Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,180
- 664
Mwinyi: Niliweka misingi bora vyama vingi
Na Ali Suleiman, Zanzibar
RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Bw. Ali Hassan Mwinyi, amesema katika kipindi cha uongozi wake, alifanya kazi kubwa ya kuweka misingi bora katika mfumo wa vyama vingi kiasi cha kuwapo uvumilivu wa kisiasa nchini.
Alhaji Mwinyi alisema hayo juzi wakati akifungua kongamano la siku mbili la uvumilivu wa kisiasa lililotayarishwa na taasisi ya kibunge ya Amani Forum mjini hapa.
Alisema misingi hiyo aliyoiweka ndiyo inayofanya kazi na kulifanya Taifa hili na vyama siasa kuwa na siasa za kuvumiliana na za kistaarabu.
"Tunaweza kuwa na vyama vingi, si tatizo, lakini cha msingi ni kujenga tabia ya kuwa na siasa za kuvumiliana zitakazoendeshwa kwa njia ya kistaarabu," alisema.
Alisema utaratibu huo umekuwa ukivutia watu wengi wa mataifa jirani, kiasi cha kuonekana Tanzania kama moja ya nchi zilizokomaa katika siasa za vyama vingi.
Rais mstaafu Mwinyi ambaye ndiye aliyeanzisha mchakato wa Tanzania kuingia katika mageuzi ya mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992, aliwataka Watanzania kuendeleza utamaduni wa kuvumiliana na kuheshimiana.
Alisema siasa si ugomvi wala vurugu, lakini ni utaratibu tu unaokubalika katika kupata viongozi kwa njia ya amani na utulivu.
Kongamano hilo liliwakutanisha viongozi mbali mbali wa kisiasa nchini, wakiwamo wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka vyama vya CCM na CUF na viongozi wa vyama vya siasa nchini, lilijadili mada mbali mbali zikiwamo siasa za kuvumiliana na njia za kuepuka migogoro.
Miongoni mwa kazi za taasisi ya Amani Forum, ni kujaribu kuipatia ufumbuzi migogoro mbali mbali katika nchi za Maziwa Makuu Afrika na kusimamia uchaguzi mbali mbali nchini.
source majira