Mwingine auwawa Iringa

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,558
MAUWAJI HAYA YATISHIA USALAMA IRINGA MJINI....


Askari kanzu wakikata kamba ili kushusha mwili wa kijana Nico Chalela aliyokutwa amejinyonga kiaina huku akiwa amepiga magoti jambo ambalo halijapata kutokea kwa mtu kujinyonga kama hivi
Wananchi wakishuhudia maiti ya kijana huyo ikitolewa na polisi

Hapa askari polisi wakiwa wameishusha maiti hiyo kutoka katika kamba

Hapa ikiingizwa katika gari ya polisi

Hivi ndivyo alivyokutwa

MAUWAJI ya kinyama yazidi kutishia maisha ya wakazi wa manispaa ya Iringa baada mfanyakazi mmoja wa kituo cha kuziba pacha za magari katika eneo la Mshindo mjini hapa Nico Chalale (28) kukutwa amekufa kifo cha mashaka kwa kunyongwa shingo usiku wa kuamkia sikukuu ya Krismasi ikiwa ni siku moja baada ya kuchinjwa mfanyabiashara wa samaki Bukuri Mvula na watu wasiofahamika jirani kabisa na eneo hilo.

Kijana huyo alikutwa akiwa amefungwa kamba shingoni huku akiwa amepiga magoti hali inayozua maswali zaidi kwa wakazi wa mjini Iringa na kuingia na hofu zaidi ya kuwepo kwa mtandao wa watu wanaojihusisha na mauwaji hayo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wakazi wa eneo la Mshindo walisema kuwa kifo cha fundi huyo ambaye wili wake ulikutwa eneo la kazini kwake unawafanya kuingiwa na hofu zaidi na kuliomba jeshi la polisi mkoa wa Iringa kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya mauwaji hayo.

Wananchi hao walisema kuwa inasikitisha na kutishia uhai wao kuona watu wakiendelea kunyongwa na kuuwawa kinyama katikati kabisa na mji huo wa Iringa .

Kwani walisema kifo cha Chalale ni tukio la tatu kutokea ndani ya kipindi kifupi cha wiki mbili ambapo tukio la kwanza lilikuwa la aliyekuwa kamanda wa kampuni ya ulinzi binafsi ya Force Group marehemu Charlesy Tulo ambaye alikutwa amejinyonga katika mti mfupi unaokisiwa kuwa na futi kama tatu wakati yeye ana urefu wa fupi 5 .

Hata hivyo walisema mauwaji hao hayakuishi hapo kwani siku moja kabla ya Krismasi mfanyabiashara huyo wa samaki Mvulla alikutwa akiwa amechinjwa shingo kama kuku na mwili wake kutelekezwa ndani ya daladala mbovu.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla ametihibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi .

MWISHO

Source: Francis Godwin ni mzee wa matukio daima
 
Mkuu siku hizi saa moja niko Ndani. Yaani ni hatari tupu
 
Back
Top Bottom