Mwinjilisti amtaka Maalim Seif kujiuzulu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwinjilisti amtaka Maalim Seif kujiuzulu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kadogoo, Jan 9, 2012.

 1. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  KUFUKUZWA KWA HAMAD RASHID KUMEINGIA KTK HATUA MPYA KWA MHUBIRI WA DINI YA KIKRISTO KUGUSWA NA HATUA YA CUF YA KUMFUKUZA MHESHIMIWA H.RASHID MBUNGE WA WAWI PEMBA HABARI KAMILI SOMA HAPA:

  na Christopher Nyenyembe, Mbeya

  Kutoka mkoani Mbeya, Mhubiri na Mwinjilisti wa kimataifa wa kanisa la Penuel Healing Ministry la Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam, Alphonce Temba, ametamka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ajiuzulu wadhifa huo kwa kuwa ameshindwa kukisimamia vyema na kukifanya kiendelee kupoteza umaarufu wake.

  Mwinjilisti Temba alisema jijini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Mbeya Peak akitokea katika ziara ya muda mrefu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC) alikokwenda kumuombea Rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila, amani ili uchaguzi huo uwe wa amani.

  Alisema kuwa ameguswa na vyama viwili vya CCM na CHADEMA kuwa ndivyo vyenye uwezo wa kuleta mabadiliko Tanzania na kuweza kushika dola lakini sio CUF chini ya uongozi wa Maalim Seif kwa madai kuwa kinaendelea kupoteza umaarufu wake.

  "Namshauri Maalim Seif kama anaitakia mema CUF aachie ngazi ya ukatibu mkuu maana huyu ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kitendo chake cha kuendelea kung'ang'ania nafasi hiyo kinakidhoofisha chama hicho kilichokuwa na upinzani mkubwa dhidi ya CCM lakini sasa hivi hakina nguvu tena," alisema Mwinjilisti Temba.

  Alidai kuwa wadhifa wa Makamu wa Rais umemfunga zaidi kutekeleza majukumu yake ya kichama na hivyo kuwa kikwazo kwa wenzake wanaotaka kuendesha mapambano ya kisiasa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi na sio kujinufaisha wenyewe.

  "Ndugu zangu napenda niwaambie kuwa haya yote nayasema kwa kuwa Watanzania wamechoka kuongozwa na vyama vya mifukoni, vyama vingine vya siasa vimekuwa kama miradi ya watu-ni kampuni," alisema Temba.

  Mwinjilisti huyo alisema uamuzi wa kumtimua uanachama, Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, na wenzake watatu kuwa hakitofautiani na ule wa NCCR-Mageuzi wa kumvua uanachama, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, uliowanyima haki wananchi waliomchagua mbunge huyo.
  "Haiwezekani wabunge wanachaguliwa na wananchi kisha wanafukuzwa na watu wasiozidi 30 wanaokaa kwenye hoteli jijini Dar es Salaam kumvua ubunge mtu ambaye hawakumchagua wao," alisema Mwinjilisti Temba.

  Uamuzi wa kiongozi huyo wa kidini kutoka dhehebu la jijini Dar es Salaam umekuja baada ya kuibuka kwa mgogoro mkubwa wa kiuongozi kati ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, na Mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohamed uliosababisha, mbunge huyo avumiliwe uanachama.

  kutoka Tanzania daima

  JAMANI CUF KILIITWA CHAMA CHA WAISLAMU NA WAVAA VIKOFIA SASA MIMI NAMSHANGAA HUYU PADRE KUDAI KUWA CUF KIMEPOTEZA UMAARUFU WAKE ILA ANAKISIFIA CCM NA CHADEMA HUU SIO UNAFIKI?
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  wewe ni mpotoshaji na mwongo mkubwa kabisa, kwenye heading umeandika padri lakini habari hii imeandika ni mchungaji

