Malafyale
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 13,813
- 11,126
MWINJILISTI wa Kanisa la Pentekoste la Mto wa Mbu, Jackson John ambaye alikuwa mmoja kati ya waliojeruhiwa kwenye mapigano baina ya
waumini wa madhehebu ya kiislamu na kikristo yaliyotokea Februari 24 wilayani Monduli amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na ndugu wa mwinjilisti huyo zinadai kuwa alifariki jana alfajiri katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Mapigano hayo yalitokea baada ya waumini wa kiislamu kuwashutumu Kiongozi wa Kanisa la Full Salvation Church, Mchungaji John Chenge (29) aliyekuwa akihubiri injili eneo la Comix kwa kukashifu dini ya kiislamu.
"Ndugu yetu kafariki, unajua alipigwa sana alitobolewa na misumari kwenye kifua hata kwenye macho. Amekufa kutokana na majeraha ya misumari aliyoyapata kwenye kifua ambako baadhi ya misumari iliichelewa kutolewa; alisema mmoja wa ndugu wa marehemu ambaye
hakupenda kutaja jina lake.
Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alikana kusikia taarifa hizo.
Kwanza nyinyi nani kawaambia mimi sina hizo taarifa, sijaletewa. Ndio nazisikia kutoka kwenu," alisema Kamanda Mpwapwa.
Katika mpigano hayo vitu mbalimbali viliharibiwa yakiwamo makanisa ya Angilikana na Pentekoste, shule ya Mama Anna na nyumba za wakazi wa Mto wa Mbu kwa kuchomwa moto.
Kutokana na vurugu hizo Jeshi la polisi linawashikilia watu kadhaa, akiwamo Bwanga Musa (54), Shaban Hassan (58), Gabriel Kamunya (45), Ana Sospeter (40), Rashid Mziray (29), Frank Mwenda (42) pamoja na Bakari Twalib (18).
Source:Gazeti la Majira March 04