Mwinyi na changamoto ya maji Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
732
475
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameigiza Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuhakikisha changamoto iliyojitokeza ya ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo ya Mji wa Zanzibar inapatiwa ufumbuzi wa haraka ili wananchi waendelee kupata huduma hiyo ipasavyo.

Dk. Mwinyi ametoa agizo hilo leo wakati alipotembelea na kukagua vyanzo vya Mradi wa Maji unaopeleka huduma hiyo Mjini Zanzibar ambapo miundombinu yake imeharibika na kusababisha kukosekana kwa huduma hiyo katika maeneo mbali mbali ya Mji wa Zanzibar kwa takriban siku nne sasa.

Rais Dk. Mwinyi aliwataka watendaji wa ZAWA kuongeza kasi katika utatuzi wa changamoto za maji zinazoukabili mji, akibainisha matumaini yake baada ya baadhi ya vifaa, ikiwemo mabomba kuwasili.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameitaka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kutengeneza mfumo utakaowawezesha wananchi wa maeneo ya Miwani, Kizimbani na Bumbwisudi kupata huduma za maji kupitia Mradi wa Maji safi na salama unaopeleka huduma hiyo Mjini Zanzibar.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom