Mwinyi ataka Mahakama itoe haki bila kuingiliwa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,682
149,886
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ameitaka Mahakama kutoa haki kwa wakati bila kuingiliwa na chombo chochote, au mtu yeyote ili kuifanya iweze kuaminiwa na wananchi.

Mzee Mwinyi maarufu Mzee Ruksa, alitoa rai hiyo jana wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria na Utoaji Elimu ya Sheria, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu ya “Umuhimu wa utoaji haki kwa wakati, kuwezesha ukuaji wa uchumi”, yatafikia kilele Februari 2 yakiashiria kuanza mwaka wa Mahakama.

Katika hotuba yake, alisema ili Mahakama itende haki kwa wakati, lazima ishirikiane na wadau wote ili kuleta ufanisi.

Alisema huo ndiyo msingi wa amani, na utulivu na ndiyo msingi wa maendeleo.

Awali, Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahimu Juma alisema sheria ni kitu muhimu katika maisha ya jamii na hakuna nyenzo nyingine yoyote inayowezesha mtu kuishi katika jamii zaidi ya sheria.


Chanzo: Mwananchi
 
Ndio kazi ya mahakama, kutafasiri sheria na kutoa haki! Kama inaingiliwa hakuna haja ya kuiita mahakama!
 
Ila kwa awamu Sheria imelekezwa kwa wale wanaokosoa selikari na wapinzani apa lazima wawe makini ukikutwa na hatia nikifungo tena bila fini
 
Mzee Mwinyi ameona mbali sana ni kweli kabisa kwa sasa kwa asilimia kubwa kesi mahakama hawatendi haki wanafanya maamuzi kwa maagizo tumeshuhudia ukandamizaji mkubwa wa sheria umefanyika kwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema kuendelea kukaa mahabusu zaidi miezi mitatu sasa kwa sababu dhamana yake imezuiwa. Huyo ni Mbunge anafanyiwa hivyo je wewe mwananchi wa kawaida itakuwaje ???
 
Ni Tanzania mahakama zinafanya kazi kwa maelezo ya mtu mmoja nampongeza sana Mzee Mwinyi kwa kusema ukweli mahakama zinatakiwa kutendeka haki bila kuingiliwa.
Utawala wa Mtukufu hakuna haki mahakamani kabisa hata Viongozi wa siasa imekula kwao
 
Back
Top Bottom