Mwingine tena aliyetoka jela kwa msamaha wa Rais Magufuli amekamatwa akiiba ng’ombe Mkoa wa Pwani

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
1576214474562.png

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa.​

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linamshikilia Mustafa Malimi (25) ambaye juzi Desemba 9, 2019 alipata msamaha wa Rais Magufuli na kuachiwa huru kwa kosa la kuiba Ng'ombe mwenye thamani ya Shilingi milioni 1.2.

Akizungumza leo Desemba 12, 2019, Kamanda Wankyo amesema kuwa Mustafa alifanya kosa hilo Desemba 10 na jana Desemba 11, majira ya saa 4:00 asubuhi, maeneo ya Nero Magorofani, katika Wilaya ya Chalinze, walimkamata tena kwa kosa ambalo hapo awali lilimfunga miezi sita gerezani.

"Huyu juzi tu amepata msamaha wa Rais na tumemkamata tena muda mfupi baada ya kuachiwa huru, awali alikuwa ni mfungwa kwenye Gereza la Ubena na jana tumemkamata akiwa ameiba Ng'ombe na kosa la awali lililokuwa limemfunga ni la wizi wa Mbuzi na alihukumiwa miezi sita kwenda jela" amesema Kamanda Wankyo.

Kamanda Wankyo ameongeza kuwa Jeshi la Polisi bado linaendelea kumshikilia na baada ya hapo watampeleka mahakamani kwa kosa la wizi wa mifugo.
 
Mimi wakati naingia JF,nilishawahi kushauri huko gerezani wafundishwe ujuzi/skills mbali mbali zitazowasaidia once wakirudi uraiani...ndio maana wenzetu wanaita ' correction facilities...…..sio kukomoana..lol
 
Mimi wakati naingia JF,nilishawahi kushauri huko gerezani wafundishwe ujuzi/skills mbali mbali zitazowasaidia once wakirudi uraiani...ndio maana wenzetu wanaita ' correction facilities...…..sio kukomoana..lol
Sisi wataalamu wa Elimu huwa tunasema Elimu sio lazima mtu inatakiwa anuie kujifunza
 
Huwa wakiachiwa wanapewa pesa ya kuanzia maisha au wanaachiuwa kama ng'ombe, yani wanafunguliwa geti wanatoka?!
 
Back
Top Bottom