.

Tulipiga stori na kunisihi sana nikasome kwa bidii kwani elimu ndo kila kitu, kwa sababu sikuwa na simu aliniandikia namba yake kwenye karatasi na kunitaka nikipata simu nimtafute, kuna mwalimu mzee alikuwa anatufindisha physics alikuwa ananipenda na kuniita mwanaye simu yake ilikuwa kama baba yangu tu nilisave namba ya yule mwanaudsm kwa simu ya ticha wangu kama Kaka Sollie, so mawasiliano yalikuwa yanaendelea vema kabisa kama kaka mtu.

Mpaka namaliza six tulikuwa kwenye mahusiano mazito sana kwa njia ya simu
Wazazi wake walinifahamu, wadogo zake, na kila mtu wake wa karibu, baada ya kumaliza mwaka wa tatu alifanya vizuri sana na kwa miaka ile aliachwa chuo kuwa Tutorial Assistant, mimi wakati huo nipo mwaka wa kwanza na mimi chuo ila si UDSM, baada ya hapo alipata Scholarship akaenda kusoma Masters Japan, na mawasiliano kwa njia ya Email yalikuwa kama kawaida wakati huo kulikuwa hakuna WhatsApp.

Aliporudi mawasiliano yalianza kufifia kumbe alipata mwanamke mwingine mtanzania huko Japan, siku hiyo nilimtafuta akapokea mdada akaniambia achana na mpenzi wangu la sivyo nitakufanya kitu kibaya.

Wapendwa nililia mimi, nakumbuka ilikuwa likizo nilikuwa naenda kushinda shambani nalala nalia karibu mwezi mzima, sikuwa naweza kula wala kufanya chochote, nililia nilibembeleza mwanaume lakini wapi, Toka hapo sikuwahi kulilia mapenzi kama nilivyolia wakati huo.

Kilikuwa kilio ambacho sijui hata sababu yake ilikuwa nini hatukuwahi kulala wote wala mapenzi yetu yalikuwa tu ya simu, kwenye simu tulipanga maisha yetu yote, nakumbuka nilikuwa naitwa Mama Lissa

Sasa hivi kaowa na ana familia yake ila sijawahi kumchukia tho hatujawahi kuonana tena.
 

Sollie

Senior Member
Aug 21, 2020
120
1,000
Pole sana, kwahiyo alimuoa huyo huyo? Je nawewe umeolewa

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
Hakumuowa huyo, huyo aliyenitishia mkwala alikuwa mtoto wa prof wa hapo UDSM wala hakumuowa ameowa mwaka juzi mtu mwingine kabisa.

Ila kabla ya kuowa alinitafuta akaniomba msamaha na kutaka kurudiana ila na mimi wakati huo nilikuwa kwenye mahusiano mengine very deep so nikamweleza akaelewa.
 

Ulweso

JF-Expert Member
May 24, 2016
17,729
2,000
Hakumuowa huyo, huyo aliyenitishia mkwala alikuwa mtoto wa prof wa hapo UDSM wala hakumuowa ameowa mwaka juzi mtu mwingine kabisa

Ila kabla ya kuowa alinitafuta akaniomba msamaha na kutaka kurudiana ila na mimi wakati huo nilikuwa kwenye mahusiano mengine very deep so nikamweleza akaelewa
Pole tena, huyo wa kufanya mkwala mbuzi kumbe naye alinyolewa, hongera kwa ujasiri wakati mwingine using'ang'anie riziki isio yako hongera sana.
 

B kal

Member
Nov 11, 2020
98
125
Ni baada ya kutambua kuwa mwenza sahihi lazima awe na sifa hizi 1.Upendo,tuwe tunapendana 2.Tunafaana,yani mtu ambae utu wake,mitazamo,imani na malengo yanafanana au kukarbiana sana 3.Anayemtanguliza Mungu.Baada ya kutambua hayo nikajua mapenz ya kwel hayalazmishwi japo upendo wa dhati unaweza kukutana na changamoto zinazoweza kufanya penzi life(Umbali,uchumi etc),yan jitahada za wote znahtajka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom