Mwinyi awataka watendaji Serikalini kuwa na mbinu mpya za kuingiza mapato

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka watendaji wa Serikali kuwa wabunifu na kuja na njia mbadala ya kutafuta fedha nje ya Bajeti ya Serikali, ili kufanikisha utekelezaji wa mipango ya Serikali.

Dk. Mwinyi amesema hayo katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Upangaji wa Vipaumbele, yalioandaliwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Tony Blair pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), yanayofanyika Chuo cha Utalii Maruhubi.

Amesema Serikali imekuwa ikishindwa kutekeleza vyema mipango yake ya maendeleo kutokana na watendaji wa taasisi kutokuwa na utamaduni wa kutayarisha maandiko ya miradi (project write-ups), hata kwa miradi ambayo Mashirikia ya Kimataifa hutoa misaada kwa nchi mbali mbali na hivyo kubaki zikiwa tegemezi.

Alisema katika kipindi hiki ambapo makusanyo ya Serikali yameshuka kwa kiasi kikubwa kutokana na athari za maradhi ya UVIKO -19, viongozi wa taasisi wamekuwa wakilalamika kwa kutokuingiziwa fedha na Serikali, bila wao kuja na mbinu nyingine ya kuzitafuta.
 
Back
Top Bottom