  mods naomba mrekebishe heading isomeke mchungaji

  thanks
   
 3. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  NINI TOFAUTI YA PARE NA MCHUNGAJIi?
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo unaandika tu bila kujua tofauti?
  :focus:
  huyo mchungaji aache kuingilia mambo ya ndani ya chama, labda angewakemea uchu na tamaa ya madaraka. akemee ongezeko la posho na mengineyo yenye kuigusa jamii zaidi maana kiini cha mgogoro wa ndani ya chama hakuna ajuae isipokua seif na hamad na wajumbe wengine tunasoma tantalila za magazeti tu huwezi kujudge(huo ndo mtazamo wangu lkn)
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Hivi mchungaji na padri ofisi zao kihuduma ni tofauti eeh?
  Makubwa!!
  .
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  heading imeshabadilishwa

  halafu hauko makini kabisa wewe hichi ulichoandika ni nini 'PARE' NA 'MCHUMGAIi'

  kama ulikuwa haujui tofauti kwanini umekurupuka kuja kupost kitu usichokijua

  very sorry, wewe ni mpotoshaji
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  FYI, UPADRI ni daraja katika utumishi wa mungu
   
 8. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  .
  Lete andiko la kuthibitisha maneko yako la sivyo tutakuhesabu mwongo. Kama padri ni daraja, mchungaji yeye ni nani? Ama mto wenye hilo daraja?
  .
   
 9. L

  LAT JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  a lazy folk,
   
 10. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  yale yale!! ionekane wakristo wanaingilia siasa.. tundelee tu na hizi chokochoko tutafika tu mnapopaota!!!!
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ni sawa na kufananisha na ugali na wali
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mods mbona mnakuwa mnatumika, Mbona mmefuta post yangu? Au kwa sababu nimetaja neno Padre?
   
 13. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  kumbe sababu unaijua halafu unauliza nini sasa!?
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Rev...Mchungaji, Padri..

  Bishop... Askofu.

  Sasa Mods wanapewa amri futa heading isomeke mchungaji nao kwa mapenzi wanafuta bila kufanya uchunguzi.

  Ebu tuambieni tofauti ya Mchungaji, Askofu na Padri.
   
 15. L

  LAT JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mabandiko ya kijinga na kipuuzii ili jf ionekane ya hovyo
   
 16. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  ...aache kuingilia mambo ya ndani ya chama, kukemea uchu na tamaa ya madaraka, kukemea ongezeko la posho....
  Hivi huo uchu na tamaa ya madaraka pamoja na ongezeko la posho si ni mambo ya vyama hayo?
  Ni nani Tanzania anahaki ya kujadili siasa...wanasiasa, wafanyakazi, wabunge...? Mimi nahisi kila mwananchi ana haki ya kujadili chochote kinachoihusu nchi yake, awe na nafasi yoyote katika jamii na liwe ni suala lolote la nchi. Kwa huyo Padri au mtu mwengine yeyote, awe mchungaji au shehe, mlala hoi au tajiri, mzoa taka au inginia, wote wana haki ya kuadili chochote.

  Binafsi ninakubaliana na huyo mwinjilisti kuwa si haki kuwafukuza wabunge waliochaguliwa na maelfu ya watu na kufukuzwa na watu wasiozidi 50.
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Wewe ndio mpuuzi uwa unaona hii JF ni mali ya mzee wako?
   
 18. L

  LAT JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  teh teh teh

  the leading architect of ignorance
   
 19. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  People..Kuna Tofauti na Padri, Mchungaji na Mwinjilisti..Hapa mtoa Mada amemsemea Mwinjilisti na Si mchungaji wala Padri...Mwinjilisti ni mtu anayehubiri neno la Mungu.na Mchungaji ni msimamizi mkuu wa Wakristo kwenye Eneo Fulani na anafundisha pia..Na padri ni anasimama kama mchungaji kwa njia tofauti kulingana na Dhehebu na Dhehebu..ukienda Anglican wana Padri lakini anaoa na ukienda Roman wana Padri lakini Haoni kabisa..Na wote ni watumishi wa Mungu..I have tried to explain....
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Reverend= Mchungaji, Padri..

  Period...
   
Loading...